Waziri wa Afya na Naibu wake wataweza kuratibu upatikanaji wa chanjo waliyokuwa wanaipinga?

Waziri wa Afya na Naibu wake wataweza kuratibu upatikanaji wa chanjo waliyokuwa wanaipinga?

Hivi hii kamati imerecommend Chanjo ipi kati ya zile 3-4 au na wao wameinia kwenye mtego wa kutaka chanjo yoyote ile, as long as tunapewa bure na COVAX?

Ile report ya professors haina lolote la maana ambalo hatukulijua kabla. Hakukuwa na haja ya kuunda Tume ili watulee report kama ile.
Wamependekeza ile juisi ya Uviko
 
Kiini cha haya yote ni KATIBA yetu - Rais wetu anapewa mamlaka makubwa mno kiasi ukienda na atakavyo yeye basi umekwenda na maji.

Wakati mwingine Waziri inabidi ufanye mambo hata kama unajua ni ya hovyo ili kumridhisha boss wako ili mkono ufike kinywani.

Hawa wasomi wa utabitu kwa sasa wanafanya kazi katika wakati mgumu mno - yaani kufanya u-turn ya nyungu na moja kwa moja kwenda kuratibu chanjo ya covid chini ya usimamizi wa mama aiseee inakuwa kazi ngumu mno.

Ningekuwa mimi nangeomba kupisha wengine.
 
Kama mtu umelazimishwa kufanya kitu ulichokuwa hukiamini ni vigumu sana kukitekeleza kwa ufanisi. Kuratibu ni pamoja na Kuagiza, kusafirisha, kutunza, kusambaza na kuhamasisha jamii waliyoiaminisha chanjo hazifai ili ipate chanjo.

Kuhamasisha jamii kunawa mikono tiririka.

Kuhamasisha watu kuvaa barakoa wakati wao hawazivai au walizipuuza.

Kuondoa imani kwa wananchi ya kujifukiza ili wapate chanjo.

Kurudisha imani kwa wananchi kuwa chanjo hazina madhara tena kwa sababu Tanzania haina chanjo yake chanjo zote ni za mabeberu.

View attachment 1788659
Jinsi walivyo wanafiki wataweza tu.
 
"Only stupid people don't change their minds"..Boutros Boutros-Ghali,Secretary-General of the United Nations from January 1992 to December 1996😷😷😷
 
Back
Top Bottom