DOKEZO Waziri wa Elimu, huu mtindo wa Kubakiza watoto shuleni wakati wa likizo ni Sahihi?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Ile tu kuwa kwenye mazingira ya shule, inampa utayari kwa mtihani; akija nyumbani na kukaa muda mrefu halafu arudi shule, inaweza kumchukua muda kuwa na ule utayari wa kufanya mtihani
Kusoma siyo kuwa tayari kufanya mtihani na shule haziko kwa ajili ya kuwapima watoto kufanya mtihani. Kusoma kuna lengo moja tu, kumuelimisha. Mtihani ni sehemu ndogo mno ya kupima kama mtoto ameelimika. Na zaidi, likizo ni muhimu sana sana na sehemu ya kusoma.
 
Uko sahihi, ili hoja yako iwe na mashiko italazimu mfumo mzima wa elimu na ajira ufanyiwe marekebisho.
 
Kuwa mwalimu wa chuo kikuu unatakiwa uwe na GPA ya ngapi?
Kuwa mwalimu wa chuo inatakiwa uwe na uelewa wa kufundisha yale yanayohusika na uwe na uwezo wa kuyawasilisha ili yaeleweke. Hayo mambo ya GPA ni kigezo kidogo sana kwani hata mwanafunzi wa darasa lla saba anaweza kupata cheti chenye GPA husika.
 
Yaani kuna wazazi wanaona watoto nyumbani ni usumbufu,na hao ndio wanafurahia watoto kubaki shuleni huko,ili wawe huru.

Baadae watoto wakiharibika wanaanza kulaumu walimu tena,wakati wanakwepa jukumu lao
 
Kuwa mwalimu wa chuo inatakiwa uwe na uelewa wa kufundisha yale yanayohusika na uwe na uwezo wa kuyawasilisha ili yaeleweke. Hayo mambo ya GPA ni kigezo kidogo sana kwani hata mwanafunzi wa darasa lla saba anaweza kupata cheti chenye GPA husika.
Uko sahihi, ila kwa mazingira ya sasa ni ufaulu kwanza; ndio maana matokeo yanapotoka huwa tunawataja wale Tanzania one
 
Uko sahihi, ili hoja yako iwe na mashiko italazimu mfumo mzima wa elimu na ajira ufanyiwe marekebisho.
Elimu ya Tanzania ilitakiwa ifumuliwe tangu juzi, imechelewa. Tulikosea sana siku za nyuma pale waalim na wasomi wengine walipoanzisha kitu kinachitwa ''tuition'' na watoto wakawa wanaenda kujifunza baada ya saa za shule. Kwennye hizo sehemu, mara nyingi walikuwa wanakaririshwa na kufunzwa kujibu maswali ya past examination papers ili wafaulu mitihani. Matokea yake tumekuwa na kizazi kinachojali zaidi kupasi mitihani na siyo kuelewa yale yanayofundishwa. Angalia kizazi cha sasa hivi, wengi hawatafakari mambo bali huyafyonza kama yalivyo. Matokeo ya kukariri.
 
Kufanya mabadiliko inaweza kuchukua muda mrefu sana, kwa sababu itahitajika kuwepo na fedha ya kutosha
 
Kufanya mabadiliko inaweza kuchukua muda mrefu sana, kwa sababu itahitajika kuwepo na fedha ya kutosha
Mkuu fedha tunazo. Trust me! Hivi unadhani serikali yetu haina fedha? Laiti ungejua zinavyopigwa ndiyo ungejua hata misaada tunayopata tusingestahili. Hebu tuache ufisadi na vipaumbele vya kijinga tunavyoweka kwenye mipango... nenda kwenye bunge. Tunahitaji kuwa na wabunge wengi namna hii? Nenda kwa wilayani na mikoani... vyeo kibao. Makundi haya yote yanatumia magari ya bei mbaya, yanasafiri kwenye madaraja ya business.. yaani sehemu za kukata matumizi ni nyingi mno.
 
Hawa wanatengeneza mradi wa kuvuna hela tu,waulize kwanini hawamalizi muhula?
 
Tatizo ni mfumo, sasa ni nani wa kuubadilisha?
 
Ni njia ya kupiga Pesa, na Bado naamini Elimu ilikuwa zamani sana kabla ujinga haujaanza,
 
Ni njia ya kupiga pesa, watoto wanakaririshwa hakuba kupumzika, na ndio maana nasema siku mitihani ikifutwa ndio tutaanza kuiona elimu bora
 
Njia ya kupiga pesa
 
Ni wakati wa kubadili mfumo wa elimu, ikiwezekana siku za kwenda shule ziwe nne badala ya tano kwa wiki.

Ijumaa iwe ni siku ya michezo tu, pia masomo yawe kwa njia ya vitendo zaidi badala ya rote learning ambayo inadumaza watoto.
Kabisa, wajinga hawatakuelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…