Waziri Ummy, Usipotoshwe maamuzi yako kuhusu ADDO na wafamasia mtawaumiza Watanzania

Mwamba ngoma huvutia kwake.

Mwambie MD atengeneze dawa km ataweza.
 
Unaonekana kuwamburura kuliko unayemponda.
 
Bora wameifuta hiyo ADDO maana haingii akilini eti MD haruhusiw kuuza dawa mpaka awe na cheti cha ADDO wakat pharmacology yote ipo kichwan,tena mbaya Zaid unakuta Baadhi ya watu wanaopewa hiyo ADDO wengine ni form 4 failures.
Mkuu, siyo swala la "pharmacology yote yote kuwa kichwani"; pamoja na kwamba hilo siyo kweli, lakini kuna sababu muhimu zaidi inayozuia hilo. Conflict of Interest, pande zote mbili.

Mfamacia asianze kutoa dawa tu hata kama anajua tatizo la mgonjwa, na hivyo hivyo, daktari naye atakuwa na conflict of interest kama atakuwa ni yeye yule yule anayeshughulika na sehemu zote mbili, kuona mgonjwa na kutoa/kumiliki dawa.
 
Umejikita kumkosoa prof bila kupiga hoja zake

Mi sio mtu wa afya ila nilitaman kupata ukweli kuhusu machache ambayo prof ameaninisha
1. Mfamasia hasomei kuhusu magonjwa chanzo na dalili zake je ni kweli? Na kama kweli

Basi mfamasia hawezi kuwa mtu sahihi hapo

Maana ni ukweli nurse anasomea hayo na dr wake

Hoja hii binafs nahitaji majibu yake
Asante mtaalamu
 
Kwenye chumba cha upasuaji unahusika na nini?
 
Upo sahihi
 
Mfamasia kazi yake siyo kutambua magonjwa, kazi yake ni dawa, sehemu zote zinazohusu dawa. Sijui kama kuna sehemu yoyote Tanzania Famacia anapolilia kuwa mtaalam wa magonjwa. Hiyo ni kazi ya wengine. Mfamasia anasomea dawa jinsi inavyofanya kazi mwilini mwa binaadam, magonjwa inayotibu, utengenezaji wa dawa hiyo, utunzaji wa dawa kufuatana na mazingira ya dawa yenyewe,kama ni kuwa kwenye ubaridi ili isiharibike au vinginevyo, n.k., n.k..

Lakini hata hivyo, kumbuka, katika kumtibu mgonjwa, kazi hiyo siyo ya mtu mmoja, ingawaje imekuwa ikifahamika hivyo tokea zamani kimakosa.

Mgonjwa anahudumiwa na timu, jopo la watu mbalimbali. siyo kazi ya daktari pekee. Hii ndiyo maana inatakiwa pawepo na ushirikiano katika utendaji wa kazi wa watu hawa.

Unaposema "Maana ni ukweli nurse anasomea hayo na dr wake" una maana gani? Nurse anasomea kazi yake, na anafanya kazi yake, hafanyi kazi ya daktari. Daktari hana nurse wake. Hawa ni watu wawili tofauti, kila mmoja anayo kazi yake na wanategemeana.
 
Kwenye chumba cha upasuaji unahusika na nini?
Kwani huko yupo daktari peke yake?
Na unajua kuna dawa ngapi zinazotumika huko kiasi cha kulazimu kila mtu awepo huko? Mazingira yenyewe ya sehemu hiyo yanalazimisha pasiwepo na utitiri wa watu hata kama ingetakiwa kuwe na kila mtaalam husika na kila jambo.

Kwa maana ya swali lako, una maana ni madaktari wote wanakuwepo kwenye vyumba vya upasuaji?
 
Wadaktri njaa wanataka kuhodhi kila kitu wao..hadi kazi yao ya msingi ya kutibu wagonjwa wameiacha..sasa wanakimbilia vyeo na pesa.

Kila kwenye pesa wanataka waingie wapige..

Nawaonya madaktari fanyeni kazi zenu za msingi..sio kuingilia kila seheme..

Ndio mana sekta ya afya nchini haisongi..ikedumazwa na madaktari wachumia tumbo.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda we ndo umepitwa na wakat
 
Jamaa alichoandika ni kweli, anayetoa dawa kwa mgonjwa ni Nurse au Dr na sivinginevyo may be tupate uzoefu kwa nchi zilizoendelea kama Kenya
 
Nimjuavyo Waziri Ummy...usikute kishakasirika kupewa ushauri huu uliokwenda shule.
 
Hakuna university Teaching hospital nchini ndiyo tatizo kubwa kwetu hapa.Wabunge hawana ulewa nini maana ya hospital ya mloganzila kujengwa?

Tujenge university Teaching hospital nchini , Tutapata wanataaluma wa uhakika siyo kama ilivyo sasa. Maprofesa wote hawafundishi tena mawodini baada ya kuishusha hazi hospital ya mloganzila.

Chonde waziri iweke hospital mloganzila under Muhas tusikilize masomo kutoka Teaching univesities duniani.
 
👍
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…