DOKEZO Waziri wa Elimu, huu mtindo wa Kubakiza watoto shuleni wakati wa likizo ni Sahihi?

DOKEZO Waziri wa Elimu, huu mtindo wa Kubakiza watoto shuleni wakati wa likizo ni Sahihi?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Wengine wanatoka saa 8.30 mchana wengine saa 9.30 mchana ijumaa wengine wanatoka saa 6.30 mchana wengine wanatoka 9.30 wengine wanafunga likizo wengine hawafungi yaana mambo hayaeleweki kila wilaya au mkoa na wanavyo jisikia
Kabisa. Imekuwa elimu inaendeshwa kwa matakwa ya msimamizi wa shule.
 
Sema kusoma mwaka mzima bila kupumzika naona haijakaa sawa kwa upande wangu.wiki nne ni chache kwa nini watoto wasikae na wazazi wao?
Sasa nimesikia hii ni kali ni hivi kidato cha kwanza hadi cha nne ngoma hailali na ni full msosi kila kitu wanapata hapo,watawaachia wiki moja ya mwisho
 
Wazazi wanaorud usiku nyumbani hawapendi watoto wawepo nyumban kuangalia singeli zenye chura na mitetemo ya matako kwenye tv,ni hatar Kwa makuzi
Watoto wao halafu hawapendi wawepo nyumbani?
 
Sema kusoma mwaka mzima bila kupumzika naona haijakaa sawa kwa upande wangu.wiki nne ni chache kwa nini watoto wasikae na wazazi wao?
Sasa nimesikia hii ni kali ni hivi kidato cha kwanza hadi cha nne ngoma hailali na ni full msosi kila kitu wanapata hapo,watawaachia wiki moja ya mwisho
Ni kweli,ni muhimu watoto kurudi kwa ajili ya mapumziko nyumbani kwao
 
Mkuu hata huko changamoto za michango hazivumiliki,nchi hii hakuna kwenye afadhali,ni kukomaa tu
Ni kweli kabisa hata shule za Serikali ni pasua kichwa, michango kila siku
Shida nyingine mtoto hana muda wa kupumzika
Mfano kitoto cha kike miaka 12 sawa kinatoka nyumban saa kumi asubuhi na giza yaani kinapita barabarani peke yake mpaka kituo cha daladala
Arafu kinarudi saa moja usiku. Zaid mvua ikiwa inanyesha na. Mafuriko kwa hapa arusha plus tope,
Na jumamosi vile kiende shule na michango wa alfu na mia tano
Eti kinaenda tuition??!! Yan huna muda wa kufundisha tabia au kumsoma mwanao tabia
Yote kwa yote ni hofu ya kufanyiwa vitendo ovu usiku wakati wa kwenda shule
Nimeandika mwandiko wa hasira mtani same he
 
Kingine watu Bado hawajashituka kwa vile mtaala mpya unataka elimu ya msingi iwe mwisho darasa la sita Sasa wakwapua pesa kwa kisingizio Cha kufaulisha, wanahonga pesa na kuweka watu washawishi elimu ya awali au chekechea iwe ya lazima wakati hao watoto wa chekechea watakuwa wadogo wanatakiwa kusoma mazingira ya nyumbani huku wakiwa chini ya uangalizi maana wengine wanavaa Bado diaper, Sasa hawa wa kuchukua watoto usiku na kuwarudisha usiku baada ya kuwa overdose masomo na kuteka muda wa watoto wa kupumzika sisi tumekaa kimya Sasa hao wakifanikiwa kuweka elimu ya awali kuwa ya lazima, sijui wazazi watalia kiasi gani.
 
Du!taabu kweli
 
Hapo kwenye elimu ya awali kuwa lazima ndio wanatafuta pa kupigia hela
 
Asante sana mdau kwa kuleta uzi huu. Kweli kabisa hii tabia imeanza shamiri mno kuna shule wao wameamua darasa la 4,6 na 7 jumamosi wawe shule na likizo kisingizio kuwa wanamitihani na garama wameongeza kama ulivyosema hapo juu.

Hawa watoto wanahitaji kupumzika nadhani mh Waziri nivizuri ukatusaidia toa muongozo kwenye hizi shule.

Huu ni uhuni wa kujiongezea mapato tu sababu hata ukifatilia unakuta walimu hawapo wote mara wanapeana zamu kwenda kifupi ni kuzuga tu hizo siku.
Af wanavyowakazania hao madogo utadhani wakimaliza hayo masomo wanaenda kuajiriwa.. kumbe ndo kwaaanza wanaanza safari. Na hicho cheti cha lasaba hata kuwa nacho ni mzigo tu mana hakina kazi kabisa.
 
