Waziri wa Fedha na Mipango ateuliwe Profesa Musa Assad

Waziri wa Fedha na Mipango ateuliwe Profesa Musa Assad

Ikimpendeza Mheshimiwa Rais, anaweza kumteua Prof. Assad kuwa Mbunge na kisha kuteuliwa Waziri wa Fedha na Mipango.

Sina shaka na utendaji wake hasa akiwa CAG, alisimama imara hali iliyompelekea kukumbwa na mizengwe ya wachumia tumbo.

Umri hauwezi kuwa kikwazo sababu tuna Mawaziri wengi wenye umri mkubwa zaidi yake.
Hiyo ni sawa sawa na kufikiria kuwa Lissu anaweza kuwa Rais wa Tanzania kisha amteue Shogake Amsterdam kuwa Vice President!
 
Unaijua Definition ya Utumishi kwa muktadha uliotumika?

Mtumishi wa Umma kwa mujibu wa Katiba ana sifa zake
Mf.Mbunge si mtumishi wa Umma japo anakula Mshahara so unapaswa kujiuliza Waziri ni mtumishi wa Umma?

Kiongozi wa Watumishi wa Umma kwa mujibu wa Katiba ni Katibu Mkuu Kiongozi, jee Mawaziri wapo chini ya Chief Secretary? Anzia hapo kwanza …
Sijui ni katiba gani umesoma (labda kuna toleo jipya) lakini mawaziri baada ya kula kiapo cha uwaziri, hula kiapo cha kufuata maadili ya utumishi wa umma mbele ya kamishna wa maadili, kiapo hicho ni kwa mujibu wa kanuni za utumishi wa umma za 2003.
Back to the point, lengo la framers kuzuia cag kuwa appointed kwa nafasi yeyote ila mara na baada ya kushika wadhifa huo ni kumfanya cag awe huru katika kazi yake bila uwoga wala upendeleo, (fear or favour)
Imagine cag anayewaza uteuzi atafanya kazi kuwafurahisha wanaoteua, au atafunika baadhi ya mapungufu kuhofia kuwauzi wateuzi in future.
 
Back
Top Bottom