Waziri wa Afya, nenda tena Hospitali ya Mwananyamala

Waziri wa Afya, nenda tena Hospitali ya Mwananyamala

chechemtungi

Senior Member
Joined
Dec 4, 2016
Posts
126
Reaction score
113
Naomba nieleze hili ambalo kwenye Moyo wangu siwezi kuliacha kamwe na sintolisahau katika mwaka uliopita linalohusu hospitali ya Mwananyamala.

Mnamo Tarehe 30/12/2020 nilimsaidia majeruhi wa pikipiki ambaye alikuwa amegongwa na gari kumuwahisha hosptali kwa ajili ya Matibabu, aligongewa mitaa ya Sinza , so awali tulifika hosptali ya Palestina then palestina kwaissue ya mgonjwa ilivyo walituambia twende hosptitali ya Mwananyamala.

Hapa ndio msingi wa Jambo ambalo nataka kuwasilisha kwenu wanajamii,

Tulipofika hosptali ya Mwanayamala majila ya saa Nne usiku tuliandikisha kadi pale Reception Then tukaenda ili tuonane na daktari, tulipofika pale tuliambiwa vyumba vinavyotoa huduma ni No 3 na No 5 lakini havikuwa na mtu,

pale pembeni pakusubiria wagonjwa tulimkuta Mama mjamzito mmoja amekaa,

ilibidi tumuulize daktari kaenda wapi, Alitujibu yeye alipofika majira ya saa mbili daktari alikuwa anatoka kwenye chumba No 5 so aliniambia anarudi ,hadi muda huu Saa Nne hajarudi,

duuh kwanza hilo lilitushtua kuona mama Mjamzito kafika Muda wote huo na bado hajapata huduma ilibidi tukae tumsubilishe mgonjwa wetu tukimsubili daktari, Muda ulienda ,waliongezeka watu kadhaa pale nao wakiwa seriously kidogo ilibidi tusubili hapo muda unaenda saa tano.

Watu uzalendo ukawashinda ikabidi kila mmoja aanze kuongea kwa Jazba kidogo,

Mimi nikiangalia kushoto kwangu kuna mtu anaumwa mbavu hapumui vizuri kulia huku kuna mtu vidole vimechanika nikimwangalia mgonjwa wangu huku naye Mguu umevunjika analalamika daaah nikasema kimoyo moyo duuh hii ni hatari sasa,

Huku nikiendelea kuwaza mara ghafla aliingia Jamaa kamuweka mtoto kwenye mikono yake miwili ya mbele wanaandikisha kadi wapo haraka haraka akiwa na mama cjui kama ndio alikuwa mama wa mtoto sikujua kabisa ,

wakafika moja kwa moja kufungua mlango chumba cha kwwnza hamna mtu chumba cha pili nacho hmna mtu kama nusu saa hivi wanahangaika kumtafuta daktari.

tulipomuangalia mtoto yule tukaona analegea kabisa ilibidi tuanze kupiga kelele pale jamani dakatri ,mara tukamuona kuna jamaa anadeki kavaa kama nguo za manesi tukazani muhusika kumbe alikuwa nimfagizi wa pale akawaambia wale waliokuja na mtoto Nendeni emergence napo emergence hamna mtu wakarudi tena ikabidi twende Reception kugomba pale mara wakapiga simu wakaongea sijui na nani mara akaja Nesi pale na daktari ikabidi sisi wote tusubili Wale wenye mtoto waanze, kufungua malango kuingia ndani kwa daktari wakakaa kama dakika Moja mara mama anatoka ndani anaanza kulia, Mtoto alikuwa kashafariki tena mikononi mwao kwa kukosa huduma ya Mapema ,mtoto wa miaka 9 au 8 maskini alipoteza uhai wake mikononi mwao wazazi wake.

