Hongera mkuu.Mkuu asante,nilikuwa safarini leo kumchukua mtoto nafika nyumbani ndio napewa taarifa kwamba waziri kazuia,kwa pamoja tumefanikiwa katika hili.
Pongezi nyingi ziende kwa uongozi wa JF
Maxence Melo and Team!
Asante mkuu,sio mbaya acha tusimamie haki ya mtoto kupumzika,hata nyie najua mnataka kilicho bora kwa watoto piaHongera mkuu.
Sisi wengine watoto wetu wapo kayumba na darasa la mtihani.
Acha waendeleee tuu kusoma.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa mkuu.Asante mkuu,sio mbaya acha tusimamie haki ya mtoto kupumzika,hata nyie najua mnataka kilicho bora kwa watoto pia
Mbona sie tulifaulu tu bila kubakizwa shule na kufundishwa jumamosi na jumapili? Kuna kitu haipo sawa tukubali. Watoto wanahitaji muda wa kusoma na muda wa kupumzika. Hii sio sawa kwa ukuaji wao kimwili na kiakili.Sitetei lakini najaribu kuzungumzia uhalisia, nani asiyetaka mwanae afanye vizuri..?
Kabisa mkuu... Hii hali sio ya kuilea. Tunawaharibia watoto future... Wanakosa hata muda wa ku synthesise kile wanachondishwa, wanameza tuNina hakika wewe ni mwalimu wa Diamond na umehisi kama maslahi yako yanahatarishwa,
Ikiwa mtu mzima tu anapumzika sembuse mtoto. Sisi tulisoma elimu hiyo hiyo na likizo tulikaa majumbani, hatukwenda shule Jumamosi na Jumapili lakini tulimaliza na leo tuna watoto. Nini cha mno kilichobadilika kwa sasa?
Exactly. Mie sikuwahi soma tuition hata moja na nimefanya vizuri, na likizo zote nilikuwa naenda nyumbani. What's so special kwa mitaala ya leo? Something is wrong somewhere.Tunapenda wafanye vizuri ila kwa utaratibu
Oogh afadhali... Watoto wapumzishwe jamani. HeeeMkuu ahsante kwa Uzi wako,naona waziri wa elimu kapigilia msumari ,watoto waende likizo
Ili watoto wabakizwe shule wakati wa likizo ni lazima wazazi na shule wakubaliane kwenye kikao cha wazazi wa darasa husika.Mheshimiwa Waziri,
Kumekuwa na mtindo wa wamiliki wa shule kuamua tu kwa utashi wao kubakiza watoto shuleni(madarasa ya mitihani) kwa kigezo kwamba wapate muda wa kumalizia mitaala tena bila kushirikisha wazazi huku wakiwa tayari wamepanga na gharama zao.
Hivi walimu wanashindwa vipi kumaliza mtaala kwenye muda uliopangwa?Kibaya zaidi wamekuwa wakiongeza gharama za ziada za Tuition fee na transport hasa kwa shule binafsi.
Sasa kama lengo la walimu ni kumaliza mtaala hili si jukumu lao,kwanini gharama zirudi kwa mzazi?
Je ni sahihi mtoto kusoma bila kupumzika?Kuna watoto wanasoma mbali na wazazi wanahitaji kuonana na wazazi wao ambao hawajawaona kwa muda mrefu,sasa kumshikilia mtoto shuleni muda mrefu kisaikolojia imekaaje?
Mimi binafsi naona shule zimeamua kubuni tu mradi wa kujipatia kipato kwa kigezo cha kumaliza mitaala.
Tayari kuna shule zimeshatoa taarifa kwamba darasa la nne hawatafunga shule ili waendelee kufundishwa,Je mmeruhusu?
Tunaomba hili suala lizuiliwe kisheria na sio kwa matamko ya kila mara maana nakumbuka mwaka Jana ulitoa tamko la kuzuia watoto kubakizwa shuleni ila naona linajirudia tena.
Pia soma: Waziri wa Elimu Prof. Mkenda, sisitiza umuhimu wa kutowabakiza watoto shule kipindi cha likizo
Ahsante.
