DOKEZO Waziri wa Elimu, huu mtindo wa Kubakiza watoto shuleni wakati wa likizo ni Sahihi?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Sisi tulikuwa shule ratiba zinaisha saa saba mchana haooo kengele ikilia nduki home kuwahi kiporo xha wali wa jana. Nikishafika ni kubadili nguo, kula kufua uniform halafu taratibu naingia kitaa kutafuta masela zangu tuendelee ma ratiba zetu na majukumu ya utoto.

Yaani ilikuwa ni unyama fulani hivi wa raha.
 
Ndo maana panakuwa na utofauti kati ya wanafunzi wa Gov na Priv, sababu Priv lazima ajue kusoma na kuandika ndo aende Class One.
Gov si lazima ndo maana kuna mtu anafika la 7 hajui soma na kuandika
 
Najiuliza nini kimeongezeka katika mitaala. Kwann watoto wanakuwa na mambo mengi kupita umri wao?

Mtoto anaamka asubuhi ya saa kumi na moja halafu anarudi saa kumi na mbili nyumbani huyu mtoto hajatimiza miaka hata 10,hivi hapa jamani wanajamii ni tumelogwa ama tunatafuta laana za MUNGU?

Kuna mtoto ambaye anakuzwa na mfumo huu atakuja kuwa mwanajamii anayependa maisha ya kifamilia na kujenga ustawi kweli?!
 
Ni njia ya kupiga pesa, watoto wanakaririshwa hakuba kupumzika, na ndio maana nasema siku mitihani ikifutwa ndio tutaanza kuiona elimu bora
Hata mimi kwa Bongo ikipendekezwa mitihani kufutwa nitaunga mkono. Tutafute njia nyingine ya kupima watahiniwa. Au kama watafanya mitihani basi structure na contents zake zibadilishwe kabisa. Tupime wanafunzi kutafakari na siyo wanavyojua kukariri.
 
Kabisa ni sawa na kulaumu pombe ina madhara kisha kuwalaumu kiwanda cha kutengeneza beer badala ya watumiaji wa bia.
 
Mbona umecomment kwa kutoheshimu mawazo ya mwenzako halafu kama unamjibu kwa dharau na chuki debe nzima. Punguza hasira na jazba huu ni mjadala wa kijamii sio mjadala wa mtu binafsi.
 
Hoja muhimu sana hii.
 
Mzaz mvivu sana wewe yan unaona raha kujiachia kwenye makochi hapo mwanao huna hata ham nae.... Ngoja arudi ukute amebadili jinsia
 
Hii ni akili kubwa sana, ulipaswa kuwa waziri wa elimu, decition making zako zingeleta manufaa kwa taifa.
Mnaona mambo rahis eeeh hio elimu yakukariri tu mashule hayana vitabu nachaki leo uanzishe kusoma kwaprojector, demonstration, laboratory.... Nchi kama inashindwa kusambaza maji mkoa wamwanza wenye ziwa utaweza hayo
 
Sijui waliwatafuta wa kazi gani. Yaani kuna mtu anapata watoto ili jamii isimuulize kuwa kwann hana mtoto. Mzazi wa kweli utamjua kwa namna analea mtoto wake.

Wengi siku hizi ni incubators sio walezi wa watoto kabisa. Sijui ni shida kula hawa kuku wa kisasa.
 
Na hio ndio ilikuwa inajenga afya na akili,kumudu mazingira pamoja na kujenga marafiki na ushirikiano.

Sasahivi mtoto ukumuuliza mtoto wa nyumba ya jirani hamjui
 
Ndo maana panakuwa na utofauti kati ya wanafunzi wa Gov na Priv, sababu Priv lazima ajue kusoma na kuandika ndo aende Class One.
Gov si lazima ndo maana kuna mtu anafika la 7 hajui soma na kuandika
Kama itatekelezwa ipasavyo itasaidia
 
Mambo mengi,madaftari makubwa wakati sisi kutumia counter books ilikuwa secondary sikihizi la nne amejaza begi limejaa makaunta
 
Anataka awe na mtoto wakati huohuo aishi kama hana mtoto,inashangaza
 
Mkuu usijali kushambuliwa,humu kuna wajinga wapo wanaishi magetoni wala hawafikirii kuoa wala kuolewa,wao wakiamka na kula na kulala inatosha ndio maisha

Wengine kataa ndoa,wengine ma- wimpy kids sasa lini atawaza kuhusu hatma ya watoto?
Bonge la point
 
Pengine wanataka watoto wapate muda mwingi zaidi wa kufundishwa mapenzi ya..
Kwakweli hata mimi naanza kuhisi. Mtu mwenye akili timamu hiwezi lazimisha kukaa na watoto wa watu hadi kipindi cha likizo wakati wanatakiwa muda huo kutumia na familia zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…