Waziri wa Katiba na Sheria Mwigulu Nchemba awajibu TLS kuhusu Rais Samia Suluhu kuteua Baraza jipya la Mawaziri

Waziri wa Katiba na Sheria Mwigulu Nchemba awajibu TLS kuhusu Rais Samia Suluhu kuteua Baraza jipya la Mawaziri

Nchi haiendeshwi kwa taratibu za kimila. TLS wao wamehadharisha tu muwe makini msikurupuke.
Si mara moja uongozi uliopita umekuwa ukikiuka katiba au anataka iwe mazoea? Mliwahi kuteuwa wabunge wa kiume wengi zaidi ya wanawake. Wanaharakati na wapinzani waliwashitukia na kuteka katiba ifuatwe. Posi alitolewa ubunge na kupewa ubalozi ili kukuwa soo.
Wameteuliwa mawaziri wawili bila kuwapo kwa waziri mkuu kinyume cha katiba. Kwa kuwa hakuna aliyewashitua katiba ilikanyagwa.
Mara ngapi wabunge wasio na chama wamekuwa wakishiriki Bunge kinyume cha katiba? Au unafikiri tunafurahi?
Leo TLS imewahadharisha unang'aka. Tuache kudharauliana.
Mwambie na yeye akienda kuapishiwa kichochoroni badala ya Ikulu. Sasa kwa vile ni mzee wa matamaa anataka kuendelea na upuuzi.
 
Mwigulu Nchemba ! Upo? [emoji56] Natamani sana utumbuliwe moja kwa moja awamu hii! Sasa sijui kama MAMA yetu atapata huo ujasiri!

Wengine ni PM, yule mwenzako wa afya, Kabudi, Bashungwa (huyu hata kupiga dana dana sijui kama anaweza! Halafu eti ni Waziri wa michezo!), Kibabu George Mkuchika, Doto James, Ole Sabaya, na wengineo wengi!! Nyinyi mlikubuhu kwa unafiki, kujikomba komba na pia kumpotosha Mzee enzi za uhai wake.
Utalia na kufa, baada ya saa 9 jioni ya leo. Uliekuwa huwataki mmoja wao ni makamu wa Rais.
 
Mwigulu anapaswa afaham kuwa Rais HAPANGIWI, Tena akipangiwa ndio hafanyi kbs. Kwa voice ya the late JPM
 
Bush lawyer ... nashauri Mwigulu aache kwanza wanaojua sheria walumbane mwisho tutapata muafaka. Halafu hii hulka ya kutaka KUWANYAMAZISHA watu utaiacha lini kaka Mwigulu???
Anajiona yeye ndiye kila kitu hapa Tz. Kumbe sivyo, huyu madelu ana kaujuaji hivi!.
 
Huyu mama Samia asipoiga udikteta wa jiwe kwa hizi siku mbili tatu watampasua kichwa kwa maushari na makelele kitoka kila kona, hawa TLS walikuwaga wapi kipindi kile Jiwe linaikanyaga Katiba na kufanya neno lake kuwa sheria.
Kama hawakusema wakati ule, na sasa wanyamaze! Tuna vilaza kila aina. Wewe wa hovyo kabisa. TLS imejulikana sana katika awamu ya tano. Ikafikia hatua serkali ikataka kutia mkono TLS. Serkali ambayo haikufuata katiba wala sheria ilisemwa sana na TLS. Ulikuwa wapi? Tundu Lissu, Fatuma Karume na sasa Nshala wote ilikuwa miiba!
 
Hakuna excuse yoyote ya kuvunja katiba kwani kuna ugumu gani kuwatambua kama waziri mkuu na mawaziri wa awamu ya tano? Lkn tunaposema raisi samia ameendesha kikao cha baraza la mawaziri na wakati yeye ni raisi wa awamu ya sita na wao ni mawaziri wa awamu ya tano, hatuko saawa
 
Mwigulu Nchemba ! Upo? [emoji56] Natamani sana utumbuliwe moja kwa moja awamu hii! Sasa sijui kama MAMA yetu atapata huo ujasiri!

Wengine ni PM, yule mwenzako wa afya, Kabudi, Bashungwa (huyu hata kupiga dana dana sijui kama anaweza! Halafu eti ni Waziri wa michezo!), Kibabu George Mkuchika, Doto James, Ole Sabaya, na wengineo wengi!! Nyinyi mlikubuhu kwa unafiki, kujikomba komba na pia kumpotosha Mzee enzi za uhai wake.
Hapo kwa PM hapana aisee aendelee tu binafsi namuelewa sana
 
Naona logic ya maombolezo ya siku 21 kuwa siku 14 kuunda serikali, siku 7 kufanya taratibu za maziko . TLS wako sahihi kutoa ushauri was kuvunja Baraza la mawaziri
 
Maza tukishamaliza kuzika kimbiza wote unawaona gozigozi na kupanga safu yako.
Nani anakusanya pesa za mchango ili nimtumie ili maza wetu aweze kufanikisha hili?
Nalog off
 
Huyu Mwigulu hatufai kwenye huu utawala,bora apewe uenyekiti wa kamati za kudumu za bunge huko
 
Nimesoma andiko la TLS, kwa heshima zote kwa chombo chetu hiki kilichopewa mamlaka kisheria, Nimeshtuka sana, I wish to say,

Kwanza KATIBA HAIJAVUNJWA KWA MHE RAIS SAMIA SULUHU kuapa, na wala hakuna Mkanganyiko wowote wa Kikatiba, kwa yeye kutoteua PM na Baraza jipya. Mmekaa wote kweli mkaona hivyo.

