Waziri wa Afya, Dkt. Gwajima anafurahisha na kuonesha aina ya viongozi nchi yetu inahitaji

Mimi nisichokielewa ni hawa wanaoitwa shirika la nyumba, hawa jamaa hawana ubunifu wowote, mi naona hawa wanafanya kazi ya kukusanya na kulipana mishahara.
Hawa jamaa Walitakiwa wajenge nyumba za bei nafuu za kutosha kwenye kila wilaya ili watu wapange. Hizi za kununua wanunue wenyewe hatuna uwezo nazo. Hii ingesaidia hata kwenye mpangilio mzuri wa miji.
 
Vyumba viwili na jiko, choo, Vyoo, sitting na dining walinambia 136 M, nikawatukana kimoyo moyo nikaondoka
 
Kweli mtupu
 
Sijasoma uzi wako ila huyo wazir ana mihemko mingi rafiki popote. Hajui hata changamoto za idara. Ananikumbusha speech za nchemba wakati anatangaza nia 2015.zilijaa story za Ds first year UDSM
 

Media itamuangusha huyu mama
 
Unajua wanasiasa wanachekesha kweli.
Changamoto zilizopo kwenye afya kwa asilimia 90 zinasababishwa na serikali kuu.
Huwezi amuru hospitali zizalishe vifaa vya hospitali wakati bajeti yu ya kuendesha hospitali haitoshi
 
Hilo ndilo tatizo maana huelewi primary objective ya kupanga mji ni nini?

Miaka ya 70 mwalimu nyerere alileta vijiji vya ujamaa, hivi unajua sababu ilikuwa ni nini? Yaani wataalamu wa kale walielewa umuhimu wa watu kukaa pamoja ili wahudumiwe, leo hii tuna wasomi wengi lakini argument zao ni hizi za kwani mtu akimiliki hekari 2 katikati ya mji analipa kodi kuna ubaya gani?

Unachokitazama ni kodi na hii ndiyo vission ya wizara kuwa provided mtu analipa kodi hakuna shida shida.

Jukumu ya la msingi la wizara ya ardhi na maendeleo ya makazi sio kukusanya kodi za rdhi.

Ni kwamba miji ni usanyiko wa watu wenye makuzi tofauti, tamaduni tofauti, fikra tofauti na haya yanapelekea kila mtu kutaka kuishi kwa fikra zake. Kuna mwingine amekulia maisha ya ukulima atataka alime katikati ya mji, kuna mwingine akulia mazingira ya ufugaji atataka afuge mjini, kuna mwingine amekulia mila za kutotumia chooo hivyo atataka kujisaidia vichakani n.k

Moja ya majukumu ya wizara hii ni kuwaambia wakazi wa mijini kuwa hapa unapoingia, tamaduni zako, makuzi yako, fikra zako mwisho wake ni huko ulikotoka na hapa utaratibu wa kuishi ni huu. Kama huko kwenu hamjisaidi kwenye vyoo, sisi hapa ni sharti kila nyumba kuwa na choo chenye sifa hizi.

Inawezekana wewe ni mkulima lakini hapa mjini unaruhusiwa kulima maua, kupanda miti na bustani ndogo tu.

Kikubwa mijini serikali inawajibika kuwafikishia wananchi wake huduma za kijamii kama shule, hospitali, barabara, maji, umeme.

sasa hivi vitu vinatolewa kwa urahisi kwa watu waliokaa pamoja na ukaweka utaraibu wa wao wakaeje ili wapate huduma hizo.
 
Atoe ufafanuzi kwanini Mloganzila siyo Teaching university Hospital? Tunapitwa hadi na Uganda?
 
Best comment of year 2020. Waziri alizoea Kuwa pelekesha watumishi wa tamisemi unadhani na wizarani itakuwa hivyo hivyo .maslahi ya watumishi wa afya yapo hoi bin taabaan wao wanataka tu natokeo
 
Acha wivu mdogo mdogo lukuvi anafanya kazi kubwa sana waambie waliokutuma kumchafua kua imebuma...au umechukuliwa ardhi yako ulioipata kifisadi??
 
Ungejua lukuvi alivyoipambania hiyo wizara iliyokuwa imejaa wezi wa viwanja usinge sema

Baada ya ufisadi jambo ambalo wananchi wengi wanyonge walilililia ni ardhi
Mwambie huyu taga mwenzio,LOOK V,alijitahidi kiasi chake.
 
Kabla ya kuteuliwa si alikua katibu wa afya....ni dhahiri atakua anaijua vizuri wizara ya afya
 
Umemaliza kila kitu.
Huo ndio ukweli.
Waziri sio kuropoka, kuzurura na vyombo vya habari na kutafuta umaarufu binafsi. Hawa akina Kigwangwalla, Gwagima ni watu wa ovyo sana. They have nothing to deliver rather than attention seeking.
Ndio maana siku hizi hawa wengine wa chini hawasikiki kabisa yaani ni mwendo wa mawaziri kupiga show off
 
Acha wivu mdogo mdogo lukuvi anafanya kazi kubwa sana waambie waliokutuma kumchafua kua imebuma...au umechukuliwa ardhi yako ulioipata kifisadi??
Hii tunaita layman's comment.

Bado narudia kazi ya waziri wa ardhi ambayo ni namba moja ni kuweka utaratibu wa makazi, kitu ambacho hakipo.

Kila mtu anaishi anavyotaka.

Kazi yake kubwa ni kuweka utarartibu ambao
1. unarahisisha maisha kwa wakazi
2. unaondoa migogoro kwa wakazi
3. unajali usalama kwa wakazi
4. unamhakikishia afya kila mkazi.