Wote tuliumia sana Huzuni ilikuwa imetawala kubwa sana tena sana mahali pale. Haikuishia hapo baada ya kutoka nilikuwa nikisikia kuna Mzee mmoja wa makamo alimfwata yule daktari nikisikia Maongezi yao kwa nje pale.

Mzee alimwambia Yule daktari hivi kuwa Kazi anayofanya siyo kazi yakuweka Maslahi mbele , Udkatari ni kazi ya Wito kutoka kwenye Moyo wako nasi vinginevyo sikuyamwisho ya hukumu atajibia hichi kitendo walichofanya leo mzee aliongea aya flani za kiislamu sikuweza kuzielewa maneno niliyosikia ndio hayo.

Nini nachotaka kuwasilisha kwenu kwanza kwa Watanzania na Kwa waziri wa Afya

Kwa waziri wa Afya jaribu kupitia hizi hosptali zako za serikali zinashida sana tena sana Hasa nyakati za usiku nakuachia wewe hili.

Kwa Watanzania Wenzangu kama unauwezo na umepata emergence issue nyakati za usiku kabisa please napenda kusema usimpeleke mgonjwa wako katika hosptali za serikali Nenda private kama unachochote mfukoni kama hauna haina Jinsi tujibane hivyo hivyo humu

ILA WATOA HUDUMA ZA UMMA TUJITATHIMINI, MH. MAGUFULI HAWA WATU WAMEANZA KUJISAHAU HEBU ILE KAMBA YA CHUMA ULIYOWAFUNGA 2015 HEBU IFUNGE TENA MWAKA 2021 TUMBUA TUMBUA HAWA WATU MH RAIS.
 
Mbona hapo kuna unafuu njoo hapa mawilayani dakitari anapatikana siku mbili tu kwa wiki, ukipata emergency akikisha inangukia siku ya dakitari, ukiwa huna bahati basi unapoteza maisha au unatafuta private kwa gharama kubwa
 
Pale hospiitalini kwenye chumba Na. 8 kuna namba za simu za maoni. Niliwahi kumpigia simu katibu wa Afya na kumlalamikia ubovu wa Hospitali ya Mwananyamala toka mwaka jana, aliniambia kwa simu wanashughulikia hilo suala lakini wapi.

Madaktari wengi wa hizi hospitali wanafanya kazi kiubabaishaji na ni wezi mno na Wizara ya Afya wapo kimya tu wanaacha raia wao wanateseka.
 
Daktari pia ni binadamu je mlifuatilia nini kilichokuwa nyuma ya tukio hadi kumfanya asiwepo hapi ? Tafakari hayo!
 
Ki ukwel mkasa huu umeniuma sana polen sana kuna muda mwingine unaweza kuingiwa na roho mbaya nayy unamaliza pale pale
 
Daktari pia ni binadamu je mlifuatilia nini kilichokuwa nyuma ya tukio hadi kumfanya asiwepo hapi ? Tafakari hayo!
Lakin alikuwa zamu haiwezekani akachlewa bila kutoa maelezo na huyo alikuwa nae wapi
 
ILA WATOA HUDUMA ZA UMMA TUJITATHIMINI,
MH. MAGUFULI HAWA WATU WAMEANZA KUJISAHAU HEBU ILE KAMBA YA CHUMA ULIYOWAFUNGA 2015 HEBU IFUNGE TENA MWAKA 2021 TUMBUA TUMBUA HAWA WATU MH RAIS.

Nimependa hii aya yako,Ila tambua kuwa watoa huduma hawa wamedharauliwa, wamenyanyaswa, wamefedheheshwa sana sana na mtu huyo kwa kutowapa HAKI na STAHIKI zao za MSINGI kabisa za kisheria.

1. Annual increment
2. Madaraja na vyeo
3. Malimbikizo

Zinafanyika siasa katika HAKI zao.

Walimu, madaktari, wauguzi, maaskari n.k wamefanya Kazi miaka 5 na 6 sasa inaelekea bila bila.


