Waziri wa elimu lingalie hili la walimu hasa wa Primary kutoza pesa kila siku eti ni mitihani

Waziri wa elimu lingalie hili la walimu hasa wa Primary kutoza pesa kila siku eti ni mitihani

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
44,629
Reaction score
83,056
Sasa ni kawaida. Kila siku watoto wanakuja wanadai hela eti kuna mtihani. Kila siku kuna mtihani. Enough is enough.
 
Dawa ni kwenda shule tu na kuwahoji
Majizi yanaongezeka kila siku
 
Uko sahihi. Kuna shule inaitwa Sinon Primary ma Secondary inamichango ya kutosha. Mtihani kila wiki sh 2000 kwa nini? Nilipiga hesabu kidogo tu ya wanafunzi 800 mara 2000 mara 4 kwa maana ya mwezi mmoja. Wanakula hela balaa
 
Serikali ingerudisha tu ada .Kwa sababu huko shuleni kumekuwa na michango mingi ambayo si rahisi hata kutrace mapato na matumizi yake.Wazazi wamekua wakiitwa shuleni kila wakati na kuambiwa wachangie hiki au kile na kwenye vikao hivyo hakuna mzazi ambaye anaweza kupinga kwa sababu ukipinga mtoto wako anayesoma hapo ataandamwa sana na walimu.
 
Sasa ni kawaida. Kila siku watoto wanakuja wanadai hela eti kuna mtihani. Kila siku kuna mtihani. Enough is enough.
Hakika mbuzi wa maskini hazai. Na kama unadhani elimu ni gharama, embu jaribu ujinga tuone.

Elimu bila malipo imekupumbaza, na sasa umekuwa huna msaada kwa badae ya mwanao. Useless kabisa.

Ukiwa kama mzazi unayejitambua, shirikiana na wazazi wenzio na bodi ya shule anaposoma mwanao, kisha ipangilieni vizuri hiyo michango ili watoto wenu wafanye mitihani yenye tija ili kuinua taaluma yao.

Muache kulialia
 
Uko sahihi. Kuna shule inaitwa Sinon Primary ma Secondary inamichango ya kutosha. Mtihani kila wiki sh 2000 kwa nini? Nilipiga hesabu kidogo tu ya wanafunzi 800 mara 2000 mara 4 kwa maana ya mwezi mmoja. Wanakula hela balaa
Wakale wapi?kila mtu anakula ofisini kwake

Wewe mwenywe hapo ofisini kwako hupigi wajingawajinga[emoji1787][emoji1787][emoji1787]???
 
Back
Top Bottom