Waziri wa Afya, nenda tena Hospitali ya Mwananyamala

Waziri wa Afya, nenda tena Hospitali ya Mwananyamala

Serikali iboreshe huduma za afya,maslahi ya watumishi yaongezwe,haiwezekani wanasiasa ,wabunge na wengineo wajilipe mishahara mikubwa huku kada nyingine zikiwa hoi.
Hawa madaktari hata morals ya kazi hawana.

Vifaa hakuna,madawa hakuna, gloves hakuna kila kitu hakuna.,
Dr.Gwajima ataenda hapo atapiga kelele tutamsifia lakini hakuna kitakachobadilika.,tulitaka mambo yaende sawa serikali iwe ya kwanza kubadilika.
 
Huu ni udhaifu, hata kama angekuwa mmoja, hiyo ni hospitali ya rufaa haiwrzekani wafanye uzembe kama huo. Uzembe unaweza kuwa wa daktari au uongozi kwa kushindwa kuweka madaktari wa kuweza kusimamia changamoto za wagonjwa kama zinavyojitokeza.

Ukimsikiliza waziri wao anaongea utagundua kinachofanyika hospital za serikali hakifikii hata 30% ya kile wanapaswa kufanya
Nadhani madaktari wanaopaswa kulaumiwa hapo ni wa kitengo cha emergency ambapo kwa nyakati za usiku wao ndio huwaona wagonjwa na kuwastabilize kabla ya kuwapeleka katika wodi husika.So emergency team ya hapo Mwananyamala means haikuwepo? Kuanzia wauguzi na madaktari? Kama ni hivyo basi hapo kuna shida.Wajaribu kuiga au kutengeneza emergency department kama za muhimbili upanga au Mloganzila...i have been there..wanafanya kazi nzuri
 
Nafikir umeshindwa kumuelewa watoa huduma ni wachache sio kwamba anahalalisha serikali iajiri fikiria hapo kuna dokta moja tu na watu walikuw wa 5 kweli asife hata mmoja?
Mkuu hapana. Hospital zetu nazijua sana. Pamoja na kuwa serikali haiwalipi vizuri na mazingira yao ni magumu sana lakini nao wana sehemu yao ya uzembe
 
Serikali iboreshe huduma za afya,maslahi ya watumishi yaongezwe,haiwezekani wanasiasa ,wabunge na wengineo wajilipe mishahara mikubwa huku kada nyingine zikiwa hoi...
Hizi kelele alipiga sana jamaa mmoja anaitwa Dr Ulimboka enzi za Kikwete. Matokeo yake akatekwa na kupigwa karibu kuuawa. Wananchi badala tuungane kum-suport tukabaki kushangaa.

Baadhi ya madaktari wenzake wakatoa tamko kuiunga mkono serikali. Matatizo mengine tunajitakia wenyewe na kila mtu atakumbana na madhila haya ya kuogopa kwa wakati wake. Hatujui kesho ni nani. Anaweza kuwa mimi au yule au wewe.
 
Umemaliza yote Mkuu.... Inasikitisha Sana kuona Watanzania wenzetu wakishupaza misuli ya shingo kuwalaumu Watumishi wa imma wa nchi hii huku wakishindwa kabisa kuwasapoti kudai hayo maslahi yao..... Mwaka wa sita Sasa bila maboresho ya maslahi yao,na Kuna maeneo mengine huko kwe hospitali za halmashauri madaktari wanaofanya ON CALL DUTIES hawalipwi allowances zao kwa madai kuwa pesa hakuna,huku wakilazimishwa kuendelea kufanya kazi.

Hawa watumishi wa umma ,ni binadamu wenzetu ambao wanahitaji maslahi bora ili waweze kuendesha maisha yao ya kila siku. Bila kujali maslahi yao, hawawezi kuwa na utulivu unaotakiwa kutimiza majukumu yao.

