Waziri wa Fedha & Uchumi wa Hamas (Abd al-Fattah al-Zari) Afariki kwa Shambulio la Ndege

Kwa mtaji huo, hamas ni wapuuzi maana kama wangalikuwa na akili, wangewaachia Mateka wote haraka ili Israel wakose sababu ya kuwatwanga
Hamas linatajwa Kwa vifo tu. Sijui wameishia pumzi?
 
Kojoa urudi kulala. Hamas wenyewe wanakiri kuuliwa kwa vigogo wake, we nani upinge? Hayp mazishi wanazikwa watu gani? Punguza mahaba.
 
Tokea mwanzo Netanyahu alikua anazungumzia kuvamia Gaza na kuivunja Hamas. Kukuomboa mateka haikuwa hoja yake, hii kaanza kuigusia baada ya maandamano nchini kwake kutaka hao mateka warejeshwe.
 
Kuua viongozi wa HAMAS hakutamaliza huo mgogoro bali wanaendeleza uchuki itayoendeleza vita.
Wanaweza wakamaliza kwa kuwa huu uhasama ume escalate na kuanzia Hamas walipochukua uongozi wa Mji Gaza mwaka 2006 kutoka kwa Fatah.

West Bank ambayo iko chini ya Fatah itikadi yake siyo kali kama ya Hamas. Maana hawa Hamas waliposhinda tu wakatangaza kuwa hawaitambui nchi inayoitwa Israel.

Ndiyo maana hata Mwenyekiti wa PLO Mahmoud Abbas anayeishi Ramalah West Bank yalipo makao makuu ya Mamlaka ya Palestine hajatia neno toka mauaji ya October 7, 2023
 
Inaitwaje hiyo novel
 
Abu Jihad Kamanda wa Fatah, aliuliwa mwaka 1988 kwa kupigwa risasi na kachero wa MOSSAD Nahum Lev akiwa nyumbani kwake Tunisia.
 
Kimsingi hata Ayatollah Khamenei yupo kwenye radar, wanamcheki tu
Ayatollah wala hawatomgusa, wanamkatia tu matawi kama walivyofanya kwa mzee baba!!!(magu)

Mwisho wa siku utasikia Ayatollah kaondoka kwa presha
 
naona wale vigogo wa Hamas wanaliwa vichwa mmoja baada ya mwingine.
Israel wanajua kumaliza tatizo ni kupambana na viongozi wakiisha hawa wako kuwadhibiti ni rahisi sana bila kumua kiongozi haujafanya lolote
 
Kwa mtaji huo, hamas ni wapuuzi maana kama wangalikuwa na akili, wangewaachia Mateka wote haraka ili Israel wakose sababu ya kuwatwanga
Kwa akili zao hao jamaa unafikiri mateka watakua bado hai?
 
R.I.P Joshua mdogo wangu. Netanyahu anakulipia uliyotendewa huku
 
Wanaweza wakamaliza kwa kuwa huu uhasama ume escalate na kuanzia Hamas walipochukua uongozi wa Mji Gaza mwaka 2006 kutoka kwa Fatah.
Uchaguzi ulifanyika, msimamizi wa nje alikuwa Jimmy Carter , Rais wa Marekani. Jimmy amesema na ameandika akisisitiza kwamba Hamas walishinda uchaguzi kwa kura na kwa uhalali. Nenyanyahu alipenda ushindi wa Hamas ili kupata ''divide and rule' Wapalestina wasiungane, alifanikiwa kwa muda bila kujua alikuwa 'anafuga jini''. Kwa miaka yote takribani miaka 18 pesa za kuendesha Gaza zilitoka Israel na liyeidhinisha ni Bibi
Ndiyo maana hata Mwenyekiti wa PLO Mahmoud Abbas anayeishi Ramalah West Bank yalipo makao makuu ya Mamlaka ya Palestine hajatia neno toka mauaji ya October 7, 2023
Sijui kauli ipi unayosema. Rais Biden alipanga kukutana na mfalme Abdullah na Mahmoud Abbas.
Mkutano huo haukufanyika kwasababu Israel ilishambulia Hospitali na kuua watu na Abbas akarudi.
Abbas alikumbana na upinzania mkali sana West Bank wakimtaka ajiuzulu.
Hata sasa hivi hali yake ni mbaya sana, kwamba, Hamas ni maarufu kuliko Fatah na Abbas.
 
Sitachoka kuwasaidia vijana wetu wa Tanzania wasio na uwezo wa kusoma au kutafuta habari

Nenda kasome resolution UN 181 halafu endelea na resolution nyingine hadi mwezi huu.
Unajua nani anazuia! Ni USA, UK, France na nchi washirika.
Kusimamisha vita ya Gaza kuna resolution zaidi ya 3 na zote zimekuwa 'vetoed' na USA

Mgogoro wa Palestina uliungwa mkono na NAM wakati huo zikiongozwa na akina Nyerere

Kuua raia wa nchi nyingine katika nchi nyingine ni ugaidi. Israel ikifanya hivyo si ugaidi.

Kupiga ubalozi wa nchi nyingine kwa mujibu wa Geneva convention ni kosa, akifanya Israel si kosa

Kuna unafiki na hapa watu wengi hawaelewi kwasababu hawana ufahamu.

JokaKuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…