"Show me your brutality I will show you blood suckers"

Nireteeni gwajima!

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Wakuilaumu zaidi serikali wakiboresha miundo mbinu na maslahi haya mambo yatapungua watu hawaajiriwi sehemu muhimu kama hizi wanaojiriwa hawana sifa kwa kuwa wanafahamiana mtu anahangaika na ndege watu wanakufa huku kwa kuwa kuna upungufu wa watoa huduma.

Mtoto kafariki watu wengi wanahusika kwenye hiyo chain hadi mwajiri mwenyewe ambae ni serikali
 
Mwananyamala hospital daah nikae tu kimya ningesema mengi sema sina id fake maana watu wangetumbuliwa leo hii hii sema watatumbuliwa sawa je siku nikiwa sijielewi mahututi nikapelekwa hapo nini kitajiri R.I.P brother
 
Mbona hapo kuna unafuu njoo hapa mawilayani dakitari anapatikana siku mbili tu kwa wiki, ukipata emergency akikisha inagukia siku ya dakitari, ukiwa huna bahati basi unapoteza maisha au unatafuta private kwa gharama kubwa
Nchi yetu elimu ni tatizo kubwa. Sasa wewe unataka kuhalalisha huo uzembe kwa kuwa huko wilayani kwenu ni wazembe zaidi? Anyways mleta mada tatizo ni sisi wenyewe watanzania.

Tunapenda kulalamika kwa maneno bila kuchukuwa hatua. Kwa mfano ingekuwa nchi nyingine huo uzembe uliokutana nao kesho yake ungeondoka na watu. Ilitakiwa mchukuwe hatua hata kukubaliana kesho yake muende kwenye ofisi za eg mkuu wa wilaya mkiwa na vyombo vya habari.
 
ILA WATOA HUDUMA ZA UMMA TUJITATHIMINI,
MH. MAGUFULI HAWA WATU WAMEANZA KUJISAHAU HEBU ILE KAMBA YA CHUMA ULIYOWAFUNGA 2015 HEBU IFUNGE TENA MWAKA 2021 TUMBUA TUMBUA HAWA WATU MH RAIS...
Anaajiri na kuboresha mazingira?
 
Nchi yetu elimu ni tatizo kubwa. Sasa wewe unataka kuhalalisha huo uzembe kwa kuwa huko wilayani kwenu ni wazembe zaidi? Anyways mleta mada tatizo ni sisi wenyewe watanzania. Tunapenda kulalamika kwa maneno bila kuchukuwa hatua. Kwa mfano ingekuwa nchi nyingine huo uzembe uliokutana nao kesho yake ungeondoka na watu. Ilitakiwa mchukuwe hatua hata kukubaliana kesho yake muende kwenye ofisi za eg mkuu wa wilaya mkiwa na vyombo vya habari.
Nafikir umeshindwa kumuelewa watoa huduma ni wachache sio kwamba anahalalisha serikali iajiri fikiria hapo kuna dokta moja tu na watu walikuw wa 5 kweli asife hata mmoja?
 
Naomba nieleze hili ambalo kwenye Moyo wangu siwezi kuliacha kamwe na sintolisahau katika mwaka uliopita linalohusu hospitali ya Mwananyamala.

Mnamo Tarehe 30/12/2020 nilimsaidia majeruhi wa pikipiki ambaye alikuwa amegongwa na gari kumuwahisha hosptali kwa ajili ya Matibabu, aligongewa mitaa ya Sinza , so awali tulifika hosptali ya Palestina then palestina kwaissue ya mgonjwa ilivyo walituambia twende hosptitali ya Mwananyamala....
Aisee
 
Mwananyamala hospital daah nikae tu kimya ningesema mengi sema sina id fake maana watubwangetumbuliwa leo hii hii sema watatumbuliwa sawa je siku nikiwa sijielewi mahututi nikapelekwa hapo nini kitajiri R.I.P brother
Mimi mwenyewe nisimalizie tu maana vilivyoendelea hapo nimeweka Moyoni tu ila nimejifunza kwa mapana sana
 
Wakuilaumu zaidi serikali wakiboresha miundo mbinu na maslahi haya mambo yatapungua watu hawaajiriwi sehemu muhimu kama hizi wanaojiriwa hawana sifa kwa kuwa wanafahamiana mtu anahangaika na ndege watu wanakufa huku kwa kuwa kuna upungufu wa watoa huduma.