Walimu wanazembea kumaliza mitaala wakijua watafidia kwenye likizo na malipo ya ziada juuExactly. Mie sikuwahi soma tuition hata moja na nimefanya vizuri, na likizo zote nilikuwa naenda nyumbani. What's so special kwa mitaala ya leo? Something is wrong somewhere.
Asante kwa ushauri hata hivyo Waziri husika tayari ameshatoa tamko la kuzuia watoto kubakizwa shuleniIli watoto wabakizwe shule wakati wa likizo ni lazima wazazi na shule wakubaliane kwenye kikao cha wazazi wa darasa husika.
Kama haijafanyika hivyo uamuzi wa kuwabakiza watoto shuleni ni batili. Wewe fika ofisi ya AFISA ELIMU KATA wa kata ilimo shule yako utapata msaada.
Na wanafanya hivyo makusudi kwa kuwa nadhani wanachaji remedial classes so kwao ni chanzo cha mapatoWalimu wanazembea kumaliza mitaala wakijua watafidia kwenye likizo na malipo ya ziada juu
Kwa kweli hata mimi utaratibu huuAsante sana mdau kwa kuleta uzi huu. Kweli kabisa hii tabia imeanza shamiri mno kuna shule wao wameamua darasa la 4,6 na 7 jumamosi wawe shule na likizo kisingizio kuwa wanamitihani na garama wameongeza kama ulivyosema hapo juu.
Hawa watoto wanahitaji kupumzika nadhani mh Waziri nivizuri ukatusaidia toa muongozo kwenye hizi shule.
Huu ni uhuni wa kujiongezea mapato tu sababu hata ukifatilia unakuta walimu hawapo wote mara wanapeana zamu kwenda kifupi ni kuzuga tu hizo siku.
Sikubaliana kabisa mtoto au mwanafunzi kubaki shuleni wakati wa likizo,la sivyo kusingekuwa na kupumzikaKuna kijana wangu mmoja yuko la saba, hivi karibuni nikajulishwa hawatarudi mpaka tareh.23; mi nimeona ni vizuri tu kwa faida yake, kwa sababu muda uliobaki ni mfupi sana kwa mtihani, akija nyumbani atachanganya mafaili au kupoteza ile mudi ya kufanya mtihani.
Mwanajeshi ili ashinde vitani, inabidi abaki kambini apate mafunzo, akirudi kwa mkewe alafu kesho aende vitani atashindwa.
Kwa mtazamo wangu mi naona ni wazo jema; hiyo michango midogo isikuumize, bali unawekeza kwa mwanao. Hutaki, muache awe bogus.
Swali la kwenda shule jumamosi na jumapili sikubali ila jumatatu hadi ijumaa watakua wanafanya nini..?Mbona sie tulifaulu tu bila kubakizwa shule na kufundishwa jumamosi na jumapili? Kuna kitu haipo sawa tukubali. Watoto wanahitaji muda wa kusoma na muda wa kupumzika. Hii sio sawa kwa ukuaji wao kimwili na kiakili.
Ikiwemo na masomo ya ziada, na mitihani ya mara kwa maraTunapenda wafanye vizuri ila kwa utaratibu
Mimi niwe Sina watoto pole sana likizo ni likizoWatoto wako wanafanya nini likizo nyumbani?
Kwanza hauna watoto,wewe ndiyo mtoto unataka ubaki nyumbani kuzurura
Siku za masomo wafundishwe ila wikiend waachwe wapumzike pia washiriki kazi za nyumbani. Masomo sio shuleni tu hata nyumbani ni sehemu ya kufundishwa uwajibikaji na majukumu mbali mbaliSwali la kwenda shule jumamosi na jumapili sikubali ila jumatatu hadi ijumaa watakua wanafanya nini..?
Kuna mtu anakuambia jumatatu hadi jumapili za mwezi mzima akae na watoto nyumbani eti wanapumzika huo ni ujingaSiku za masomo wafundishwe ila wikiend waachwe wapumzike pia washiriki kazi za nyumbani. Masomo sio shuleni tu hata nyumbani ni sehemu ya kufundishwa uwajibikaji na majukumu mbali mbali