DOKEZO Waziri wa Elimu, huu mtindo wa Kubakiza watoto shuleni wakati wa likizo ni Sahihi?

DOKEZO Waziri wa Elimu, huu mtindo wa Kubakiza watoto shuleni wakati wa likizo ni Sahihi?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Ile tu kuwa kwenye mazingira ya shule, inampa utayari kwa mtihani; akija nyumbani na kukaa muda mrefu halafu arudi shule, inaweza kumchukua muda kuwa na ule utayari wa kufanya mtihani
Kusoma siyo kuwa tayari kufanya mtihani na shule haziko kwa ajili ya kuwapima watoto kufanya mtihani. Kusoma kuna lengo moja tu, kumuelimisha. Mtihani ni sehemu ndogo mno ya kupima kama mtoto ameelimika. Na zaidi, likizo ni muhimu sana sana na sehemu ya kusoma.
 
Uko sahihi, ili hoja yako iwe na mashiko italazimu mfumo mzima wa elimu na ajira ufanyiwe marekebisho.
 
Kuwa mwalimu wa chuo kikuu unatakiwa uwe na GPA ya ngapi?
Kuwa mwalimu wa chuo inatakiwa uwe na uelewa wa kufundisha yale yanayohusika na uwe na uwezo wa kuyawasilisha ili yaeleweke. Hayo mambo ya GPA ni kigezo kidogo sana kwani hata mwanafunzi wa darasa lla saba anaweza kupata cheti chenye GPA husika.
 
Wazazi WA Siku hizi sio walezi wanajua kuzaa TU ndo maana maadli yanashuka tunasingia Ulaya,Lea mwanao mwenyewe Kaa nae likizo msome Mtoto ujue tabia zake
Mnataka walimu wawaleee na housemade from January to December,Hivi hamuoni haya na Hilo suala Hapo ukute Kuna mzazi kaliunga mkono la watoto kubaki shule
Katoto ka std 4 kanabaki kufanya Nini?!!lini wazazi tutajua watoto wety tabia zao?uwezo wao?madhaifu Yao?!
Yaani tunakoelekea ni mtihani Sana Mungu atulinde...!!!
Yaani kuna wazazi wanaona watoto nyumbani ni usumbufu,na hao ndio wanafurahia watoto kubaki shuleni huko,ili wawe huru.

Baadae watoto wakiharibika wanaanza kulaumu walimu tena,wakati wanakwepa jukumu lao
 
Kuwa mwalimu wa chuo inatakiwa uwe na uelewa wa kufundisha yale yanayohusika na uwe na uwezo wa kuyawasilisha ili yaeleweke. Hayo mambo ya GPA ni kigezo kidogo sana kwani hata mwanafunzi wa darasa lla saba anaweza kupata cheti chenye GPA husika.
Uko sahihi, ila kwa mazingira ya sasa ni ufaulu kwanza; ndio maana matokeo yanapotoka huwa tunawataja wale Tanzania one
 
Uko sahihi, ili hoja yako iwe na mashiko italazimu mfumo mzima wa elimu na ajira ufanyiwe marekebisho.
Elimu ya Tanzania ilitakiwa ifumuliwe tangu juzi, imechelewa. Tulikosea sana siku za nyuma pale waalim na wasomi wengine walipoanzisha kitu kinachitwa ''tuition'' na watoto wakawa wanaenda kujifunza baada ya saa za shule. Kwennye hizo sehemu, mara nyingi walikuwa wanakaririshwa na kufunzwa kujibu maswali ya past examination papers ili wafaulu mitihani. Matokea yake tumekuwa na kizazi kinachojali zaidi kupasi mitihani na siyo kuelewa yale yanayofundishwa. Angalia kizazi cha sasa hivi, wengi hawatafakari mambo bali huyafyonza kama yalivyo. Matokeo ya kukariri.
 
Kufanya mabadiliko inaweza kuchukua muda mrefu sana, kwa sababu itahitajika kuwepo na fedha ya kutosha
 
Kufanya mabadiliko inaweza kuchukua muda mrefu sana, kwa sababu itahitajika kuwepo na fedha ya kutosha
Mkuu fedha tunazo. Trust me! Hivi unadhani serikali yetu haina fedha? Laiti ungejua zinavyopigwa ndiyo ungejua hata misaada tunayopata tusingestahili. Hebu tuache ufisadi na vipaumbele vya kijinga tunavyoweka kwenye mipango... nenda kwenye bunge. Tunahitaji kuwa na wabunge wengi namna hii? Nenda kwa wilayani na mikoani... vyeo kibao. Makundi haya yote yanatumia magari ya bei mbaya, yanasafiri kwenye madaraja ya business.. yaani sehemu za kukata matumizi ni nyingi mno.
 
Unazungumzia uzoefu au utaalam?

Mtaala pamoja na mohtasari ikitekelezwa kama ilivyopangwa, muda unatosha kabisa!

