Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba awataka Watanzania kuacha tabia ya kuhifadhi fedha nyumbani

Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba awataka Watanzania kuacha tabia ya kuhifadhi fedha nyumbani

Ukawii kusikia bank imekuwa mufilisi na vi amana vyenyewe kwishinei.................
 
Amini nakwambia kutunza chini ya mto kwenye hii nchi ya Watawala Walamba Asali ni Salama kuliko huko kwenye Mabenki kwenye Matozo na Makato kila Kona.... Unless Jamaa ana-Tanzania yake kwenye Jamuhuri ya Kichwa chake...
 
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amewataka Watanzania kutumia benki kuhifadhi fedha zao ili kuhakikisha usalama wa fedha zao na usalama wao na kuacha tabia ya kuhifadhi fedha nyumbani.

Dkt. Nchemba aliyasema hayo Jijini Dodoma wakati akizindua Tawi la Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ) kwa niaba ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye alitarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo na kushindwa kutokana na majukumu mengine ya Kitaifa.

Dkt. Nchemba alisema ni vema Wananchi wakajenga utamaduni wa kutumia benki kwa kuwa uendeshaji wa uchumi wa kisasa unategemea zaidi matuminzi ya utaratibu wa kibenki ambao kwa sasa umerahisishwa na unapatikana kwa urahisi.

“Utaratibu wa kuchimbia fedha ni utaratibu wa kizamani, benki sasa zipo kiganjani kwanini uchimbie fedha? Popote ulipo unawezakupata huduma za benki,” alisisitiza Nchemba.
Dkt. Nchemba alisema Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha itaendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na benki zote hapa nchini kama utekelezaji wa sera jumuishi za masuala ya kifedha na kiuchumi zinazolenga kuwasogezea wananchi huduma karibu hasa hizi za kifedha.

‘’Naomba kutumia fursa hii kuwaomba wafanyabiashara, watumishi wa umma na binafsi, viongozi wa Serikali wa ngazi mbalimbali na wananchi kwa ujumla kuiunga mkono na kuitumia Benki ya PBZ katika shughuli zetu za kiuchumi, kwani benki hii imekuwa ikitoa huduma zake kwa uaminifu mkubwa na kwa riba nafuu.’’

Akitoa salamu za Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango, Zanznibar, Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Ali Suleiman Amir alisema Serikali imeamua kuhakikisha huduma za fedha zinawafikia wananchi wote kwa urahisi.

Aliipongeza Benki hiyo kwa kuendelea kutimiza azma ya Serikali kwa kufungua matawi yao katika maeneo mbalimbali nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Benki ya Mtendaji wa PBZ, Dkt. Muhsin Salim Masoud, alisema kuwa Benki hiyo ina vituo vya kutolea huduma takribani 45 ambapo vituo 34 vipo Zanzibar na vituo 11 vikiwa Tanzania Bara huku akiahidi kuongeza vituo vya kutolea huduma ili kuwafikia watanzania wengi zaidi.

‘’Katika mpango kazi wetu, mwakani tutafungua kituo katika mikoa ya Morogoro, Mbeya, Mwanza, Arusha na Tanga ili kuwafikia Watanzania wengi na kuwapatia huduma za kifedha kwa gharama nafuu sana," alibainisha Dkt. Masoud.

Aliongeza kuwa Benki hiyo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa ikiwa ni pamoja na kupata tuzo ya mlipaji kodi bora Zanzibar iliyotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kuongezeka kwa faida, kufuatia juhudi mbalimbali zilizofanywa kuhakikisha wateja wanapata huduma kwa weledi.

‘’Mafaniko ya Benki hii yametokana na Sera nzuri za Fedha hapa Nchini, Sera nzuri za Benki ya PBZ, mahusiano mazuri ya wateja, huduma zenye gharama nafuu na juhudi za wafanyakazi wa Benki yetu," alisema Dkt. Masoud.

Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) ni Taasisi ya kifedha inayomilikiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa asilimia mia moja. Benki hiyo ilianzishwa mwaka 1966 kwa lengo la kutoa huduma za kifedha kwa wananchi ambapo kwa sasa inamtaji wa takribani bilioni 150.

