Waziri wa Afya, nenda tena Hospitali ya Mwananyamala

Serikali iboreshe huduma za afya,maslahi ya watumishi yaongezwe,haiwezekani wanasiasa ,wabunge na wengineo wajilipe mishahara mikubwa huku kada nyingine zikiwa hoi.
Hawa madaktari hata morals ya kazi hawana.

Vifaa hakuna,madawa hakuna, gloves hakuna kila kitu hakuna.,
Dr.Gwajima ataenda hapo atapiga kelele tutamsifia lakini hakuna kitakachobadilika.,tulitaka mambo yaende sawa serikali iwe ya kwanza kubadilika.
 
Nadhani madaktari wanaopaswa kulaumiwa hapo ni wa kitengo cha emergency ambapo kwa nyakati za usiku wao ndio huwaona wagonjwa na kuwastabilize kabla ya kuwapeleka katika wodi husika.So emergency team ya hapo Mwananyamala means haikuwepo? Kuanzia wauguzi na madaktari? Kama ni hivyo basi hapo kuna shida.Wajaribu kuiga au kutengeneza emergency department kama za muhimbili upanga au Mloganzila...i have been there..wanafanya kazi nzuri
 
Nafikir umeshindwa kumuelewa watoa huduma ni wachache sio kwamba anahalalisha serikali iajiri fikiria hapo kuna dokta moja tu na watu walikuw wa 5 kweli asife hata mmoja?
Mkuu hapana. Hospital zetu nazijua sana. Pamoja na kuwa serikali haiwalipi vizuri na mazingira yao ni magumu sana lakini nao wana sehemu yao ya uzembe
 
Serikali iboreshe huduma za afya,maslahi ya watumishi yaongezwe,haiwezekani wanasiasa ,wabunge na wengineo wajilipe mishahara mikubwa huku kada nyingine zikiwa hoi...
Hizi kelele alipiga sana jamaa mmoja anaitwa Dr Ulimboka enzi za Kikwete. Matokeo yake akatekwa na kupigwa karibu kuuawa. Wananchi badala tuungane kum-suport tukabaki kushangaa.

Baadhi ya madaktari wenzake wakatoa tamko kuiunga mkono serikali. Matatizo mengine tunajitakia wenyewe na kila mtu atakumbana na madhila haya ya kuogopa kwa wakati wake. Hatujui kesho ni nani. Anaweza kuwa mimi au yule au wewe.
 
Umemaliza yote Mkuu.... Inasikitisha Sana kuona Watanzania wenzetu wakishupaza misuli ya shingo kuwalaumu Watumishi wa imma wa nchi hii huku wakishindwa kabisa kuwasapoti kudai hayo maslahi yao..... Mwaka wa sita Sasa bila maboresho ya maslahi yao,na Kuna maeneo mengine huko kwe hospitali za halmashauri madaktari wanaofanya ON CALL DUTIES hawalipwi allowances zao kwa madai kuwa pesa hakuna,huku wakilazimishwa kuendelea kufanya kazi.

Hawa watumishi wa umma ,ni binadamu wenzetu ambao wanahitaji maslahi bora ili waweze kuendesha maisha yao ya kila siku. Bila kujali maslahi yao, hawawezi kuwa na utulivu unaotakiwa kutimiza majukumu yao.

Niwashauri tu ,Watanzania wenzangu tuache kuwalaumu Watumishi wetu wa umma, badala yake tupaze sauti kuitaka serikali ya Rais Magufuli kuheshimu na kujali maslahi yao ili wawe na utulivu,furaha ya kufanya majukumu yao, watuhudumie vema.
ILA WATOA HUDUMA ZA UMMA TUJITATHIMINI,
MH. MAGUFULI HAWA WATU WAMEANZA KUJISAHAU HEBU ILE KAMBA YA CHUMA ULIYOWAFUNGA 2015 HEBU IFUNGE TENA MWAKA 2021 TUMBUA TUMBUA HAWA WATU MH RAIS...
 
Mkuu hapana. Hospital zetu nazijua sana. Pamoja na kuwa serikali haiwalipi vizuri na mazingira yao ni magumu sana lakini nao wana sehemu yao ya uzembe

Ishinikizeni Serikali iboreshe maslahi ya watumishi hao, iboreshe pia upatikanaji wa vitendea kazi alafu ndio uwalaumu.

Hao unaowalaumu kwa uzembe hapo ( kwe hospitali za umma) ndio hao hao wanatumiwa na hospitali binafsi ambazo unasifia huduma zao.
 
Sasa kwanini tuamue kufanya hivi kwa watu ambao ni hawakupaswa kufanyiwa vitendo kama hivi,
Kama unaona maslahi hamna tujaribu kuwaachia wenye wito wakufanya kazi hizi wafanye
Watu wasio na hatia wanaumia nachosisitiza
Usiombee hili likukute
 
Ukiona kazi haikulipi achana nayo usilazimishe,

Sekta ya afya ni sehemu nyeti sana, kama unahisi una tatizo na muajiri wako ni vema aidha kuomba likizo au kuacha lakini sio kunyanyasa wagonjwa.
 