Mtoto kafariki watu wengi wanahusika kwenye hiyo chain hadi mwajiri mwenyewe ambae ni serikali
Tunaweza kuwalaumu serikali lakini tutambue kuwa hizi kazi za kuwahudumia watu zinaongozwa na wito na si maslahi tunatakiwa tujifunze baadhi ya vitu kama binadamu.
 
Tunaweza kuwalaumu serikali lakini tutambue kuwa hizi kazi za kuwahudumia watu zinaongozwa na wito na si maslahi tunatakiwa tujifunze baadhi ya vitu kama binadamu.
Daktari yupo mmoja walikuwa kama 6 hapo wanataka huduma tena za dharula na hatujui kafanya kazi muda gan au hakupata mapumziko kabisa hilo limekaaje? Tuangalie pande zote mbili ieleweke sitetei uovu
 
Naomba nieleze hili ambalo kwenye Moyo wangu siwezi kuliacha kamwe na sintolisahau katika mwaka uliopita linalohusu hospitali ya Mwananyamala.

Mnamo Tarehe 30/12/2020 nilimsaidia majeruhi wa pikipiki ambaye alikuwa amegongwa na gari kumuwahisha hosptali kwa ajili ya Matibabu, aligongewa mitaa ya Sinza , so awali tulifika hosptali ya Palestina then palestina kwaissue ya mgonjwa ilivyo walituambia twende hosptitali ya Mwananyamala....
Nimemtumia hii mheshimiwa waziri Dorothy
 
Naomba nieleze hili ambalo kwenye Moyo wangu siwezi kuliacha kamwe na sintolisahau katika mwaka uliopita linalohusu hospitali ya Mwananyamala.

Mnamo Tarehe 30/12/2020 nilimsaidia majeruhi wa pikipiki ambaye alikuwa amegongwa na gari kumuwahisha hosptali kwa ajili ya Matibabu, aligongewa mitaa ya Sinza , so awali tulifika hosptali ya Palestina then palestina kwaissue ya mgonjwa ilivyo walituambia twende hosptitali ya Mwananyamala...
Pole sana mkuu na mgonjwa wako na hao wengine; hasa huyo mtoto aliyepoteza uhai.

Haya ni mambo ya kusikitisha sana. Hukueleza, kama baadae mgonjwa wako na hao wengine mlihudumiwa vizuri, au mliendelea kusotea hapo hapo kwa kusubiri?

Huo ulioueleza ni zaidi ya uzembe wa mtu mmoja, daktari; huo ni uozo wa mfumo mzima. Huyo mzazi (wazazi) waliopoteza mtoto wao, hata kama haiwasaidii chochote baada ya kumpoteza mpendwa wao, lakini wana wajibu wa kutoliacha hili jambo lipite hivi hivi. Kuna taratibu, hata huko kwa taaluma ya madaktari unaosimamia haki na kuwaadhibu baadhi yao wanaokiuka maadili ya kazi zao.

Hawa wazazi wanastahili kupewa msaada wa kusimamia hatua za kuhakikisha hawa madaktari waliofanya uzembe hawaachwi hivi hivi na kuendeleza uzembe wao. Jambo hili linastahili kufikishwa kwenye taratibu za kuwaashughulikia hawa watumishi wasiokuwa na roho za kiutu.
 
Back
Top Bottom