Waziri wa Ardhi njoo Maswa kuna madudu mengi

Waziri wa Ardhi njoo Maswa kuna madudu mengi

Mwanantogakulya

Senior Member
Joined
Mar 18, 2025
Posts
157
Reaction score
155
Mheshimiwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Leonard Akwilapo, wananchi wa Wilaya ya Maswa wamepokea kwa masikitiko taarifa ya kuahirishwa kwa ziara yako. Wengi walikuwa na matumaini makubwa kuwa ujio wako ungekuwa mwanzo wa kupata ufumbuzi wa migogoro ya ardhi inayowatesa kwa miaka mingi.

Maswa ndiyo wilaya inayokabiliwa na migogoro mingi ya ardhi katika Mkoa wa Simiyu, hususan maeneo ya Maswa Mjini, Malampaka, Lalago, Nguliguli, Ipililo na Sangamwalugesha. Migogoro hiyo imekuwa chanzo cha migongano, kesi zisizoisha na malalamiko ya wananchi.

Pamoja na kuwepo kwa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya, wananchi wengi bado wanalalamikia ucheleweshaji wa maamuzi na changamoto mbalimbali katika utoaji wa haki. Hivyo, wanakuomba upange ziara ya kufika Maswa ili ujionee hali halisi na kusikiliza kero zao moja kwa moja badala ya kutegemea taarifa za mezani.
Masuala ya ardhi Maswa yanahitaji uamuzi wa haraka na usimamizi wa karibu wa Serikali. Wananchi wanaamini ujio wako utatoa matumaini mapya na kuchochea kupatikana kwa suluhisho la kudumu kwa migogoro hiyo.
 
Chanzo cha migogoro ya ardhi ni rushwa, siasa, matumizi mabaya ya madaraka, upendeleo, utapeli

Inapaswa idara ya ardhi waletwe wafanyakazi wengine, vunja baraza la ardhi na kuunda jingine, fukuza Mkuu wa wilaya
 
Back
Top Bottom