Kuna kazi za wito inabidi watu waambiwe na si kuweka maslahi mbele mkuu hizi huduma wanapata wengi maskini na matajili waliokuwa nacho na wasiokuwa nacho.
 
Kasheshe iko palestina kwenye kujiungua,mambo yanayofanyika pale rushwa zinazoombwa na manesi shida tupu,serikali fanya mitego kwa manesi jaman sis wanyonge tunaumia,ili sijaadithiwa nimejionea mwenyew rushwa inagawiwa kwenye kibaraza Cha kupanda kwenda grofa ya kwanza wodin,na kuna giza pale taa hamna hatar tupu
 
Sasa kwanini tuamue kufanya hivi kwa watu ambao ni hawakupaswa kufanyiwa vitendo kama hivi,
Kama unaona maslahi hamna tujaribu kuwaachia wenye wito wakufanya kazi hizi wafanye
Watu wasio na hatia wanaumia nachosisitiza
Usiombee hili likukute

Ndugu, hii kauli ya eti "ni wito" isiwe kisingizio Cha kuminya maslahi ya hao watu, tambua na wao Wana familia za kuzihudumia.... Wito bila utulivu wa fikra haiwezekani.

Cha msingi ni kwa sisi Wananchi tunaoumizwa na hayo badala ya kuwalaumu watoa huduma hao, tuishinikize serikali iboreshe maslahi yao plus mazingira wanayofanyia kazi ili wasiathiriwe na msongo wa mawazo unaotokana na ugumu wa maisha ili watuhudumie vizuri.
 
Kuna kazi za wito inabidi watu waambiwe na si kuweka maslahi mbele mkuu hizi huduma wanapata wengi maskini na matajili waliokuwa nacho na wasiokuwa nacho.

Hakuna kazi ya wito siku hizi ndugu,hata hao watu wa dini wamegeuka wajasiriamali siku hizi....FUTA KABISA HIYO "MENTALITY"
 
Kwahiyo unaona akirudi ndo atamaliza tatizo. Tupunguze mihemko. Mbona hatujiulizi kwanini wahumu wa Afya wamefikia hapo?

Mnajua nao Wana familia, wanashida zao, wanamatarajio yao?

Sasa basi ili watibu vema basi umma uwape hayo
 
Nimevutiwa na hoja yako
 
Pole sana kwa kuyashuhudia hayo maswaibu, Pole zaidi zimuendee Mama aliyempoteza Mwanae.

Kwanza nyie mlitakiwa kutoa taarifa kwa uongozi wakati huohuo au pia mngepiga simu/kutuma msg kwa Waziri alishatoa namba zake za simu.

Maelezo yako yameeleweka lakini in case tungepata maelezo ya upande wa pili huenda tungemlalamikia mtu/mhimili mwingine kuliko mtoa huduma. Huenda huko alikokuwa alikuwa akitoa huduma kwa mgonjwa mwingine mwenye dharura.

Wafanyakazi sekta ya afya katika hospitali zetu ni wachache na wamebebeshwa mzigo mzito, Serikali hailioni hilo hata kufikiria kuwapa motisha imeshindwa badala yake imeongeza makato kwenye marejesho ya mkopo wa loan board na kuminya stahiki zao, katika hali hii usitegemee kuona wito.

Je, Umewahi kuona utendaji wa hospitali Kama MOI ulivyo? At least hapo MOI ukienda muda wote utapata huduma ila Siri iliyopo pale ni utaratibu motisha kwa Wafanyakazi wao.

Bado tunayo safari ndefu kubadili mfumo wetu wa kutenda kazi ktk taaaisisi za serikali na mojawapo ya mambo ya kuzingatia ni uboreshaji wa mazingira ya kazi, vitendea kazi na maslahi ya Wafanyakazi, Serikali ikikwepa hilo jukumu tusitegemee mabadiliko makubwa hata kama watumishi watatumbuliwa kila kukicha.

Happy New Year.. 2021
 
Hahaha kwa wale wageni nchi hii na msiojua tunafanya nini.

TUNAJENGA MAJENGO MENGI, HIZO HUDUMA MTAJIJUA WENYEWE.

Tuliwaambia tunajenga miundo mbinu, maendeleo ya vitu siyo watu.
 
Mbona hapo kuna unafuu njoo hapa mawilayani dakitari anapatikana siku mbili tu kwa wiki, ukipata emergency akikisha inangukia siku ya dakitari, ukiwa huna bahati basi unapoteza maisha au unatafuta private kwa gharama kubwa
Da,Hawa wahudumu wa afya ni wajinga,kwani kama wanadai ongezeko la mshahara wangetumia taratibu sahihi.Ni dhambi kusababisha mtu apoteze maisha,hiyo laana hawataikwepa.Wajirekebishe.
 
Hizi changamoto watu hawaelewi kabisa...tangu nianze kazi hosp flan ya serikali natimiza mwaka sasa sijawah pata on call allowance hata moja...na mshahara ulikuw wa november..na hii ndio january...ila tunaendelea kufanya kazi kwa kuw ni wajibu wetu despite na mazingira husika
 
Hispitali nyingi za serikali huduma zao za usiku ni tatizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…