TANZIA Waziri wa Fedha, Dkt. Willliam Mgimwa afariki dunia!

TANZIA Waziri wa Fedha, Dkt. Willliam Mgimwa afariki dunia!

Sijakupata, mhe. Dr Mgimwa hakuwa na nafasi ya nini? Pole kwa msiba wa mh. Dr Mgimwa

Kulikuwa hakuna namna nyingine,

Kila mmoja alijaribu kwa namna aliyoweza,

Lakini haikuwezekana.

Wengine walikesha wakikuombea,

Wengine walishinda karibu na kitanda chako wakikuhudumia

Na wengine walitumia kila ujuzi waliokua nao kukuepusha na mauti,

Wala haikusaidia.

Aliyekupa pumzi alikwisha kufanya maamuzi,

Hakutaka uondoke bila kuifahamu sura ya mwaka mpya aliouandaa,

Sijui,

pengine ulikuwa mwema sana,

Ama kuna jambo alitaka kulitimiza,

Nani nayejua?

Umelitumikia taifa kwa kadri ulivyoweza,

Na mwenyezi Mungu atatenda kwako ka kadri ya matendo yako,

KWA KHERI MBUNGE WA KALENGA..

KWA KHERI WAZIRI WETU WA FEDHA..

TULIKUPENDA SANA
 
Poleni wafiwa.Pole Amina.Pole baba Ritz.Poleni Gambaz!
 
Marehem wilium Mgimwa ni daktari (PhD), amefanya kazi kama mbunge kisha waziri wa fadha, Ni Mnyalukolo mwili wake utasafirishwa na serikali kurudi home (unyaluni???). KUMBUKUMBU: Marehemu Balali pia ni daktari (PhD), alifanya kazi umoja wa mataifa kisha wizara ya fedha kama gavana, ni mnyalukolo, mwili wake haukurudi. hii serikali ina double standard eee!!!!:drama:

Nimekusoma sawiya!.....
 
Rose mayemba,
naelewa sasa ni mapema mno na maombi na faraja kwa familia ni muhimu

naomba kujua hali ya kisiasa ya chadema kalenga nilifanya research yangu ndogo niliyoifanya ktk uchaguzi uliopita
mgombea wa chadema anaitwa REHEMA hakufanya vizuri kwy jimbo hili najua hali na mazingira yamebadilika ukilinganisha na 2010 naomba kujua mtazamo wako juu ya cdm kuweza kuibuka kidedea.
 
Poleni sana, mungu amempenda zaidi tumuombee ndio kubwa zaidi lililopo mbele yetu.
 
Rose mayemba,
naelewa sasa ni mapema mno na maombi na faraja kwa familia ni muhimu

naomba kujua hali ya kisiasa ya chadema kalenga nilifanya research yangu ndogo niliyoifanya ktk uchaguzi uliopita
mgombea wa chadema anaitwa REHEMA hakufanya vizuri kwy jimbo hili najua hali na mazingira yamebadilika ukilinganisha na 2010 naomba kujua mtazamo wako juu ya cdm kuweza kuibuka kidedea.

Ni mapema mno kujadili hali ya kisiasa jimbo la kalenga kamanda, tumwache kwwanza kwenzetu apumzike kwa amani
 
Mungu atusaidie kuzihesabu siku zetu maana hatujui siku wala saa ya kuondoka kwetu duniani. R.I.P Mzee wetu
 
Natoa pole za dhati kwa familia ya Dr. Msigwa, Mungu awajalie faraja wakati huu mgumu wa pigo kubwa kwa familia yao. Natoa pia pole kwa ndugu jamaa, marafiki na wale wote ambao wameumizwa na msiba huu Mungu kwenye faraja awaponye na kuwasimamia wakati huu wa majonzi. Raha ya Milele Umpe Ee Bwana...
 
Back
Top Bottom