Niwashauri tu ,Watanzania wenzangu tuache kuwalaumu Watumishi wetu wa umma, badala yake tupaze sauti kuitaka serikali ya Rais Magufuli kuheshimu na kujali maslahi yao ili wawe na utulivu,furaha ya kufanya majukumu yao, watuhudumie vema.
ILA WATOA HUDUMA ZA UMMA TUJITATHIMINI,
MH. MAGUFULI HAWA WATU WAMEANZA KUJISAHAU HEBU ILE KAMBA YA CHUMA ULIYOWAFUNGA 2015 HEBU IFUNGE TENA MWAKA 2021 TUMBUA TUMBUA HAWA WATU MH RAIS...
 
Mkuu hapana. Hospital zetu nazijua sana. Pamoja na kuwa serikali haiwalipi vizuri na mazingira yao ni magumu sana lakini nao wana sehemu yao ya uzembe

Ishinikizeni Serikali iboreshe maslahi ya watumishi hao, iboreshe pia upatikanaji wa vitendea kazi alafu ndio uwalaumu.

Hao unaowalaumu kwa uzembe hapo ( kwe hospitali za umma) ndio hao hao wanatumiwa na hospitali binafsi ambazo unasifia huduma zao.
 
Sasa kwanini tuamue kufanya hivi kwa watu ambao ni hawakupaswa kufanyiwa vitendo kama hivi,
Kama unaona maslahi hamna tujaribu kuwaachia wenye wito wakufanya kazi hizi wafanye
Watu wasio na hatia wanaumia nachosisitiza
Usiombee hili likukute
 
ILA WATOA HUDUMA ZA UMMA TUJITATHIMINI,
MH. MAGUFULI HAWA WATU WAMEANZA KUJISAHAU HEBU ILE KAMBA YA CHUMA ULIYOWAFUNGA 2015 HEBU IFUNGE TENA MWAKA 2021 TUMBUA TUMBUA HAWA WATU MH RAIS.

Nimependa hii aya yako,Ila tambua kuwa watoa huduma hawa wamedharauliwa,wamenyanyaswa,wamefedheheshwa sana sana na mtu huyo kwa kutowapa HAKI na STAHIKI zao za MSINGI kabisa za kisheria.

1 Annual increment
2Madaraja na vyeo
3Malimbikizo

Zinafanyika siasa katika HAKI zao.

Walimu,madaktari,wauguzi,maaskari n.k wamefanya Kazi miaka 5 na 6 sasa inaelekea bila bila.

"Show me your brutality I will show you blood suckers"

Nireteeni gwajima!
Au nasema uongo ndugu zangu?
Ukiona kazi haikulipi achana nayo usilazimishe,

Sekta ya afya ni sehemu nyeti sana, kama unahisi una tatizo na muajiri wako ni vema aidha kuomba likizo au kuacha lakini sio kunyanyasa wagonjwa.
 
Umemaliza yote Mkuu.... Inasikitisha Sana kuona Watanzania wenzetu wakishupaza misuli ya shingo kuwalaumu Watumishi wa imma wa nchi hii huku wakishindwa kabisa kuwasapoti kudai hayo maslahi yao..... Mwaka wa sita Sasa bila maboresho ya maslahi yao,na Kuna maeneo mengine huko kwe hospitali za halmashauri madaktari wanaofanya ON CALL DUTIES hawalipwi allowances zao kwa madai kuwa pesa hakuna,huku wakilazimishwa kuendelea kufanya kazi.

Hawa watumishi wa umma ,ni binadamu wenzetu ambao wanahitaji maslahi bora ili waweze kuendesha maisha yao ya kila siku. Bila kujali maslahi yao, hawawezi kuwa na utulivu unaotakiwa kutimiza majukumu yao.

Niwashauri tu ,Watanzania wenzangu tuache kuwalaumu Watumishi wetu wa umma, badala yake tupaze sauti kuitaka serikali ya Rais Magufuli kuheshimu na kujali maslahi yao ili wawe na utulivu,furaha ya kufanya majukumu yao, watuhudumie vema.
Kuna kazi za wito inabidi watu waambiwe na si kuweka maslahi mbele mkuu hizi huduma wanapata wengi maskini na matajili waliokuwa nacho na wasiokuwa nacho.
 
