Waziri wa Elimu kama kazi imemshinda ajiuzulu, walimu shule binafsi wanalipwa mishahara finyu na hasemi chochote

Umewahi kutoa malalamiko yako sehemu inayostahili ndugu??
 
Hata hizo laki 2 wanakulipa nyingi sn, wewe unatakiwa upewe chumba na kitanda hapo shuleni basi
 
Hiyo kazi mmeshikiwa bunduki kufanya? Si njaa zako ndo zinakuweka hapo?
 
Huko private si ndo mlikuwa mnalipwa mishahara minono, nini kimetokea?
 
Wakiona walimu wamekataa watalegeza masharti, tatizo vijana mnajirahisi mno mpaka mnadharaulika.
Unalijua soko huria.

Ondoka Tarime, njoo Dar ujionee.

Watu wanakaa miezi 4 hawajalipwa mishahara na hawana nguvu ya kuacha kazi🤣
 
Sheria ya kazi imeshaweka minimum wage ni Tsh 270,000 kama kuna mtu analipwa chini ya hapo, ananyonywa. TAESA wanaolipa Tsh 150,000 wajitathmini.
 
Kima cha chini cha mshahara ni shilingi ngapi...?
 
Umewahi kutoa malalamiko yako sehemu inayostahili ndugu??
Kabla hujamlaumu hizo shule binafsi kwanza fuatilia kima cha chini cha mshahara wa sekta binafsi kilichowekwa na serikali yenyewe miaka 8 iliyopita.

Ukishakijua ndio ujiulize hizo shule kuna taratibu zozote wanakiuka ?

Kwa taarifa yako serikali mpaka leo inamlipa mwalimu wa primary Tsh 344,000 Gross! kwa mwezi.

Kuna mashirika ya serikali ambayo wanalipa watu wao mpaka Tsh 170,000.

Mimi nimewahi kufanya kazi kama Mwalimu kwenye shule za jumuiya ya wazazi, CCM walikuwa wananilipa Tsh 130,000 hapo sipewi NSSF wala bima.

Sasa jiulize kama wao wenyewe wako hivyo, hiyo nguvu ya kukutetea wewe ulioko sekta binafsi wataitoa wapi ???
 
Kuwa mwalimu ni wito, vumilieni tu hata wabunge mishahara yao haitoshi...jana walianza kulalamika🐒🤸🤣
 
Sheria ya kazi imeshaweka minimum wage ni Tsh 270,000 kama kuna mtu analipwa chini ya hapo, ananyonywa. TAESA wanaolipa Tsh 150,000 wajitathmini.
Re-visit your sources. Kima cha chini cha mshahara wa sekta binafsi kwa mujibu wa serikali hakizidi Tsh 150,000.
 
Mnalazamishwa kwenda huko ,halafu huwa mnatucheka tunaotengeneza mtaji kitaa kumbe ni watumwa tu. Waziri usiwasikie hao.
 
kumbe unajuwa chakufanya? halafu unakuja kuharisha hapa halafu unatembea bila kunawa unanuka nzi wanakufuata , unapoenda kuomba kazi kuna makubaliano kabla huajaanza kazi hapo ndiyo utaambbiwa utalipwa kiasoi gani utakubali au kukataa sasa unakubali mshahara mdogo ili uje utusumbue huku jukwaani pumbavu wewe kwanza njaa itakuuwa na unaonyesha ni kiasigani ulivyo mjinga kuja kuandika ujinga humu
 
Ungeweka na mfano wa shule ingekuwa vema.

Hivi vyama vya wafanyakazi ndio vyakulaumiwa, vimekaa kimya wakati wanachama wake wananyanyasika.

Waziri unamlaumu bure.
Ama kweli Jukwaa limevamiwa. Yaani huyu hajui kama kuna Wizara inashughulika na kazi na masuala ya watumishi? Kazi ya Vyama vya wafanyakazi ni nini?

Mhe Rais wakati wa Mei Mosi aliwataka wafanyakazi kwenye sekta binafsi kutoa taarifa kwa mamlaka husika kama wana changamoto zozote ili hatua stahiki zichukuliwe. Kwa nini hawataki kupeleka malalamiko yao kwenye wizara inayohusika na kazi?
 
Mkuu hiyo ni lapse of the tongue tu. Mi nimesoma english medium wala hunikamati kwa kingereza. Mind your own bussiness
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…