Waziri wa Katiba na Sheria Mwigulu Nchemba awajibu TLS kuhusu Rais Samia Suluhu kuteua Baraza jipya la Mawaziri

Yaani wapinzani kulalamika ni jadi yao! Mnadhani kuna kupumua hapa? Magu spirit will prevail
Hili suala haliwahusu Wapinzani bali linahusu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na ndiyo maana Jiwe wakati wa uhai wake alijiimarisha pekee badala ya kuimarisha mifumo. Hii ni kutokana na kugundua kuwa waliomzunguka wengi wao wana mawazo finyu kama ulivyo wewe.
 
Kama ni ww unayeteua sawa!
Tatizo lenu nyie mataga ni kudhani kuamini kuwa kila anayepinga au kukosoa baadhi ya watendaji wa serikali ya ccm basi ni mpinzani na yupo nje ya system.

Mnafanya kosa kubwa sana
Kwa taarifa yenu humu wengine wapo jirani na meza ya wenye maamuzi ya nchi hii.
 
Mbona watu wa sheria mnakanyagana.

Kipi ni kipi??
💔💔💔💔💔💔💔💔💔
 
Mungu atatutea!! Wako wapi akina farao??
 
Ww ndio taga, aliyekuambia ss hatumo kwenye ' inner circle' ni nani? Ona sasa umesababisha nimejilipua mfyuuuuuu!
 
Ww ndio taga, aliyekuambia ss hatumo kwenye ' inner circle' ni nani? Ona sasa umesababisha nimejilipua mfyuuuuuu!
Ndiyo ujue kuwa haupo sehemu hiyo maana hata the principle Ethics za utumishi hujui
 
Mwigulu kama unajua tupo kwenye majonzi mazito, nguvu ya kuperuse mitandaoni kuitafuta ile doc ya TLS, kuisoma na kuijubunkwa hoja mufilisi umezitoa wapi?

Wewe pia upo unawaza mirathi badala ya mazishi na maslahi yako yapo at high stake kuliko hata hao TLS.
 
Bush lawyer ... nashauri Mwigulu aache kwanza wanaojua sheria walumbane mwisho tutapata muafaka. Halafu hii hulka ya kutaka KUWANYAMAZISHA watu utaiacha lini kaka Mwigulu???
 
Kwa hekima na busara kabisa Miwigulu Nchemba pamoja na kuwa wewe ni waziri wa sheria ulitakiwa ukae kimya tu katika hili kwasababu wewe una mgongano wa ki-maslahi katika bandiko la TLS.

Kwasababu Mh. Rais akiamua kulivunja Baraza la Mawaziri na wewe utakuwa muathirika No. 1. Kwahiyo tunakushauri Mwigulu Nchemba kaa kimya katika hili usitake kuwavuruga watu kwenye huu mjadala muhimu.
 
Huyu mama Samia asipoiga udikteta wa jiwe kwa hizi siku mbili tatu watampasua kichwa kwa maushari na makelele kitoka kila kona,hawa TLS walikuwaga wapi kipindi kile Jiwe linaikanyaga Katiba na kufanya neno lake kuwa sheria
Mama umeshaapa katiba yetu inakupa madaraka makubwa Sana!! Mtu asikupangie!! Fanya uonavyo vyema ili maadamu unacheza kwenye mamlaka Yako.
Inavyoelekea watu wanataka kukujaribu!! Mtangulizi wako aliwaambia wazi: "mimi sijaribiwi". Waonyeshe kwa vitendo wanaokujaribu kuwa haujaribiwi!! Mungu yuko pamoja nawe na watanzania walio wengi wako pamoja nawe!! Hawa wachache wanaopiga makelele wala usihangaike nao, wadharau tu! Watachoka na kuacha wenyewe!! Mfano mdogo tu, kwani TLS imeanza leo? mbona ilikuwa kimya mpaka tulishaisahau? Ni kwa sababu mbinu zao za kiharakati zilidharaulika!!
 
Yaani wapinzani kulalamika ni jadi yao! Mnadhani kuna kupumua hapa? Magu spirit will prevail
Magu spirit ipi tena jamaani, si tumekubaliana amekufa??? Au mna mpango wa kumfufua??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…