TANZIA Waziri wa Fedha, Dkt. Willliam Mgimwa afariki dunia!

TANZIA Waziri wa Fedha, Dkt. Willliam Mgimwa afariki dunia!

poleni wafiwa ila taadhari hatutaki maziahi kama ya balali tuna ardhi ya kutosha rudisheni mwili nyumbani RIP MGIMWA
 
Marehem wilium Mgimwa ni daktari (PhD), amefanya kazi kama mbunge kisha waziri wa fadha, Ni Mnyalukolo mwili wake utasafirishwa na serikali kurudi home (unyaluni???). KUMBUKUMBU: Marehemu Balali pia ni daktari (PhD), alifanya kazi umoja wa mataifa kisha wizara ya fedha kama gavana, ni mnyalukolo, mwili wake haukurudi. hii serikali ina double standard eee!!!!:drama:

Wafeeeee woote na Lukuvi waooooo
 
Fumbo la kifo ni gumu sana. Pamoja na wimbo Remy aliimbia kifo bado alichukuliwa. Poleni familia palen watz wenzangu. Pole Africa Waziri wa fedha wizara iliyotulia kwa sasa.
 
Mzee wa mimba kumbuka kwamba sisi sote ni watanzania, kua magamba si kuwaombea wafe. Inatakiwa wawepo wayaone mabadiliko yakitokea.
 
Marehem wilium Mgimwa ni daktari (PhD), amefanya kazi kama mbunge kisha waziri wa fadha, Ni Mnyalukolo mwili wake utasafirishwa na serikali kurudi home (unyaluni???). KUMBUKUMBU: Marehemu Balali pia ni daktari (PhD), alifanya kazi umoja wa mataifa kisha wizara ya fedha kama gavana, ni mnyalukolo, mwili wake haukurudi. hii serikali ina double standard eee!!!!:drama:

Kesho Lukuvi
 
Poleni sana wafiwa.
Marehemu hakukaa muda mrefu toka aukwae uwaziri, ila ki-ufanisi alikuwa kama CCM na serikali yake.
 
Poleni sana.

Hakika Tanzania hususan wale wa fani ya banking wamepoteza mtu mahiri sana. kwani tete alikuwa lulu katika fani hiyo na mzalendo wa kweli.

Yeye ni zao la wengi sana katika fani hiyo. Nilimfahamu miaka ya mwishoni mwa 80,s ambapo tulihudhuria kozi moja nje ya nchi yeye akitokea BOT na mimi wizara ya fedhwa.

Nakumbuka alistahafu BOT akiwa mkuu wa chuo cha BOT pale kapripoint Mwanza.

RIP Mgimwa
 
Kulikuwa hakuna namna nyingine,

Kila mmoja alijaribu kwa namna aliyoweza,

Lakini haikuwezekana.

Wengine walikesha wakikuombea,

Wengine walishinda karibu na kitanda chako wakikuhudumia

Na wengine walitumia kila ujuzi waliokua nao kukuepusha na mauti,

Wala haikusaidia.

Aliyekupa pumzi alikwisha kufanya maamuzi,

Hakutaka uondoke bila kuifahamu sura ya mwaka mpya aliouandaa,

Sijui,

pengine ulikuwa mwema sana,

Ama kuna jambo alitaka kulitimiza,

Nani nayejua?

Umelitumikia taifa kwa kadri ulivyoweza,

Na mwenyezi Mungu atatenda kwako ka kadri ya matendo yako,

KWA KHERI MBUNGE WA KALENGA..

KWA KHERI WAZIRI WETU WA FEDHA..

TULIKUPENDA SANA
 
Back
Top Bottom