Waziri wa Afya, nenda tena Hospitali ya Mwananyamala

Waziri wa Afya, nenda tena Hospitali ya Mwananyamala

Daktari yupo mmoja walikuwa kama 6 hapo wanataka huduma tena za dharula na hatujui kafanya kazi muda gan au hakupata mapumziko kabisa hilo limekaaje? Tuangalie pande zote mbili ieleweke sitetei uovu
Huu ni udhaifu, hata kama angekuwa mmoja, hiyo ni hospitali ya rufaa haiwrzekani wafanye uzembe kama huo. Uzembe unaweza kuwa wa daktari au uongozi kwa kushindwa kuweka madaktari wa kuweza kusimamia changamoto za wagonjwa kama zinavyojitokeza.

Ukimsikiliza waziri wao anaongea utagundua kinachofanyika hospital za serikali hakifikii hata 30% ya kile wanapaswa kufanya
 
Daktari yupo mmoja walikuwa kama 6 hapo wanataka huduma tena za dharula na hatujui kafanya kazi muda gan au hakupata mapumziko kabisa hilo limekaaje? Tuangalie pande zote mbili ieleweke sitetei uovu
Ina maana hujui taratibu za kazi hizo; au unatafuta kisingizio tu cha uzembe wa hali ya hatari kabisa. Watu wanapoteza maisha bado unatafuta visababu vya uongo na kweli?
 
Ina maana hujui taratibu za kazi hizo; au unatafuta kisingizio tu cha uzembe wa hali ya hatari kabisa. Watu wanapoteza maisha bado unatafuta visababu vya uongo na kweli?
Kwamba watu wote 6 alitakiwa awalaze kitanda kimoja? Hii nchi ina msomi huyo mmoja?
 
Naomba nieleze hili ambalo kwenye Moyo wangu siwezi kuliacha kamwe na sintolisahau katika mwaka uliopita linalohusu hospitali ya Mwananyamala.

Mnamo Tarehe 30/12/2020 nilimsaidia majeruhi wa pikipiki ambaye alikuwa amegongwa na gari kumuwahisha hosptali kwa ajili ya Matibabu, aligongewa mitaa ya Sinza , so awali tulifika hosptali ya Palestina then palestina kwaissue ya mgonjwa ilivyo walituambia twende hosptitali ya Mwananyamala...
Ndiyo maana nasema waziri asikurupuke, afanye ki utafiti kwa mfumo mzima ili atatue changamoto, inauma sana tena sana
 
Huu ni udhaifu, hata kama angekuwa mmoja, hiyo ni hospitali ya rufaa haiwrzekani wafanye uzembe kama huo. Uzembe unaweza kuwa wa daktari au uongozi kwa kushindwa kuweka madaktari wa kuweza kusimamia changamoto za wagonjwa kama zinavyojitokeza.

Ukimsikiliza waziri wao anaongea utagundua kinachofanyika hospital za serikali hakifikii hata 30% ya kile wanapaswa kufanya
Ndio uzembe wa pande zote mbili hapo uongozi n serikali watu wanapoteza maisha kwa sababu pengine baadhi ya mambo yanachukuliwa simple nafikir afya na elimu ni sehem nyeti kuwekeza
 
Lakin alikuwa zamu haiwezekani akachlewa bila kutoa maelezo na huyo alikuwa nae wapi
Mantiki yangu kubwa ni Kiapo cha Utabibu cha Hippocrates kinasema "Do no harm" daktari yupo hapo kabla hajawa daktari tukumbuke pia ni binadamu so mlishawahi kujua matatizo wanayoyapata madaktari hasa nyakati za usiku au ni namna gani daktari wa kitanzania anakuwa motivated kulingana na uzito wa kazi wazifanyazo ! Ukiyajua hayo basi hutopata shida karibuni nchi za watu mjifunze namna mambo yanavyoendeshwa kwa uweledi.
 
Kwamba daktari ni mmoja tu asipokuwepo basi mambo hayaendi? Sasa kama hospital kubwa kama hiyo kuna mambo hayo, can you imagine hospital nyingine za serikali zikoje? USIOMBE
Mantiki yangu kubwa ni Kiapo cha Utabibu cha Hippocrates kinasema "Do no harm" daktari yupo hapo kabla hajawa daktari tukumbuke pia ni binadamu so mlishawahi kujua matatizo wanayoyapata madaktari hasa nyakati za usiku au ni namna gani daktari wa kitanzania anakuwa motivated kulingana na uzito wa kazi wazifanyazo ! Ukiyajua hayo basi hutopata shida karibuni nchi za watu mjifunze namna mambo yanavyoendeshwa kwa uweledi...
 
Ndio uzembe wa pande zote mbili hapo uongozi n serikali watu wanapoteza maisha kwa sababu pengine baadhi ya mambo yanachukuliwa simple nafikir afya na elimu ni sehem nyeti kuwekeza
Mkuu kwa hili suala mpaka hapa uzembe wa srikali haujadhihirika. Ila uzembe wa daktari. Kuna vyumba viwili vya madaktari na pia kuna emergence wote hawakuwepo. Unaweza kuta wanapigana miti tu na manesi au stori.

Uongozi wa hospitali hizi una jambo la kufanya kwani uzembe huu unawagusa wao pia.
 
Inauma sana. Mimi siwezi laumu moja kwa moja kwani huwezi kujua huyo daktari alikuwa wapi wakati. Huenda labda alikuwa wodini kuhudumia wagonjwa wengine...
Afya ni taifa na taifa ni afya....kama taifa lisingekuwa na afya hata hiyo MITANO HUWEZI KUIONA au hiyo miradi haiwezi kutekelezeka.

