Binafsi nimefurahishwa na jinsi Waziri wa Afya alivyoanza kazi.
Anaonekana mtu mwenye kuelewa wizara yake inavyofanya kazi, ina changamoto zipi na ana dira ya maboresho yanayohitajika kuleta tija.
Amekuwa tofauti na Mawaziri wengi ambao wanaonekana kufanya kazi sio kwa kuelekeza nini kifanyike bali wao kutumia ukali tu kama kutumbua watumishi wa chini na kufanya ziara tu.
Leo nimemsikiliza akitoa maelekezo ya kufanyia matengenezo vifaa, juzi nilimsikia akielekeza wataalamu kujihusisha na maboresho ya kanuni, n.k.
Kwa kweli mpaka raha sana.
Tunajua kuwa awamu ya Tano ilitakiwa kuanza na Serikali yenye ukali ili kubadili mindset za watanzania ambao bila shaka wangeng'ang'ania mazoea. Hilo limefanyika kwa mafanikio makubwa sana ndani ya miaka 5 ya kwanza lakini sasa kuendeleza ukali tu bila viongozi kutoa miongozo na maelekezo sahihi yenye kulenga kuongeza tija.
Mfano mimi leo ukiniambia nimtumbue waziri mmoja Tu, nitasema kwa haraka bila kusita kuwa "WAZIRI WA ARDHI NA MAENDELEO YA MAKAZI" atumbuliwe leo hii.
Kazi ya msingi ya wizara hii ni kuweka utaratibu mzuri wa makazi ambao utaboresha maisha ya watanzania.
Utaratibu wa makazi utakaowekwa na wizara hii ndiyo utakaopelekea watanzania kupata huduma kwa urahisi au kwa shida, maji, umeme, huduma za hospitali, shule, usafiri n.k
Wizara hii kwa sasa inatazama ukusanyaji wa kodi na kutatua migogoro ya ardhi.
Hebu chukulia mji wowote ule, chukua aerial view picture, utagundua labda makazi katika miji yetu yamechukua only 50% na 50% ni mapori ndani ya miji. Ukitaka kuwapatia umeme hawa wakazi unahitaji kutandaza mtandao wa bomba 50% extra kuliko mahitaji halisi. Ukitaka kuwapa umeme, unatandaza huduma hii kwa 50% extra. Kutokana na bajeti yetu ya kutoa huduma za jamii kuwa ndogo tunajikuta watu wengi mijini wanaishi maisha yao bila huduma za msingi kwa uzembe unaoanzia wizara ya makazi.
Yaani kama wizara ya makazi ingekuwa na makini, wakatunga sheria za makazi zinazozuia mtu kutunza ardhi katikati ya mji isipokuwa taasisi za umma tu, kila mtu anunue kiwanja anapotaka kujenga na mwenye kiwanja asichotumia analazishwa kuuza, tukaondoa mapori katikati ya miji huduma za kijamii zisingekuwa shida.
Ni sawa na mtu aliyetakiwa kuweka utaratibu kwamba wakati wa kula watu wote wakusanyike dining room, akaacha kuweka utaratibu na kila mtu amekaa kivyake na kupelekea mwenye dhamana ya kuwapa chakula kulazimika kumfuata kila mtu alipo. Unaweza kuona mda hautoshi, vifaa havitoshi kumbe ni jambo dogo tu la kuwaweka pamoja.
Leo hii tunajigamba umeme utafika vijiji vyote by 2025, lakini ukitazama watu wa vijijini wanavyokaa unajiuliza tunachokifanya ni kitu gani?
Ni kwa nini wizara hii ya makzi isibuni mpango wa makazi vijijni kwamba kila kijiji kinakuwa na center ya makazi na wanaenda kulima mashambani. Kwenye senta maji yakifika tuna uhakika kila mwanakijiji anaweza kupata maji, umeme ukifika kila mwanakijiji anaweza kupata umeme, shule, vituo vya afya vinakuwa hapa na wanatoka kwenda kulima mashambani.
Lakini hakuna udhibiti wowote wa makazi, popote unapofika unaanzisha makazi iwe mjini au kijijini na wenye dhamana ya huduma tofauti wananza kuhangaika kutafuta jinsi gani wakufikishie huduma pale ulipoamua kukaa. Cha msingi kwa wizara hii ni wewe kulipa kodi maana wanahalalisha squatter ili zilipe kodi.
Sijasema waliojenga holela wabomolewe bali ninasema wizara hii ichore mstari kwamba miji yetu imevurugika vya kutosha kuanzia hapa tunataka twende mbele kwa kila mtanzania anayenga leo kufanya kitu sahihi na wote waliofanya makosa huko nyuma tunawapa mda mfano miaka 10 kurekebisha ili miaka 10 ijayo tuwe na miji bora na tuwe na vijiji bora.
Dk Gwajima anaonyesha njia na hawa wengine waige au mkulu atuletee wa design ya Gwajima wenye dira katika sekita zao