DOKEZO Waziri wa Elimu, huu mtindo wa Kubakiza watoto shuleni wakati wa likizo ni Sahihi?

DOKEZO Waziri wa Elimu, huu mtindo wa Kubakiza watoto shuleni wakati wa likizo ni Sahihi?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Sitetei lakini najaribu kuzungumzia uhalisia, nani asiyetaka mwanae afanye vizuri..?
Mbona sie tulifaulu tu bila kubakizwa shule na kufundishwa jumamosi na jumapili? Kuna kitu haipo sawa tukubali. Watoto wanahitaji muda wa kusoma na muda wa kupumzika. Hii sio sawa kwa ukuaji wao kimwili na kiakili.
 
Nina hakika wewe ni mwalimu wa Diamond na umehisi kama maslahi yako yanahatarishwa,

Ikiwa mtu mzima tu anapumzika sembuse mtoto. Sisi tulisoma elimu hiyo hiyo na likizo tulikaa majumbani, hatukwenda shule Jumamosi na Jumapili lakini tulimaliza na leo tuna watoto. Nini cha mno kilichobadilika kwa sasa?
Kabisa mkuu... Hii hali sio ya kuilea. Tunawaharibia watoto future... Wanakosa hata muda wa ku synthesise kile wanachondishwa, wanameza tu
 
Mheshimiwa Waziri,

Kumekuwa na mtindo wa wamiliki wa shule kuamua tu kwa utashi wao kubakiza watoto shuleni(madarasa ya mitihani) kwa kigezo kwamba wapate muda wa kumalizia mitaala tena bila kushirikisha wazazi huku wakiwa tayari wamepanga na gharama zao.

Hivi walimu wanashindwa vipi kumaliza mtaala kwenye muda uliopangwa?Kibaya zaidi wamekuwa wakiongeza gharama za ziada za Tuition fee na transport hasa kwa shule binafsi.

Sasa kama lengo la walimu ni kumaliza mtaala hili si jukumu lao,kwanini gharama zirudi kwa mzazi?

Je ni sahihi mtoto kusoma bila kupumzika?Kuna watoto wanasoma mbali na wazazi wanahitaji kuonana na wazazi wao ambao hawajawaona kwa muda mrefu,sasa kumshikilia mtoto shuleni muda mrefu kisaikolojia imekaaje?

Mimi binafsi naona shule zimeamua kubuni tu mradi wa kujipatia kipato kwa kigezo cha kumaliza mitaala.

Tayari kuna shule zimeshatoa taarifa kwamba darasa la nne hawatafunga shule ili waendelee kufundishwa,Je mmeruhusu?

Tunaomba hili suala lizuiliwe kisheria na sio kwa matamko ya kila mara maana nakumbuka mwaka Jana ulitoa tamko la kuzuia watoto kubakizwa shuleni ila naona linajirudia tena.

Pia soma: Waziri wa Elimu Prof. Mkenda, sisitiza umuhimu wa kutowabakiza watoto shule kipindi cha likizo

Ahsante.
Ili watoto wabakizwe shule wakati wa likizo ni lazima wazazi na shule wakubaliane kwenye kikao cha wazazi wa darasa husika.

Kama haijafanyika hivyo uamuzi wa kuwabakiza watoto shuleni ni batili. Wewe fika ofisi ya AFISA ELIMU KATA wa kata ilimo shule yako utapata msaada.
 
Ili watoto wabakizwe shule wakati wa likizo ni lazima wazazi na shule wakubaliane kwenye kikao cha wazazi wa darasa husika.

Kama haijafanyika hivyo uamuzi wa kuwabakiza watoto shuleni ni batili. Wewe fika ofisi ya AFISA ELIMU KATA wa kata ilimo shule yako utapata msaada.
Asante kwa ushauri hata hivyo Waziri husika tayari ameshatoa tamko la kuzuia watoto kubakizwa shuleni
 
jibu rahisi mnaulizwa huyo aliyetoa agizo mtoto wake anasoma humo!!huku kitaa watoto wa maskini hawana wa kuwasemea wamebaki yatima kwenye nchi Yao kama wakimbizi maana angalia hao watawala wangekuwa watoto wao wanasoma hizi shule za ufagio na kidumu elimu yetu ingepewa uthamani Sasa wanasiasa wametufanya mazombi ambayo kila watu wenye akili wakiwaamsha bado yanarudi kule kule,yaani kutwa nzima mtu haiwezi kuwaza hatima ya mtoto wake Kwa kesho yake ,yaani Simba Yanga .
 
Mnasaidiwa bado mnaleta ngebe, yakifeli lawama kwa walimu tena.