Kwa mujibu wa Katiba Ibara ya 42(5) kuna watu wa aina mbili wanaweza kuwa Rais. Moja, Rais Mteule ambaye anatokana na Ibara ya 42(1). Mbili, Mtu anayeshika kiti cha Rais ambaye anatokana na ibara ya 37(5) na 50(2)(d) ambaye ni Makamu wa Rais. Kwa Mazingira haya, Makamu wa Rais, baada ya kifo cha Rais, anakuwa Kaimu Rais baadae ndio ameapa na kuwa RAIS wa Nchi. Rais Mteule anapatikana kutokana na uchaguzi. Hivyo basi ibara ya 57(2)(f) ya Katiba haitumiki katika mazingira haya. Kwa mjibu wa Sheria, Mhe Rais alitakiwa kutoa taarifa hii kwenye Baraza la Mawaziri baada ya kuapa na alifanya hivyo, maana yake Baraza lipo.

Hata hivyo kwa tamaduni za Kiafrika, kitanzania na Misingi ya UTU, SIONI KAMA NI JAMBO JEMA SANA KUANZA KUJADILI MGAWANYO WA MADARAKA TUNGALI HATA HATUJAMZIKA ALIYEKUWA KIONGOZI WETU. HUU SIO MSIBA MDOGO, JAMBO HILI ZITO LIKO MIKONONI MWA RAIS WETU MAMA SAMIA SULUHU, HALAFU SISI TUANZE KUMPATIA MAMBO YA MARA TEUA PM, MARA VUNJA BARAZA, KATIBA INAELEKEZA RAIS KUAPA NA NAMNA YA KUMPATA MAKAMU WA RAIS.

KWA MJIBU WA KATIBA RAIS ANARUHUSIWA KUVUNJA BARAZA MUDA WOWOTE NA KUPANGA ATAKAVYO HATA SIO KWA MAZINGIRA KUAPA KWAKE,

KWANINI HATUIONI HEKIMA YAKE YA KUSHUGHULIKIA MSIBA KUMSITIRI KWANZA ALIYEKUWA KIONGOZI WETU? TUNAANZA NA MAZISHI AU MIRATHI? [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]

Pia soma > TLS: Kwa Mujibu wa Katiba, sasa Tanzania haina baraza la Mawaziri, Rais Samia atakiwa kuteua Waziri Mkuu ndani ya siku 14
TLS Act Section 4(c) inataja madhumuni (objects) za TLS ni:

... ....................to assist the Government and the Courts in all matters affecting legislation, and The administration and practice of the law in Tanzania..........


This means what it says, KUSAIDIA. Haisemi kuipa amri au kuiongoza au kuishauri Serkali, imesema KUSAIDIA. Yaani unasaidia tu pale wakati UMEOMBWA MSAADA. Na kwa vile hiyo no object, ni lazima ulipwe.


Secondly, this is a general clause, a WISH LIST, OBJECTS za taasisi binafsi, si ya Serkali. Kila Lawyer kwenye list ya majukumu yake ni lazima utakuta:

.....TO ASSIST THE GOVERNMENT, TO ASSIST CLIENTS, TO ASSIST....

Ukiangalia madhumuni ya Makandarasi, Wahasibu, Madakatri, Walimu, kila mmoja lazima ana sehemu inasema TO ASSIST CLIENTS, THE PUBLIC, THE GOVERNMENT ETC ETC, of course kwa kulipwa ujira husika, si bure.

Maana yake ni kwamba utasaidia tu ukiombwa msaada, na utalipwa.

Tenganisha na madhumuni ya Polisi: TO ARREST CRIMINALS, TO GUARD PUBLIC PROPERTY. Au ya TPDF au ya TAKUKURU, kazi yao ni WAJIBU wao,siyo kusaidia, si kuombwa, ni JUKUMU ("THE DUTIES SHALL BE:...

MWISHO, Rais ana madaraka ya kuvunja Baraza la Mawaziri, au chochote kila, kwa uamuziwake mwenyewe AT ANY TIME. Rais wa kurithi kama huyu atakaa kwa mujibu wa Ilani iliyopita, kwa hiyo mwanya wa kutenda tafauti
sana ni mdogo, lakini madaraka yako pale pale.

Hawezi akaamrishwa na TLS.

Tulichonacho hapa ni USHAURI WA BURE, hakuna Amri yeyote kwa vile TLS ni tassisi bonafsi haikuchaguliwaxna mtu yeyote. Nadhani TLS katika hili wanejichanganya. Lakini sishangai: hawa si ndiyo watu wa tundulissu na fatmakarume? Sijui kama kuna Mtanzania yeyote ana imani nao.
 
Ili mama afanye Kazi yake vizuri ni lazima avunje kivuli cha Magu na hii ndio changamoto yake kubwa kwa sasa vinginevyo hilo genge litataka kumfanya kwamba yeye hana akili na Urais ameupata kwa hisani sasa hapo Kazi kwake.

Huwezi endesha nchi kwa kufuata genge la mtangulizi,kila Rais ana utashi wake,ndio maana Magu alienda kinyume na JK nk nk

Katiba inampa Rais uamzi huo ,so kwa maoni yangu lazima atimue genge la Chato lote na aweke watu wake royal
 
Back
Top Bottom