Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa ameifunga ofisi ya Idara ya Ardhi ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma na kuamuru Watumishi wa Idara hiyo kuhamia kwenye Ofisi za Kamishna wa Ardhi Mkoa.
Hatua hiyo inafuatia kukithiri kwa migogoro ya ardhi katika jiji hilo linalotajwa kuwa na kesi zaidi ya 3,000 za ugawaji wa viwanja kwa wamiliki zaidi ya mmoja.