Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar, akiwasilisha Mapendekezo ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2026/27 bungeni leo, ametangaza mabadiliko makubwa katika utoaji wa huduma za Mamlaka ya Usajili na Utambuzi wa Watu (NIDA), ikiwemo kuanza kutoza ada kwa wananchi na taasisi zinazohitaji kupata taarifa kutoka kwenye kanzidata (database) ya mamlaka hiyo.
Balozi Khamis amebainisha kuwa uamuzi huo umekuja baada ya kubainika kuwa na mahitaji makubwa na ya mara kwa mara ya taarifa hizo, jambo ambalo limekuwa likisababisha gharama kubwa za uendeshaji kwa upande wa serikali.
Kupitia mabadiliko hayo ya Kanuni za Sheria ya Usajili na Utambuzi wa Watu ya Mwaka 2014, wananchi watakaohitaji nakala ya taarifa zao sasa watatakiwa kulipia kiasi cha shilingi 1,000, huku taasisi zote zinazotumia mifumo ya NIDA kuhakiki taarifa nazo zikitakiwa kulipia ada maalum.