Siku za kusoma ni 194 ambazo zimetokana na masaa ya kufundisha na muda wa mtoto kupumzika. Hili lenu la kuona muda ni mdogo unatokana na ama hamjui kuandaa namna ya kufundisha na kujifunza ama mnajipa kazi ambazo zinawachosha na hazileti ufanisi na maarifa kwa mtoto.
Hawa wanatengeneza mradi wa kuvuna hela tu,waulize kwanini hawamalizi muhula?
 
Mkuu fedha tunazo. Trust me! Hivi unadhani serikali yetu haina fedha? Laiti ungejua zinavyopigwa ndiyo ungejua hata misaada tunayopata tusingestahili. Hebu tuache ufisadi na vipaumbele vya kijinga tunavyoweka kwenye mipango... nenda kwenye bunge. Tunahitaji kuwa na wabunge wengi namna hii? Nenda kwa wilayani na mikoani... vyeo kibao. Makundi haya yote yanatumia magari ya bei mbaya, yanasafiri kwenye madaraja ya business.. yaani sehemu za kukata matumizi ni nyingi mno.
Tatizo ni mfumo, sasa ni nani wa kuubadilisha?
 
Mheshimiwa Waziri,

Kumekuwa na mtindo wa wamiliki wa shule kuamua tu kwa utashi wao kubakiza watoto shuleni(madarasa ya mitihani) kwa kigezo kwamba wapate muda wa kumalizia mitaala tena bila kushirikisha wazazi huku wakiwa tayari wamepanga na gharama zao.

Hivi walimu wanashindwa vipi kumaliza mtaala kwenye muda uliopangwa?Kibaya zaidi wamekuwa wakiongeza gharama za ziada za Tuition fee na transport hasa kwa shule binafsi.

Sasa kama lengo la walimu ni kumaliza mtaala hili si jukumu lao,kwanini gharama zirudi kwa mzazi?

Je ni sahihi mtoto kusoma bila kupumzika?Kuna watoto wanasoma mbali na wazazi wanahitaji kuonana na wazazi wao ambao hawajawaona kwa muda mrefu,sasa kumshikilia mtoto shuleni muda mrefu kisaikolojia imekaaje?

Mimi binafsi naona shule zimeamua kubuni tu mradi wa kujipatia kipato kwa kigezo cha kumaliza mitaala.

Tayari kuna shule zimeshatoa taarifa kwamba darasa la nne hawatafunga shule ili waendelee kufundishwa,Je mmeruhusu?

Tunaomba hili suala lizuiliwe kisheria na sio kwa matamko ya kila mara maana nakumbuka mwaka Jana ulitoa tamko la kuzuia watoto kubakizwa shuleni ila naona linajirudia tena.

Pia soma: Waziri wa Elimu Prof. Mkenda, sisitiza umuhimu wa kutowabakiza watoto shule kipindi cha likizo

Ahsante.
Ni njia ya kupiga Pesa, na Bado naamini Elimu ilikuwa zamani sana kabla ujinga haujaanza,
 
Asante sana mdau kwa kuleta uzi huu. Kweli kabisa hii tabia imeanza shamiri mno kuna shule wao wameamua darasa la 4,6 na 7 jumamosi wawe shule na likizo kisingizio kuwa wanamitihani na garama wameongeza kama ulivyosema hapo juu.

Hawa watoto wanahitaji kupumzika nadhani mh Waziri nivizuri ukatusaidia toa muongozo kwenye hizi shule.

Huu ni uhuni wa kujiongezea mapato tu sababu hata ukifatilia unakuta walimu hawapo wote mara wanapeana zamu kwenda kifupi ni kuzuga tu hizo siku.
Ni njia ya kupiga pesa, watoto wanakaririshwa hakuba kupumzika, na ndio maana nasema siku mitihani ikifutwa ndio tutaanza kuiona elimu bora
 
Ni mtindo wa kipuuzi uliojengeka na kuzoeleka. Inakuwa haina maana kuwa na likizo kwa mwanafunzi, huko ni kumchosha.

Unakuta wanafunzi wanafululiza kusoma mwaka mzima huku hakuna cha maana wanachofundishwa zaidi ya kukaririshwa kama kasuku.

Hawa ni watoto wadogo inawapasa kupumzika baada ya kusoma mada nyingi kwa muhula mzima.

Akili inatakiwa ipumue ili kupokea maarifa mapya
Njia ya kupiga pesa
 
Ni wakati wa kubadili mfumo wa elimu, ikiwezekana siku za kwenda shule ziwe nne badala ya tano kwa wiki.

Ijumaa iwe ni siku ya michezo tu, pia masomo yawe kwa njia ya vitendo zaidi badala ya rote learning ambayo inadumaza watoto.
Kabisa, wajinga hawatakuelewa
 
Back
Top Bottom