Af wanavyowakazania hao madogo utadhani wakimaliza hayo masomo wanaenda kuajiriwa.. kumbe ndo kwaaanza wanaanza safari. Na hicho cheti cha lasaba hata kuwa nacho ni mzigo tu mana hakina kazi kabisa.
[emoji2][emoji2],inashangaza sana
 
Serikali irekebishe mtaala kama watoto tunawataka wasome muda mchache, kwa schedule ilivyo kwa elimu yetu kwa mwaka ni ngumu kumaliza topics zote with accuracy kwa muda husika..

Kwa ratba ya vipind 5 kwa wiki, approximately dk 200k unataka mtoto amalize syllabus ya physics au biology form 3??? Apo hatujazungumzia advance..

Sometimes shule zetu na walimu wetu wanatafta namna ya kusaidia watoto wetu kwa mazingira ambayo sio rfk af watu tunalaumu tuu...

Kwa primary naweza kukubaliana na nyie ila kwa o level na advanc ni sawa walimu ni sahihi kuwafundsha watoto mpk likizo unless otherwise tubadilishe mtaala ila kwa mtaala huu wa sasa acha wasome
Unazungumzia uzoefu au utaalam?

Mtaala pamoja na mohtasari ikitekelezwa kama ilivyopangwa, muda unatosha kabisa!

Siku za kusoma ni 194 ambazo zimetokana na masaa ya kufundisha na muda wa mtoto kupumzika. Hili lenu la kuona muda ni mdogo unatokana na ama hamjui kuandaa namna ya kufundisha na kujifunza ama mnajipa kazi ambazo zinawachosha na hazileti ufanisi na maarifa kwa mtoto.
 
Mitaala na ratiba za muhula wote ziko wazi. Ila uvivu wa walimu wanatumia kipindi cha likizo na weekend kutafuta kipato haramu.
Pia linalosikitisha zaidi ni kwamba madarasa ya mtihani kuwekwa busy maana yake tanzania tunasomea mtihani tu
Ni kweli, hapo ni kusomea mtihani tu,sijui kama watoto wanaelewa hata kinachofundishwa
 
Kwani mtoto wako akibaki nyumbani anafukuzwa shule?
Mpeleke shule za serikali ambazo hawabaki.
  • Hata shule za serikali wanabaki ndg! Huu ujinga ulianzia shule binafsi, ukaachwa na sasa umefika mpaka shule za serikali.
  • Ni moja ya mambo yanayoongeza gharama za maisha.
  • Watu wanaotetea haki za watoto hawasikiki ktk hili.
  • Watoto hawajui kazi ndogondogo kama kupika maandazi kibiashara, n.k Kwa kuwa muda wote - usiku na mchana - 'WANATAFUTA THAMANI YA X'; mbaya zaidi haiwasaidii kupambana na maisha.
  • Waziri wa Elimu atakwa via ni jukumu la TAMISEMI; usishangae TAMISEMI wakakwambia ni hiari kutoa ama kutotoa. Mambo ya kitaifa yanafanywa kiholela.
  • Wabunge wapo tayari hata kurusha ngumi kutetea huu utaratibu kwa kuwa wanamiliki shule au watetea shule za washkaji zao.
  • Huko duniani msisitizo upo kwenye ubunifu, huku kipaumbele ni kufaulu
Ni wakati wa kubadili mfumo wa elimu, ikiwezekana siku za kwenda shule ziwe nne badala ya tano kwa wiki.

Ijumaa iwe ni siku ya michezo tu, pia masomo yawe kwa njia ya vitendo zaidi badala ya rote learning ambayo inadumaza watoto.
Naunga mkono hoja 💯💯.
Kwa sasa ubunifu kwa watoto umepotea kabisa!
 
Huu ulimwengu wa kibepari huu, usipopambana na vijana wako, watakuja kuwa wafungua mageti kwa watu.
Kumuacha shule ndo kumpambania.hapo unapambania watoto wa walimu sio wakwako.Nenda hapo shuleni kwao utakuta wamebaki walimu wawili wengine wako makwao kufanya mambo yao.watoto nikupiga makelele nakupewa na maasignment yasiyona kichwa wala miguu.
 
Haki ya Mungu tena,shida ya watanzania ni kupenda ujinga na kulalamika lalamika.
Yaani wanasiasa wapange maisha mazuri ya mwanao?
Ina maana uelewi kazi ya serikali?.Au mzazi mmoja mmoja atawezaje kubadilisha jambo linalofanywa kwenye jamii ya wengi.Walioweka serikali hawakua wajinga.
 
Back
Top Bottom