Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
NCHI INAYOENDELEA LAZIMA IKOPE
"Duniani kote nchi zinazotekelea miradi mikubwa ya maendeleo na zenye uchumi mkubwa, zina madeni makubwa, ipo hivyo nendeni mkaangalie
Huwezi linganisha uchumi wa Tanzania na Marekani,” - Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba
Kuna nchi masikini hazina madeni na hazikopesheki, watu wajue kadiri unavyotekeleza miradi mikubwa ndivyo deni lako linavyokuwa, hivyo ni uchaguzi wako tu
Mfano Tanzania kabla ya kuunganisha barabara zote deni lilikuwa chini ya Bilioni 10 tu
Leo hii tunafurahia 4G na 5G lakini mkongo wentu wa taifa tumetengeneza deni. Miradi ya aina hiyo ni mingi
Watanzania wajue deni la taifa ni tofauti na fedha za kwenye ATM, deni ni mikataba inayosainiwa na fedha zitaingia kulingana na mikataba
Kuna madeni tumemalizia kulipa ya Awamu ya Kwanza, nimesaini kulipa deni ambalo lilikopwa sijazaliwa, yapo madeni ya Awamu ya 2, 3, 4 na 5 na tunakopa sasa yataipwa baadaye
Anayekopa siyo Rais, inakopeshwa Serikali na hakukopeshwi kwa awamu
Mikopo ya muda mrefu ndio inayotakiwa ina masharti nafuu kuliko ya muda mfupi, mfano mkopo wa Bwawa la Mwalimu ilishasainiwa, mradi unaendelea na tunaendelea kupokea fedha zake
Mikopo ya SGR tunaendelea kuipokea fedha
Fedha ya mkopo haitoki siku moja, zinapoendelea kuingia ndivyo deni linavyokua
Tumepata mkopo wa UVIKO19 ambao hauna riba, huwezi kuuacha kwa kuwa watangulizi walishakopa na deni limeshakuwa kubwa, pia huwezi kuacha kukopa kuogopa deni
Niwahakikishie hakuna mkopo unaolipwa kwa matumizi ya kawaida wala kwa matumizi ya mishahara au posho, ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo
Hatuwezi kuachia mradi njiani, deni la Serikali uwiano wake na pato la taifa tupo 31%, ukomo ni 55%
Deni la nje kwa uwiano wa pato la taifa tupo 18% ukomo wake ni 40%, deni la nje kwa mauziano ya nje 142% ukomo wake ni 180%
Rais anapotafuta mikopo anazingatia ile ya masharti nafuu na inayoenda katika miradi muhimu