Yeye akiweka utaratibu akagawa hati za makazi ni kazi ya tra kuhangaika na wakazi walipe kodi za ardhi.

lakini kwa sababu waziri wa ardhi hatimizi majukumu yake, inakuwa vigumu kwa TRA kudai kodi za radhi kwa sababu hawa jamaa hawajatengeneza mfumo ambao unawawezesha TRA kujua sehemu fulani kuna makazi haya na ninaweza kuwadai hivi. Ili kuonekana wanafanya kazi ni waziri wa ardhi mwenyewe kudai kodi za ardhi.

Serikali inatumia fedha kubwa kutekeleza miradi ya kijamii kama umeme, huduma za maji n.k.

Hawa jamaa wanaotoa huduma hizi tutawalaumu kila siku maana hawana plani yoyote workable. Ili mtoa huduma za maji mfano atengeneze master plan za maji katika miji, kuwa mtaa fulani nitapeleka bomba la maji la saizi fulani na mtaa fulani nitapeleka bomba la maji saizi fulani, ni lazima ajue mtaa huo utakuwa na watu wangapi? ajue mpangilio wa makazi ukoje. Yote haya wanakuwa hawajui, wanabahatisha tu.

Bado watanzania na umbumbu wetu tunaona waziri kuzunguka mikoa anaita wenye matatizo na hati kuleta kero eti anafanya kazi?

Binafsi sisemi hatukuwa na matatizo ya hati, na sisemi hatukuwa na migogoro ya ardhi bali ninachokisema wizara ya ardhi na maendeleo ya makazi ndiye planner namba moja anayeweza kuboresha kila huduma ya kijamii katika miji na vijiji. na huyu asipofanya kazi yake Daima tutahangaika na huduma za kijamii katika miji na vijiji.

Tutabakia kujisia umeme umefikia vijiji vyote may be by 2025 lakini ukweli ubakie umeme utakuwa umefikia makazi machache sana. Kama mwalimu Nyerere alianzisha vijiji vya ujamaa ili awape huduma watu, kwamba huwezi ukawa na watu wametapakaa porini kila mmoja anaishi kivyake, hakuna anayejali bali tunakusanya kodi kuwajengea hawa shule hospitali, barabara n.k.

Kwa binadamu yeyote anayejitambua atasema hatuwezi kufanya kazi hivi, ni lazima tuweke utaratibu wa watu kukaa pamoja ili kupata hizi public services pamoja. Nani aweke huu utaratibu kama sio wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi?

Kuna watu ni mbumbu, anaweza kwenda kukaa katikati ya pori peke yake, watoto ama hawaendi shule, ana wanahangaika kutembea kilomita kadhaa kutafuta elimu. Mtu anakaa porini hamna hospitali, hamna huduma yoyote ya kijamii. Kama Taifa hatuwezi kukubali mbumbu awatese watanzania kwa kuwapeleka kuishi maisha yasiyo na huduma za kijamii na kama Taifa tunaweza kuwaacha watu wanaofanya hivyo, tunawataazama tu, basi taifa zima tunakuwa mbumbumbu.

Ni lazima waziri waziri wa ardhi, nyumba na makazi aweke utaratibu kwamba ni lazima makazi yawe ya mijini, yawe ya vijini yakae pamoja ili kila mtanzania apatae haki yake ya kupata huduma za kijamii kutoka serikalini. Na ikitokea kuna mtu anataka kuishi peke yake porini basi kwanza ni lazima awe na uwezo wa kugharamia huduma za msingi kwa watu anaoenda kuishi nao huko porini.

Upo mfano mwingine, mimi nikiwa mdogo, maeneo ya kwetu tulikuwa na misitu, ina miti na mito. Leo hii misitu yote imefyekwa, watu wanalima, wanajenga, mito yote imekauka. Ukitazama jambo hili kwa juu juu utaona ni kama jambo la watu wa mazingira lakini ukweli shida kubwa liko wizara ya ardhi, nyumba na makazi kutotimiza wajibu wao na kusababisha watu kufanya shughuli za maendeleo popote. Lazima wizara fulani iwaambie watu ni marufuku kujenga, kulima au kufanya shughuli yoyote ya kimaendeleo katika msitu wa asili iwapo kile unachokifanya kinahatarisha msitu huo. Lakini wizara hiyo iende mbali zaidi kuwaambia wananchi wa sehemu hii mtakaa hapa, kwa utaratibu huu na yeyote mwenye dhamana ya kuwaletea huduma yoyote atawakuta hapa. Na kwa utaraibu tuliowawekea huduma yoyote inayofika kila mwananchi hapa ataweza kuipata bila usumbufu.

Lakini Tanzania ya Leo unafyeka msitu wa asili, unalima shamba na kujenga nyumba "it is no body's business". Anayehusika na mazingira utamuona anahangaika kupanda miti michache na sio kulinda mazingira yaliyopo na mwenye kuhusika na kupanga matumizi ya ardhi yeye anasema anahangaika na migogoro tu.


Lakini sisi kwa umbumbumbu wetu tunaitazama wizara hii kama nani
 
MM NIMETABIRI HUYU MAMA HAWEZI KUFIKA MBALI!
 
Sijasoma uzi wako ila huyo wazir ana mihemko mingi rafiki popote. Hajui hata changamoto za idara. Ananikumbusha speech za nchemba wakati anatangaza nia 2015.zilijaa story za Ds first year UDSM
HALAFU HUYU MAMA NI MSHAMBAMSHAMBA HIVI!
 
kama bima ya magari na pikipiki ni kwaajili ya ktimiza takwa la serikali tu na haina msaada wowote sembuuuuse afya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…