Kama ulikua unataka kuonana na mwanao ungempeleka day schools. Nyie kina dady mna lawama sana kisa hujamuona junya miezi 2 tu ushaanzisha uzi aisee.

Acha dogo apige kitabu, form four anarudi home kufanya nini, mda wa kumpuzika anao wa kutosha. November hapo anamaliza mtakaa nae hadi mumchoke. Form two mapemaa october anarudi nyumbani.

Std 7 ndo mwezi wa 9 keshokutwa hapo anarudi, std 4 mwezi november tu hapo anarudi muendelee kucheza nae.

Na hizo siku anazokua shule anakua na muda mrefu sana wa kupumzika, huwa wanasoma kwa muda mfupi na kuna wiki 1 au 2 za mwisho kukingana na utaratibu wa shule husika huwa nao wanafunga wakapumzike.

Matoto yenu hayana akili ndio maana yanakazaniwa walau yaelewe hata huo mwezi pia. Wakiachwa wanarudi hawana kitu kabisa kichwani. Huko nyumbani hayasomi yanacheza game na kupigwa pipe hovyo.
 
Asante sana mdau kwa kuleta uzi huu. Kweli kabisa hii tabia imeanza shamiri mno kuna shule wao wameamua darasa la 4,6 na 7 jumamosi wawe shule na likizo kisingizio kuwa wanamitihani na garama wameongeza kama ulivyosema hapo juu.

Hawa watoto wanahitaji kupumzika nadhani mh Waziri nivizuri ukatusaidia toa muongozo kwenye hizi shule.

Huu ni uhuni wa kujiongezea mapato tu sababu hata ukifatilia unakuta walimu hawapo wote mara wanapeana zamu kwenda kifupi ni kuzuga tu hizo siku.
Kwa kweli hata mimi utaratibu huu
Kuna kijana wangu mmoja yuko la saba, hivi karibuni nikajulishwa hawatarudi mpaka tareh.23; mi nimeona ni vizuri tu kwa faida yake, kwa sababu muda uliobaki ni mfupi sana kwa mtihani, akija nyumbani atachanganya mafaili au kupoteza ile mudi ya kufanya mtihani.

Mwanajeshi ili ashinde vitani, inabidi abaki kambini apate mafunzo, akirudi kwa mkewe alafu kesho aende vitani atashindwa.

Kwa mtazamo wangu mi naona ni wazo jema; hiyo michango midogo isikuumize, bali unawekeza kwa mwanao. Hutaki, muache awe bogus.​
Sikubaliana kabisa mtoto au mwanafunzi kubaki shuleni wakati wa likizo,la sivyo kusingekuwa na kupumzika
 
Mbona sie tulifaulu tu bila kubakizwa shule na kufundishwa jumamosi na jumapili? Kuna kitu haipo sawa tukubali. Watoto wanahitaji muda wa kusoma na muda wa kupumzika. Hii sio sawa kwa ukuaji wao kimwili na kiakili.
Swali la kwenda shule jumamosi na jumapili sikubali ila jumatatu hadi ijumaa watakua wanafanya nini..?
 
Watoto wako wanafanya nini likizo nyumbani?
Kwanza hauna watoto,wewe ndiyo mtoto unataka ubaki nyumbani kuzurura
Mimi niwe Sina watoto pole sana likizo ni likizo
Nini maana ya likizo
kama hivyo watoe kabisa likizo
Ubongo wa binadamu unahitaji mapumziko na hizi likizo ziliwekwa kwa sababu ya research mbalinbali pamoja na education theories mbalinbali sio kwamba watu walikurupuka tu wakaweka likizo
Hata mfanyakazi anapewa likizo kazini itakuwa mwanafunzi?
Halafu watoto wanabak shule Ikukaririshwa na sii kufundushwa kwa vitendo napinga kabisa Hilo suala
 
Swali la kwenda shule jumamosi na jumapili sikubali ila jumatatu hadi ijumaa watakua wanafanya nini..?
Siku za masomo wafundishwe ila wikiend waachwe wapumzike pia washiriki kazi za nyumbani. Masomo sio shuleni tu hata nyumbani ni sehemu ya kufundishwa uwajibikaji na majukumu mbali mbali
 
Siku za masomo wafundishwe ila wikiend waachwe wapumzike pia washiriki kazi za nyumbani. Masomo sio shuleni tu hata nyumbani ni sehemu ya kufundishwa uwajibikaji na majukumu mbali mbali
Kuna mtu anakuambia jumatatu hadi jumapili za mwezi mzima akae na watoto nyumbani eti wanapumzika huo ni ujinga
 
Back
Top Bottom