Fantastic Beast
Member
- Feb 18, 2019
- 53
- 539
Mheshimiwa Waziri wa Afya, nikiwa kama "collateral" ambaye nina ndugu yangu anayefanya kazi pale Mloganzila Hospitali, naomba nikufikishie taarifa kwamba wafanyakazi wa pale hawajalipwa posho za UVIKO-19 (Risk Allowances) hata za wimbi 1 japokuwa hizo pesa mlishazilipa kulingana na tangazo mlilolitoa.
Inajulikana kwamba Hospitali ya Taifa Muhimbili (Upanga & Mloganzila), zina uongozi mmoja. Lakini cha kushangaza ni kwamba kwenye huu mgao wa pesa za UVIKO 19 wale wa Upanga wamepata posho zao zote za milipuko 3, wakati wale wa Mloganzila hawajapata hata za wimbi 1.
Nimesikia mwezi wa saba Mloganzila itaanza kujitegemea, lakini naomba nikuambie tuu sidhani uongozi wa mpito uliowekwa kama umeisaidia sana hiyo hospitalikuweza kujiendesha yenyewe. Hilo jengo ni "State-of-Art" facility, linahitaji zaidi ya siasa kuliendesha. Mojawapo ni staff motivation. Lakini ukienda pale wafanyakazi wa hapo wanachofurahia ni kiyoyozi lakini mioyoni mwao wana machungu yasiyoelezeka kutokana na ukandamizwaji wanaofanyiwa na uongozi wa Upanga, hili la posho za UVIKO ni sehemu tuu lakini wana madai mengine mengi mfano Over Time Allowances ambazo hawajalipwa mwaka mzima sasa toka mwaka jana January, na pale wanafanya kazi masaa 12 ya siku.
Ni hayo tuu Mheshimiwa, ukipendezwa lifuatilie hili pamoja na mengine mengi, otherwise naomba nikuambie tuu Mloganzila itakuwa "Failed Project" kama hamtachukua hatua za makusudi kuhakikisha inasimama kwenye mstari.