Waziri wa Ardhi Ndejembi: Nyumba iliyojengwa kimakosa Iyumbu ivunjwe

Waziri wa Ardhi Ndejembi: Nyumba iliyojengwa kimakosa Iyumbu ivunjwe

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,536
Reaction score
7,194
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi amemwelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuchukua hatua za haraka za kuvunja nyumba iliyojengwa kimakosa katika kiwanja namba 1/31 kilichopo Block D, Iyumbu North jijini humo.

Waziri Ndejembi ametoa agizo alipotembelea eneo hilo baada ya kupata malalamiko kutoka familia ya marehemu Thobias Simon Msigwa ambaye ni mmliki halali wa viwanja 1/30, 1/31, 1/32 na 1/33 kitalu D, Iyumbu North jijini Dodoma baada ya kupokea malalamiko ya msimamizi wa mirathi.

Waziri Ndejembi amesisitiza kuwa mwenye hati halali ya kiwanja hicho ni msimamizi wa mirathi Bi. Prisca Lukas Lulambo ambaye ni msimamizi wa mirathi ya marehemu Thobias Simon Msigwa.

Kwa upande wake msimamizi wa mirathi Bi. Prisca Lukas Lulambo amesema kuwa aligundua kuwa eneo hilo limevamia mwaka 2021 na kugundua mvamizi ni Geogre Beno Mlonge na alienda kujiridhisha kwa jiji juu ya umiliki wake na kujulishwa umiliki wa kiwanja hicho ni wa Thobias Simon Msigwa.

 
Back
Top Bottom