Kasheshe iko palestina kwenye kujiungua,mambo yanayofanyika pale rushwa zinazoombwa na manesi shida tupu,serikali fanya mitego kwa manesi jaman sis wanyonge tunaumia,ili sijaadithiwa nimejionea mwenyew rushwa inagawiwa kwenye kibaraza Cha kupanda kwenda grofa ya kwanza wodin,na kuna giza pale taa hamna hatar tupu
 
Sasa kwanini tuamue kufanya hivi kwa watu ambao ni hawakupaswa kufanyiwa vitendo kama hivi,
Kama unaona maslahi hamna tujaribu kuwaachia wenye wito wakufanya kazi hizi wafanye
Watu wasio na hatia wanaumia nachosisitiza
Usiombee hili likukute

Ndugu, hii kauli ya eti "ni wito" isiwe kisingizio Cha kuminya maslahi ya hao watu, tambua na wao Wana familia za kuzihudumia.... Wito bila utulivu wa fikra haiwezekani.

Cha msingi ni kwa sisi Wananchi tunaoumizwa na hayo badala ya kuwalaumu watoa huduma hao, tuishinikize serikali iboreshe maslahi yao plus mazingira wanayofanyia kazi ili wasiathiriwe na msongo wa mawazo unaotokana na ugumu wa maisha ili watuhudumie vizuri.
 
Kuna kazi za wito inabidi watu waambiwe na si kuweka maslahi mbele mkuu hizi huduma wanapata wengi maskini na matajili waliokuwa nacho na wasiokuwa nacho.

Hakuna kazi ya wito siku hizi ndugu,hata hao watu wa dini wamegeuka wajasiriamali siku hizi....FUTA KABISA HIYO "MENTALITY"
 
Naomba nieleze hili ambalo kwenye Moyo wangu siwezi kuliacha kamwe na sintolisahau katika mwaka uliopita linalohusu hospitali ya Mwananyamala.

Mnamo Tarehe 30/12/2020 nilimsaidia majeruhi wa pikipiki ambaye alikuwa amegongwa na gari kumuwahisha hosptali kwa ajili ya Matibabu, aligongewa mitaa ya Sinza , so awali tulifika hosptali ya Palestina then palestina kwaissue ya mgonjwa ilivyo walituambia twende hosptitali ya Mwananyamala.

Hapa ndio msingi wa Jambo ambalo nataka kuwasilisha kwenu wanajamii,

Tulipofika hosptali ya Mwanayamala majila ya saa Nne usiku tuliandikisha kadi pale Reception Then tukaenda ili tuonane na daktari, tulipofika pale tuliambiwa vyumba vinavyotoa huduma ni No 3 na No 5 lakini havikuwa na mtu,

pale pembeni pakusubilia wagonjwa tulimkuta Mama mjamzito mmoja amekaa,

ilibidi tumuulize daktari kaenda wapi,
Alitujibu yeye alipofika majira ya saa mbili daktari alikuwa anatoka kwenye chumba No 5 so aliniambia anarudi ,hadi muda huu Saa Nne hajarudi,

duuh kwanza hilo lilitushtua kuona mama Mjamzito kafika Muda wote huo na bado hajapata huduma ilibidi tukae tumsubilishe mgonjwa wetu tukimsubili daktari,
Muda ulienda ,waliongezeka watu kadhaa pale nao wakiwa seriously kidogo ilibidi tusubili hapo muda unaenda saa tano ,

Watu uzalendo ukawashinda ikabidi kila mmoja aanze kuongea kwa Jazba kidogo,

Mimi nikiangalia kushoto kwangu kuna mtu anaumwa mbavu hapumui vizuri kulia huku kuna mtu vidole vimechanika nikimwangalia mgonjwa wangu huku naye Mguu umevunjika analalamika daaah nikasema kimoyo moyo duuh hii ni hatari sasa,

