Bima ya Afya yenyewe ishakuwa UTOPOLO.Kumshawishi mwananchi aliyepo hapa MABAREGERA awe na bima ya afya, ni matumizi mabaya ya akili sababu hata hata akiugua, dawa ya malaria haipatikani zahanati za serikali.
Sasa bima ya afya ya nini sababu dawa lazima utaenda kununua duka la dawa.
Yote kwa yote wanasiasa wote wapo vizuri sana sababu wanashibisha matumbo yao ipasavyo.
Huyo mama kaanza vyema. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni ngoja tusubiri siku zijazo
Ni lazima tubaki kwenye jukumu la msingi la wizara ni nini? na tutazame je jukumu hilo linatekelezwa?Ungejua lukuvi alivyoipambania hiyo wizara iliyokuwa imejaa wezi wa viwanja usinge sema
Baada ya ufisadi jambo ambalo wananchi wengi wanyonge walilililia ni ardhi
Leo hii watu wanauziana viwanja vidogo sana, mtu akijenga nyumba kiwanja kimeisha hana hata pa kuchimba choo, nani nayewajibika kuweka utaratibu kuwa size ya chini ya kiwanja mjini ni hii?Ungejua lukuvi alivyoipambania hiyo wizara iliyokuwa imejaa wezi wa viwanja usinge sema
Baada ya ufisadi jambo ambalo wananchi wengi wanyonge walilililia ni ardhi
Leo hii watu wanauziana viwanja vidogo sana, mtu akijenga nyumba kiwanja kimeisha hana hata pa kuchimba choo, nani nayewajibika kuweka utaratibu kuwa size ya chini ya kiwanja mjini ni hii?
Leo hii kuna watu binafsi wameshikilia ardhi ekari mbili katikati ya mji na wanapewa hati? hiki ni kiwanja au ni shamba mjini? nani aseme maximum size ya kiwanja mjini ni hii?
viwanja watu wanauziana havina barabara, na mnunuzi ndiye anakuja kuhangaika kutafuta njia, wengine wanaanza kwa kukatiza katikati ya viwanja vya wengine na kuchukulia ndiyo barabara na baadae wenye viwanja wakifunga barabara inazua migogoro maana watu wanaona kama wanafungiwa njia.
yaani makazi hayana muongozaji
Mleta mada hujui lolote, umeandika kusifia badala ya kuchimbua uhalisia.Binafsi nimefurahishwa na jinsi waziri wa afya alivyoanza kazi.
Anaonekana mtu mwenye kuelewa wizara yake inavyofanya kazi, ina changamoto zipi na ana dira ya maboresho yanayohitajika kuleta tija.
Amekuwa tofauti na mawaziri wengi ambao wanaonekana kufanya kazi sio kwa kuelekeza nini kifanyike bali wao kutumia ukali tu kama kutumbua watumishi wa chini na kufanya ziara tu.
Leo nimemsikiliza akitoa maelekezo ya kufanyia matengenezo vifaa, juzi nilimsikia akielekeza wataalamu kujihusisha na maboresho ya kanuni, n.k.
Kwa kweli mpaka raha sana.
Tunajua kuwa awamu ya Tano ilitakiwa kuanza na serikali yenye ukali ili kubadili mindset zaq watanzania ambao bila shaka wangeng'ang'ania mazoea. Hilo limefanyika kwa mafanikio makubwa sana ndani ya miaka 5 ya kwanza lakini sasa kuendeleza ukali tu bila viongozi kutoa miongozo na maelekezo sahihi yenye kulenga kuongeza tija.
Mfano mimi leo ukiniambia nimtumbue waziri mmoja Tu, nitasema kwa haraka bila kusita kuwa "WAZIRI WA ARDHI NA MAENDELEO YA MAKAZI" atumbuliwe leo hii.
Kazi ya msingi ya wizara hii ni kuweka utaratibu mzuri wa makazi ambao utaboresha maisha ya watanzania.
Utaratibu wa makazi utakaowekwa na wizara hii ndiyo utakaopelekea watanzania kupata huduma kwa urahisi au kwa shida, maji, umeme, huduma za hospitali, shule, usafiri n.k
Wizara hii kwa sasa inatazama ukusanyaji wa kodi na kutatua migogoro ya ardhi.
Hebu chukulia mji wowote ule, chukua aerial view picture, utagundua labda makazi katika miji yetu yamechukua only 50% na 50% ni mapori ndani ya miji. Ukitaka kuwapatia umeme hawa wakazi unahitaji kutandaza mtandao wa bomba 50% extra kuliko mahitaji halisi. Ukitaka kuwapa umeme, unatandaza huduma hii kwa 50% extra. Kutokana na bajeti yetu ya kutoa huduma za jamii kuwa ndogo tunajikuta watu wengi mijini wanaishi maisha yao bila huduma za msingi kwa uzembe unaoanzia wizara ya makazi.
Yaani kama wizara ya makazi ingekuwa na makini, wakatunga sheria za makazi zinazozuia mtu kutunza ardhi katikati ya mji isipokuwa taasisi za umma tu, kila mtu anunue kiwanja anapotaka kujenga na mwenye kiwanja asichotumia analazishwa kuuza, tukaondoa mapori katikati ya miji huduma za kijamii zisingekuwa shida.
