KERO Waziri wa Ardhi uje utusaidie Kata ya Kihonda Yespa – Morogoro kuna migogoro mingi ya ardhi

KERO Waziri wa Ardhi uje utusaidie Kata ya Kihonda Yespa – Morogoro kuna migogoro mingi ya ardhi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Yespa1.jpeg

Yespa.jpeg
Kilio cha wanyonge sisi Wakazi wa Kihonda Yespa, Manispaa ya Morogoro nyuma ya tuta la mwendokasi, tunaomba maafisa ardhi waje kutatua migogoro mikubwa huku mtaani kwetu, kuna kiongozi anasema yeye ni Diwana Kata ya mabibo na ndiye Naibu Meya Manispaa ya Ubungo.

Kaja maeneo tuliojenga tangu 2019 anadai ni maeneo yake kanunua Mwaka 2006 cha kushangaza kajitokeza mwaka huu 2026 kudai maeneo yake na kesi kapeleka Baraza la Kata ya Kihonda kafungua shauri na kulifuta ili aandae ushahidi wa kutosha ndani ya miezi miwili akidai mashaidi wake wengine wapo nnje ya nchi.

Wasiwasi wetu Maafisa Ardhi Manispaa ya Morogoro taarifa za hilo faili tumezipata zinaandaliwa dokumenti za kutengenezwa na baadhi ya Maafisa wasio waaminifu, hivyo wawe makini pia.

Waziri mwenye dhamana na Manaibu wake wafike Kata ya Kihonda Yespa kuna madudu makubwa sana.

Viwanja zaidi ya 70 vina migogoro mikubwa tukiwa tumeuziwa na mtu mmoja tu kama ‘sqwater’ na ametoroka hajulikani alipo mpaka sasa tangu Mwaka 2019.
 
Back
Top Bottom