Huku nikiendelea kuwaza mara ghafla aliingia Jamaa kamuweka mtoto kwenye mikono yake miwili ya mbele wanaandikisha kadi wapo haraka haraka akiwa na mama cjui kama ndio alikuwa mama wa mtoto sikujua kabisa ,

wakafika moja kwa moja kufungua mlango chumba cha kwwnza hamna mtu chumba cha pili nacho hmna mtu kama nusu saa hivi wanahangaika kumtafuta daktari ,
tulipomuangalia mtoto yule tukaona analegea kabisa ilibidi tuanze kupiga kelele pale jamani dakatri ,mara tukamuona kuna jamaa anadeki kavaa kama nguo za manesi tukazani muhusika kumbe alikuwa nimfagizi wa pale akawaambia wale waliokuja na mtoto Nendeni emergence napo emergence hamna mtu wakarudi tena ikabidi twende Reception kugomba pale mara wakapiga simu wakaongea sijui na nani mara akaja Nesi pale na daktari ikabidi sisi wote tusubili
Wale wenye mtoto waanze,
kufungua malango kuingia ndani kwa daktari wakakaa kama dakika Moja mara mama anatoka ndani anaanza kulia,
Mtoto alikuwa kashafariki tena mikononi mwao kwa kukosa huduma ya Mapema ,mtoto wa miaka 9 au 8 maskini alipoteza uhai wake mikononi mwao wazazi wake ,

Wote tuliumia sana Huzuni ilikuwa imetawala kubwa sana tena sana mahali pale .
Haikuishia hapo baada ya kutoka nilikuwa nikisikia kuna Mzee mmoja wa makamo alimfwata yule daktari nikisikia Maongezi yao kwa nje pale ,

Mzee alimwambia Yule daktari hivi kuwa
Kazi anayofanya siyo kazi yakuweka Maslahi mbele , Udkatari ni kazi ya Wito kutoka kwenye Moyo wako nasi vinginevyo sikuyamwisho ya hukumu atajibia hichi kitendo walichofanya leo mzee aliongea aya flani za kiislamu sikuweza kuzielewa maneno niliyosikia ndio hayo .

Nini nachotaka kuwasilisha kwenu kwanza kwa Watanzania na Kwa waziri wa Afya

Kwa waziri wa Afya jaribu kupitia hizi hosptali zako za serikali zinashida sana tena sana Hasa nyakati za usiku nakuachia wewe hili.

Kwa Watanzania Wenzangu kama unauwezo na umepata emergence issue nyakati za usiku kabisa please napenda kusema usimpeleke mgonjwa wako katika hosptali za serikali Nenda private kama unachochote mfukoni kama hauna haina Jinsi tujibane hivyo hivyo humu

ILA WATOA HUDUMA ZA UMMA TUJITATHIMINI,
MH. MAGUFULI HAWA WATU WAMEANZA KUJISAHAU HEBU ILE KAMBA YA CHUMA ULIYOWAFUNGA 2015 HEBU IFUNGE TENA MWAKA 2021 TUMBUA TUMBUA HAWA WATU MH RAIS.
Kwahiyo unaona akirudi ndo atamaliza tatizo. Tupunguze mihemko. Mbona hatujiulizi kwanini wahumu wa Afya wamefikia hapo?

Mnajua nao Wana familia, wanashida zao, wanamatarajio yao?

Sasa basi ili watibu vema basi umma uwape hayo
 
Ndugu, hii kauli ya eti "ni wito" isiwe kisingizio Cha kuminya maslahi ya hao watu, tambua na wao Wana familia za kuzihudumia.... Wito bila utulivu wa fikra haiwezekani.

Cha msingi ni kwa sisi Wananchi tunaoumizwa na hayo badala ya kuwalaumu watoa huduma hao, tuishinikize serikali iboreshe maslahi yao plus mazingira wanayofanyia kazi ili wasiathiriwe na msongo wa mawazo unaotokana na ugumu wa maisha ili watuhudumie vizuri.
Nimevutiwa na hoja yako
 
Pole sana kwa kuyashuhudia hayo maswaibu, Pole zaidi zimuendee Mama aliyempoteza Mwanae.