Ni sawa na mtu aliyetakiwa kuweka utaratibu kwamba wakati wa kula watu wote wakusanyike dining room, akaacha kuweka utaratibu na kila mtu amekaa kivyake na kupelekea mwenye dhamana ya kuwapa chakula kulazimika kumfuata kila mtu alipo. Unaweza kuona mda hautoshi, vifaa havitoshi kumbe ni jambo dogo tu la kuwaweka pamoja.
Leo hii tunajigamba umeme utafika vijiji vyote by 2025, lakini ukitazama watu wa vijijini wanavyokaa unajiuliza tunachokifanya ni kitu gani?
Ni kwa nini wizara hii ya makzi isibuni mpango wa makazi vijijni kwamba kila kijiji kinakuwa na center ya makazi na wanaenda kulima mashambani. Kwenye senta maji yakifika tuna uhakika kila mwanakijiji anaweza kupata maji, umeme ukifika kila mwanakijiji anaweza kupata umeme, shule, vituo vya afya vinakuwa hapa na wanatoka kwenda kulima mashambani.
Lakini hakuna udhibiti wowote wa makazi, popote unapofika unaanzisha makazi iwe mjini au kijijini na wenye dhamana ya huduma tofauti wananza kuhangaika kutafuta jinsi gani wakufikishie huduma pale ulipoamua kukaa. Cha msingi kwa wizara hii ni wewe kulipa kodi maana wanahalalisha squatter ili zilipe kodi.
Sijasema waliojenga holela wabomolewe bali ninasema wizara hii ichore mstari kwamba miji yetu imevurugika vya kutosha kuanzia hapa tunataka twende mbele kwa kila mtanzania anayenga leo kufanya kitu sahihi na wote waliofanya makosa huko nyuma tunawapa mda mfano miaka 10 kurekebisha ili miaka 10 ijayo tuwe na miji bora na tuwe na vijiji bora.
Dk Gwajima anaonyesha njia na hawa wengine waige au mkulu atuletee wa design ya Gwajima wenye dira katika sekita zao
Umemaliza kila kitu.Mawaziri wengi wanaosifiwa siku hizi ni wale wanaijifanya kufanya kazi za Katibu mkuu wa Wizara
Kazi kubwa za Waziri ni za kisera sio za kufuatilia Register ya Wagonjwa haijajazwa na mfano wa hizo
Wengi ni show off, ukiwafuatilia kiutendaji wanaondoka hawajaacha legacy yoyote,
Kigwangala na style yake ya kufungia geti wachelewaji au kurusha kichura chura Askar wa wanyamapori ilileta athari gani, au mbwembwe za Kangi Lugola?
kuna Waziri Sijui Luhaga Mpina alikuwa anafunga safari yeye na msafara wa Maafisa kwenda Kanda ya Ziwa kuchoma nyavu za Wavuvi eti zina matundu madogo mara sijui kutembea na tape ya kupima urefu wa samaki huku wakiacha maduka yanayouza hizo nyavu yakiendelea na biashara kama kawaida yakiwa na leseni na mzigo huo umepita bandarini umekaguliwa na kulipa tozo zote za kisheria
Waziri anatakiwa kuwaza na ku act globally kisera na kimuundo, akiona kuna tatizo lazima atathmin na kujua chanzo kisha kutafuta suluhu kama ni kuboresha sera, muundo au sheria!
Bongo ukianza kuzurula kutwa kucha unapiga kelele tu kwenye media kwa matamko uchwara ndio unaonekana unachapa kazi balaa.Umemaliza kila kitu.
Huo ndio ukweli.
Waziri sio kuropoka, kuzurura na vyombo vya habari na kutafuta umaarufu binafsi. Hawa akina Kigwangwalla, Gwagima ni watu wa ovyo sana. They have nothing to deliver rather than attention seeking.
Good commentMawaziri wengi wanaosifiwa siku hizi ni wale wanaijifanya kufanya kazi za Katibu mkuu wa Wizara
Kazi kubwa za Waziri ni za kisera sio za kufuatilia Register ya Wagonjwa haijajazwa na mfano wa hizo
Wengi ni show off, ukiwafuatilia kiutendaji wanaondoka hawajaacha legacy yoyote,
Kigwangala na style yake ya kufungia geti wachelewaji au kurusha kichura chura Askar wa wanyamapori ilileta athari gani, au mbwembwe za Kangi Lugola?
kuna Waziri Sijui Luhaga Mpina alikuwa anafunga safari yeye na msafara wa Maafisa kwenda Kanda ya Ziwa kuchoma nyavu za Wavuvi eti zina matundu madogo mara sijui kutembea na tape ya kupima urefu wa samaki huku wakiacha maduka yanayouza hizo nyavu yakiendelea na biashara kama kawaida yakiwa na leseni na mzigo huo umepita bandarini umekaguliwa na kulipa tozo zote za kisheria
Waziri anatakiwa kuwaza na ku act globally kisera na kimuundo, akiona kuna tatizo lazima atathmin na kujua chanzo kisha kutafuta suluhu kama ni kuboresha sera, muundo au sheria!