Kabla ya kuwashauri wananchi kuwa wasiweke fedha zao kwenye vibubu nyumbani wapeleke benki, Mwigulu ulitakiwa ufanya utafikti na kujua sababu zinazowafanya watu wasiweke fedha zao benki!
Moja ya sababu inayofanya Watu waweke fedha zao nyumbani ni benki kutotunza siri za miamala ya wateja wao [non confidentiality of customers information}. benki zinatakiwa zitunze siri za wateja wao kuhusu miamala yao lakini si hivyo tena siku hizi!! TRA wanaweza kwenda benki na kufungua account za wateja wanavyotaka wao. Si hivyo tu wafanyakazi wa benki wanatoa taarifa za account za wateja kwa matapeli wa Simu na majambazi!!

Sababu ya pili inayowafanya Watu waweke Fedha zao nyumbani ni utitili wa bank charges amabzo ni unjustified. It does not make sense kumtoza mteja kwa kutoa fedha zake! BOT wanatakiwa wachunguze bank charges za haya mabenki na kuona kama kweli wanastahili kuwatoza wateja wao. Mfano mzuri anagalia statement ya CRDB bank ya mwezi mmoja uone kiasi gani kinakusanywa toka kwa mteja kwa mwezi mmoja kama bank charges!!

Haya mambo yote yako chini ya uwezo wa wizara ya Fedha kuyarekebisha lakini kwa kuwa Serikali ina kipaumbele cha kukusanya TOZO tu bila kujua athari zake kwa jamii ndio maana tumefika hapo tulipofika.
 
Kabla ya kuwashauri wananchi kuwa wasiweke fedha zao kwenye vibubu nyumbani wapeleke benki, Mwigulu ulitakiwa ufanya utafikti na kujua sababu zinazowafanya watu wasiweke fedha zao benki!
Moja ya sababu inayofanya Watu waweke fedha zao nyumbani ni benki kutotunza siri za miamala ya wateja wao [non confidentiality of customers information}. benki zinatakiwa zitunze siri za wateja wao kuhusu miamala yao lakini si hivyo tena siku hizi!! TRA wanaweza kwenda benki na kufungua account za wateja wanavyotaka wao. Si hivyo tu wafanyakazi wa benki wanatoa taarifa za account za wateja kwa matapeli wa Simu na majambazi!!

Sababu ya pili inayowafanya Watu waweke Fedha zao nyumbani ni utitili wa bank charges amabzo ni unjustified. It does not make sense kumtoza mteja kwa kutoa fedha zake! BOT wanatakiwa wachunguze bank charges za haya mabenki na kuona kama kweli wanastahili kuwatoza wateja wao. Mfano mzuri anagalia statement ya CRDB bank ya mwezi mmoja uone kiasi gani kinakusanywa toka kwa mteja kwa mwezi mmoja kama bank charges!!

Haya mambo yote yako chini ya uwezo wa wizara ya Fedha kuyarekebisha lakini kwa kuwa Serikali ina kipaumbele cha kukusnya TOZO tu bila kujua athahari zake kwa jami ndio maana tumefika hapo tuipofika.
Watawalafa ni wanafiki sana wao wanaanglali tu ma VAT waliyoyawka ndani il saa100 amepate hela za kuzurura uaesbun na kununua magoli ya yanga
 
Amini nakwambia kutunza chini ya mto kwenye hii nchi ya Watawala Walamba Asali ni Salama kuliko huko kwenye Mabenki kwenye Matozo na Makato kila Kona.... Unless Jamaa ana-Tanzania yake kwenye Jamuhuri ya Kichwa chake...
Mabenk ya matozo sojui ma VAT mengi mmno unaweza kushanga ukafanya transaction 100 ukawa umewapa bank na serikila kama 100000 hivi za bure
 
Hiyo tabia haitakoma kutokana na utaratibu wa sheria za hovyo tulizonazi sasa.

Mfano mamlaka ya kuzuia akaunti za wateja katika benki amepewa kamishna mkuu wa TRA lakini unakuta zinatekelezwa hadi na maafisa wa kawaida.

Kwanza hii sheria ingeangaliwa upya na kuwa na namna ngumu ya kuitekeleza ikiwa ni pamoja kamishna mwenyewe kutoa agizo hili sio kwa kukaimisha mtu. Hii itasaidia hawa maafisa njaa kuacha kuwaonea wafanyabiashara.
 
Pesa zikiwepo benki hasa zikiwa nyingi TRA wanazitaka kwa udi na uvumba.
 
Back
Top Bottom