Kwanza nyie mlitakiwa kutoa taarifa kwa uongozi wakati huohuo au pia mngepiga simu/kutuma msg kwa Waziri alishatoa namba zake za simu.

Maelezo yako yameeleweka lakini in case tungepata maelezo ya upande wa pili huenda tungemlalamikia mtu/mhimili mwingine kuliko mtoa huduma. Huenda huko alikokuwa alikuwa akitoa huduma kwa mgonjwa mwingine mwenye dharura.

Wafanyakazi sekta ya afya katika hospitali zetu ni wachache na wamebebeshwa mzigo mzito, Serikali hailioni hilo hata kufikiria kuwapa motisha imeshindwa badala yake imeongeza makato kwenye marejesho ya mkopo wa loan board na kuminya stahiki zao, katika hali hii usitegemee kuona wito.

Je, Umewahi kuona utendaji wa hospitali Kama MOI ulivyo? At least hapo MOI ukienda muda wote utapata huduma ila Siri iliyopo pale ni utaratibu motisha kwa Wafanyakazi wao.

Bado tunayo safari ndefu kubadili mfumo wetu wa kutenda kazi ktk taaaisisi za serikali na mojawapo ya mambo ya kuzingatia ni uboreshaji wa mazingira ya kazi, vitendea kazi na maslahi ya Wafanyakazi, Serikali ikikwepa hilo jukumu tusitegemee mabadiliko makubwa hata kama watumishi watatumbuliwa kila kukicha.

Happy New Year.. 2021
 
Hahaha kwa wale wageni nchi hii na msiojua tunafanya nini.

TUNAJENGA MAJENGO MENGI, HIZO HUDUMA MTAJIJUA WENYEWE.

Tuliwaambia tunajenga miundo mbinu, maendeleo ya vitu siyo watu.
 
Mbona hapo kuna unafuu njoo hapa mawilayani dakitari anapatikana siku mbili tu kwa wiki, ukipata emergency akikisha inangukia siku ya dakitari, ukiwa huna bahati basi unapoteza maisha au unatafuta private kwa gharama kubwa
Da,Hawa wahudumu wa afya ni wajinga,kwani kama wanadai ongezeko la mshahara wangetumia taratibu sahihi.Ni dhambi kusababisha mtu apoteze maisha,hiyo laana hawataikwepa.Wajirekebishe.
 
Umemaliza yote Mkuu.... Inasikitisha Sana kuona Watanzania wenzetu wakishupaza misuli ya shingo kuwalaumu Watumishi wa imma wa nchi hii huku wakishindwa kabisa kuwasapoti kudai hayo maslahi yao..... Mwaka wa sita Sasa bila maboresho ya maslahi yao,na Kuna maeneo mengine huko kwe hospitali za halmashauri madaktari wanaofanya ON CALL DUTIES hawalipwi allowances zao kwa madai kuwa pesa hakuna,huku wakilazimishwa kuendelea kufanya kazi.

Hawa watumishi wa umma ,ni binadamu wenzetu ambao wanahitaji maslahi bora ili waweze kuendesha maisha yao ya kila siku. Bila kujali maslahi yao, hawawezi kuwa na utulivu unaotakiwa kutimiza majukumu yao.

Niwashauri tu ,Watanzania wenzangu tuache kuwalaumu Watumishi wetu wa umma, badala yake tupaze sauti kuitaka serikali ya Rais Magufuli kuheshimu na kujali maslahi yao ili wawe na utulivu,furaha ya kufanya majukumu yao, watuhudumie
Hizi changamoto watu hawaelewi kabisa...tangu nianze kazi hosp flan ya serikali natimiza mwaka sasa sijawah pata on call allowance hata moja...na mshahara ulikuw wa november..na hii ndio january...ila tunaendelea kufanya kazi kwa kuw ni wajibu wetu despite na mazingira husika
 
Hispitali nyingi za serikali huduma zao za usiku ni tatizo
 
Back
Top Bottom