Inabidi selikari iwekeze sana kwenye afya
Madaktari na manesi wapo wengi tu mtaani lakini hawaajairiwi.

Doctor: patient ratio bado hatujaifikia
Nesi: patient ratio bado hatujaifikiwa.

Mfano nesi anatakiwa ahudumie watu 4 hadi 6 kama sikosei lakini unaweza kuta shift yake anahudumia wodi nzima!! Does it make sense
 
Mkuu kwa hili suala mpaka hapa uzembe wa srikali haujadhihirika. Ila uzembe wa daktari. Kuna vyumba viwili vya madaktari na pia kuna emergence wote hawakuwepo. Unaweza kuta wanapigana miti tu na manesi au stori.

Uongozi wa hospitali hizi una jambo la kufanya kwani uzembe huu unawagusa wao pia.
Hapa nimekupata vizur mkuu inaweza kuwa point
 
Ni Kweli pale mwananyamala bado kuna matatizo ingawa kuna madaktari wapya wameajiriwa.

Malalamiko bado ni mengi , kuna haja ya kuiangalia hii hospitali kwa ukaribu zaidi.
 
Ndiyo maana nasema waziri asikurupuke, afanye ki utafiti kwa mfumo mzima ili atatue changamoto, inauma sana tena sana
Viongozi wengi wanakurupuka tu kutoa maamuzi yaani hawatafuti root cause ya jambo...mara nyingi wanafanya ile inaitwa MSHIKWA NA MFUPA ndo anayewajibishwa. Je, mla nyama??
 
Mkuu hayo.mambo ni hospital karibu zote za serikali pale Buguruni hospital ya PLAN ukienda usiku huwezi mkuta daktari na hata ukimkuta atakupa panadol kisha atakuambia njoo kesho.
 
Kwamba watu wote 6 alitakiwa awalaze kitanda kimoja? Hii nchi ina msomi huyo mmoja?
Hapana.
Kwamba alipotakiwa kuwahudumia watu hao kwa nyakati mbalimbali usiku huo, hakuwepo kutoa huduma hiyo kwa wakati mwafaka.

Huyo anatakiwa ajibu uhalifu huo aliofanya kwa usiku huo.
 
We jamaa kwa hili usiwatetee mimi nipo hii sekta tunawajua hao madaktari walivyo washenzi hasa wa hospital za serikali na wanafanyaga makusudi hasa shift za usiku .
Daktari pia ni binadamu je mlifuatilia nini kilichokuwa nyuma ya tukio hadi kumfanya asiwepo hapi ? Tafakari hayo!
 
Buzuruga mwanza Ni zaidi ya kuzimu kwa wagonjwa wa emergency..nilimpeleka mwanangu amegongwa na pikipiki..kichwa kinabonyea Yuko vibaya..nikakuta jamaa mmoja naambiwa Ni daktari..alinaimbia kwa Sasa (saa 12 jioni) niko mwenyewe kwahiyo mlaze mtoto hapo (chini kwenye zege flani) hadi nitakapo maliza kutibu wagonjwa wengine..nilikaa Kama dkk 30..watu wangine wakaniambia kimbia bugando hapa mtoto wako atakufa.

Nimbeba mtoto fasta nikampeleka bugando.. Bugando kwa emergency Ni hospital Bora Sana Sana..nilipokelewa na kundi kubwa la madaktari na wahudumu wengine..mtoto akafanyiwa vipimo fasta Kama CT SCAN na huduma nyingine..
Nawashukuru Sana madaktari na wasaidizi wao kwa Kazi njema..
 
Hapana.
Kwamba alipotakiwa kuwahudumia watu hao kwa nyakati mbalimbali usiku huo, hakuwepo kutoa huduma hiyo kwa wakati mwafaka.

Huyo anatakiwa ajibu uhalifu huo aliofanya kwa usiku huo.
haya mkuu nimekupata
 
Nchi yetu elimu ni tatizo kubwa. Sasa wewe unataka kuhalalisha huo uzembe kwa kuwa huko wilayani kwenu ni wazembe zaidi? Anyways mleta mada tatizo ni sisi wenyewe watanzania. Tunapenda kulalamika kwa maneno bila kuchukuwa hatua. Kwa mfano ingekuwa nchi nyingine huo uzembe uliokutana nao kesho yake ungeondoka na watu. Ilitakiwa mchukuwe hatua hata kukubaliana kesho yake muende kwenye ofisi za eg mkuu wa wilaya mkiwa na vyombo vya habari.
Eeenh, mkuu 'macho', watageuziwa kibao na kuambiwa "wameandamana", na unajua nchi hii tusivyopenda maandamano ya aina yoyote!
 
Naomba nieleze hili ambalo kwenye Moyo wangu siwezi kuliacha kamwe na sintolisahau katika mwaka uliopita linalohusu hospitali ya Mwananyamala.

Mnamo Tarehe 30/12/2020 nilimsaidia majeruhi wa pikipiki ambaye alikuwa amegongwa na gari kumuwahisha hosptali kwa ajili ya Matibabu, aligongewa mitaa ya Sinza , so awali tulifika hosptali ya Palestina then palestina kwaissue ya mgonjwa ilivyo walituambia twende hosptitali ya Mwananyamala...
Hawa watumishi unaweza kuwatetea kwa nguvu kwa sababu hayajakukuta,Ila yakikukuta ndo utajua anachofanya JPM Ni sahihi kabisa kuwashughulikia.
 
Mbona hii hospital mnaioneaga sana yaani kila kiongozi nenda mwananyamala, nkuu nkoa nenda mwananyamala, wilaya nenda nyamala ect ect 3ct
 
Back
Top Bottom