Waziri wa Katiba na Sheria Mwigulu Nchemba awajibu TLS kuhusu Rais Samia Suluhu kuteua Baraza jipya la Mawaziri

Waziri wa Katiba na Sheria Mwigulu Nchemba awajibu TLS kuhusu Rais Samia Suluhu kuteua Baraza jipya la Mawaziri

Nimesoma andiko la TLS, kwa heshima zote kwa chombo chetu hiki kilichopewa mamlaka kisheria, Nimeshtuka sana, I wish to say,

Kwanza KATIBA HAIJAVUNJWA KWA MHE RAIS SAMIA SULUHU kuapa, na wala hakuna Mkanganyiko wowote wa Kikatiba, kwa yeye kutoteua PM na Baraza jipya. Mmekaa wote kweli mkaona hivyo.

Kwa mujibu wa Katiba Ibara ya 42(5) kuna watu wa aina mbili wanaweza kuwa Rais. Moja, Rais Mteule ambaye anatokana na Ibara ya 42(1). Mbili, Mtu anayeshika kiti cha Rais ambaye anatokana na ibara ya 37(5) na 50(2)(d) ambaye ni Makamu wa Rais. Kwa Mazingira haya, Makamu wa Rais, baada ya kifo cha Rais, anakuwa Kaimu Rais baadae ndio ameapa na kuwa RAIS wa Nchi. Rais Mteule anapatikana kutokana na uchaguzi. Hivyo basi ibara ya 57(2)(f) ya Katiba haitumiki katika mazingira haya. Kwa mjibu wa Sheria, Mhe Rais alitakiwa kutoa taarifa hii kwenye Baraza la Mawaziri baada ya kuapa na alifanya hivyo, maana yake Baraza lipo.

Hata hivyo kwa tamaduni za Kiafrika, kitanzania na Misingi ya UTU, SIONI KAMA NI JAMBO JEMA SANA KUANZA KUJADILI MGAWANYO WA MADARAKA TUNGALI HATA HATUJAMZIKA ALIYEKUWA KIONGOZI WETU. HUU SIO MSIBA MDOGO, JAMBO HILI ZITO LIKO MIKONONI MWA RAIS WETU MAMA SAMIA SULUHU, HALAFU SISI TUANZE KUMPATIA MAMBO YA MARA TEUA PM, MARA VUNJA BARAZA, KATIBA INAELEKEZA RAIS KUAPA NA NAMNA YA KUMPATA MAKAMU WA RAIS.

KWA MJIBU WA KATIBA RAIS ANARUHUSIWA KUVUNJA BARAZA MUDA WOWOTE NA KUPANGA ATAKAVYO HATA SIO KWA MAZINGIRA KUAPA KWAKE,

KWANINI HATUIONI HEKIMA YAKE YA KUSHUGHULIKIA MSIBA KUMSITIRI KWANZA ALIYEKUWA KIONGOZI WETU? TUNAANZA NA MAZISHI AU MIRATHI? 😭😭😭😭

Pia soma > TLS: Kwa Mujibu wa Katiba, sasa Tanzania haina baraza la Mawaziri, Rais Samia atakiwa kuteua Waziri Mkuu ndani ya siku 14
Naunga mkono hoja ya Mhe. Mwigulu Nchemba
P
 
Huu weusi wa Pages za hii Site ya JF ni alama ya maombolezo?
 
Mwigulu Nchemba ! Upo? 😇 Natamani sana utumbuliwe moja kwa moja awamu hii! Sasa sijui kama MAMA yetu atapata huo ujasiri!

Wengine ni PM, yule mwenzako wa afya, Kabudi, Bashungwa (huyu hata kupiga dana dana sijui kama anaweza! Halafu eti ni Waziri wa michezo!), Kibabu George Mkuchika, Doto James, Ole Sabaya, na wengineo wengi!! Nyinyi mlikubuhu kwa unafiki, kujikomba komba na pia kumpotosha Mzee enzi za uhai wake.
DUA LA KUKU
 
Aliyetoa bandiko la TLS ni kilaza mmoja, kama TLS nzima basi wamedhalilisha Taaluma zao.
Wanashindwaje kutofautisha Rais mteule, na Rais kwa sababu za kiafya au kifo.

Kwahiyo huyo Rais kama kweli anaendelea na hilo baraza la awamu ya 5 kwanini yeye anaitwa Rais wa awamu ya 6. Hivi mtu mwenye akili unaweza kujiaminishabkuwa baraza la awamu 5 linaweza kuvushwa kwenye awamu ya 6 bila kufanyika uteuzi. Mbona watu tunapenda kupotosha ili kulinda matumbo badala ya kulinda katiba na sheria. TLS wamefanya kazi nzuri sana na kwa wakati. Sababu hawakujuwa kama AG angeshindwa kumshauri Rais kuhusu kuwa na baraza jipya. Kwanini AG hakumshauri makamo wa Rais kuitisha kikao cha baraza la mawaziri na kuwatangazia kifo cha Rais na hilo baraza likaishia hapo? Jibu AG ameshindwa kutekeleza wajibu wake.
 
Dah! Mwigulu kama anajua tupo kwenye msiba mzito ametoa wapi nguvu ya kuandika haya? Hapa ninachokiona ni namna ya kujipigia debe ili asiachwe kwenye baraza lijalo. Hakuna chochote cha msingi alichokiongea. TLS wametoa mwanga kuhusu issue nzima ya kikatiba kuhusu hali iliyopo, sasa hapa Mwigulu hata haieleweki anaongea nini.
TLS wametoa wapi?
 
Back
Top Bottom