Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndiyo, tena nime-summarize tu, mfano ukija kwenye vipozi utakuta kuanzia vipodozi vya ngozi mpaka uturi (perfumes) zile za ghali, zina extracts za bangi.He kumbe zao la bangi linamatumizi mengi hivi?
Nan amekwambia skanka linaumiza watu wewe mama?Nafahamu wengi wakisikia "bangi" akili zao zinakwenda katika kilevi cha bangi. Kilevi cha bangi ni matumizi duni ya bangi, ingawa na yenyewe inaweza kufanyiwa tafiti ikapatikana mbegu isiyo na madhara na ikauzwa kihalali kuliko hivi sasa tunaletewa mbegu za kutia watu wazimu. Mpaka skanka limejaa sasa hivi linaumiza vijana.
Ukisoma huelewi basi hata kuona huoni?Nan amekwambia skanka linaumiza watu wewe mama?
Kongole dada.Mheshimiwa Hussein Bashe, natumai na Rais wetu mama Samia Suluhu Hasan na washauri wake wengine utawafikia ujumbe huu.
Zao la bangi za aina tofauti tofauti (different varieties of hemp) linastawi vizuri sana Tanzania. Ni wakati muafaka, tena tumechelewa sana, kuanzisha zao la bangi kwa faida. Zao la bangi linaweza kututowa kwenye umasikini kwa haraka sana.
Baadhi ya faida zinazotokana na zao la bangi ni pamoja na:
Dawa aina mbali mbali, zinazotumika hivi sasa mahospitalini na dawa mbadala.
Pia bangi inaweza kutengeza karatasi, inaweza kutengeza mbao, inaweza kutengeza, "vigae" vya kuezekea, "boards" mbali mbali za kujengea na kuundia fanicha, inaweza kutengeza bodi za magari ambazo ni bora kuliko za mabati.
Licha ya hayo, inaweza kutengeneza virutubisho mbali mbali vya kutumika na binadam, wanyama na mimea. Pamoja na madawa ya kuzuia wadudu wa mimea.
Pia bangi inaweza kutengeneza mafuta ya kutumika kwenye magari ambayo ni bora kuliko ethanol na methanol.
Kinachotakiwa kufanywa ni kuanza na aina moja au mbili ya bidhaa muhimu na kufunguliwa kituo maalum cha utafiti na kuzalisha mbegu bora kwa biashara.
hatuna haja ya kutegemea mataifa ya nje kwenye hili, tunaweza kuzalisha mali ghafi zetu wenyewe na kuwauzia nje bidhaa zinazotokana na bangi. Ni kujipanga tu.
Nafahamu Bashe utaweza hili kwa ufanisi mkubwa ukilivalia njuga. Weka legacy kijana kupitia bangi.
Nafahamu wengi wakisikia "bangi" akili zao zinakwenda katika kilevi cha bangi. Kilevi cha bangi ni matumizi duni ya bangi, ingawa na yenyewe inaweza kufanyiwa tafiti ikapatikana mbegu isiyo na madhara na ikauzwa kihalali kuliko hivi sasa tunaletewa mbegu za kutia watu wazimu. Mpaka skanka limejaa sasa hivi linaumiza vijana.
Tuondokane na ujinga na kufata watu wa magharibi. Tumepata elimu ili itukombowe siyo tuendelee kuwa wajinga wa kuburuzwa kama misukule, wanachotaka mabwana wakubwa ndiyo tukifate, ni wakati Tanzania tukajifanyia yetu wenyewe na hao wakubwa tuwaimbishe nyimbo tunazotaka sisi. Rasilimali tunazo, kwanini watuendeshe na mali zetu?
Uchumi tunao lakini tunaukalia, Nyerere. Kwa kudanganywa tu na nchi za magharibi tutaendelee kuwa watumwa wao daima.
Naamini ndani ya miaka mitatu ya kuruhusu zao la bangi na tafiti zake za kina, hatutakopa tena nje, sisi tutakuwa wakopeshaji.
Nawasilisha.
Dini yangu ni Uislam, najivunia sana kuwa Muislam.Kongole dada.
Usipoingiza "upofu" wako wa CCM na dini, unakuwa vyema sana kichwani na kuwa na hoja za msingi.
Ubarikiwe sana. Pita hapo Panone Supermarket chukua Sprite lita 2 nakuja kulipa.
Uachane na upofu kwa CCM na dini ili uache legacy ya kuweka mawazo bora ya namna ya kutoka kwenye huu mkwamo tulionao kama taifa kwa maslahi ya Watanzani wote.
Uliyoyaandika ni sahihi sana na kwa kweli sina cha kuongeza zaidi ya kuweka msisitizo kwa serikali kulibeba hili wazo bora na kulifanyia kazi.
Ukishaona imemuathiri mtu basi ujue haimfai,nimeanza kutumia since 2003 kipindi nabalehe na sijaona madhara yake japo wapo watu nimeona wametumia na imewaletea matokeo hasi,ni kama pombe tuu sio wote wana vichwa vya pombeUkisoma huelewi basi hata kuona huoni?
Nenda sober haouse za unga ukaone wavute skanka wanavyojaa siku hizi.
Fanye r"esearch" japo ndogo ya kwenye mtandao ujisomee.
Dunia ya leo unangoja uambiwe wakati unayo kiganjani?
Unajua leo ni ijumaa siku ya swala, nakutakia Ijumaa Kareem mamaWewe mamaya au mamayo?
Bangi ni zao lenye thamani kubwa sana kuliko ujuavyo.Tuna madini,
Tuna gesi
Tuna misitu
Tumeshindwa kupata maendeleo huku kwenye vitu vya thamani kubwa tuje kupata maendeleo kwenye bangi??
twende kwenye soko, gram moja ya bangi na gram moja ya dhahabu,Sikushangai