Black Legend
Senior Member
- Jul 28, 2015
- 174
- 301
Taasisi ya Elimu TET au maarufu TIE, ni chombo cha serikali kilichopewa jukumu la kukuza na kuendeleza Elimu kwa upande wa UKUZAJI MITAALA na UANDAAJI WA MAUDHUI YA MITAALA.
Jambo la kusikitisha saana , kumekuwa na madudu mengi saana katika taasisi hii muhimu katika Elimu yetu. Ni jukumu kuu la Waziri mwenye dhamana ya wizara ya Elimu kutumia jicho na kufanya marekebisho makubwa ya Utendaji wa chombo hiki.
Yafuatayo ni madudu machache yanayoendelea kwenye taasisi hii nyeti ya Elimu:
1. Kutoa nafasi za kazi kwa upendelea bila kuangalia vigezo na taaluma ya watu( mara nyingi kazi katika idara hii hutolewa kwa vi memo).
2. Maandalizi ya nyaraka kwa kutozingatia ubora wa kazi.....kazi nyingi za TET/ TIE hufanywa kwa zimamoto bila kuzingatia ubora wa kazi husika. Na mara nyingine kazi kupewa watu wasio wataalamu wa Maeneo husika.
3. Ucheleweshaji wa malipo na kulipa malipo yasiyo stahili. Kwa mfano, Kuna kazi zinafanyika, wataalamu toka mikoa mbalimbali wanakuaanyika kufanya kazi hiyo wakitegemea pia katika kuishi eneo mbali na maeneo yao halisi ya kazi basi watapewa posho za stahiki kwa wakati, lakini cha ajabu posho hizo huchukua mpaka miezi 4 kuja kulipwa. Hii inachangia utendaji MBOVU wa ukuzaji na uandaaji nyaraka muhimu za Elimu kama vitabu nk.
HAYA NI BAADHI TU YA MADUDU YA TAASISI HII MUHIMU YA SERIKALI, KUNA, MENGI SAANA YA HOVYO. NI JUKUMU LA WAZIRI NA WADAU WENGINE WENYE DHAMANA YA ELIMU YA NCHI YETU KUANGALIA NA KUINGILIA KATI UTENDAJI MBOVU WA TAASISI HII YA ELIMU---- TET/TIE .
Nawasilisha✍🏽🙏🏽