MINOCYCLINE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2015
- 8,018
- 16,802
" Sekta ya Madini nchini haitakiwi iwe au iwekewe Sheria Kali kwa Wadau wake kwani itawakimbiza na hatutopata Faida yoyote kama Serikali na itatuchelewesha kama nchi. Tuongozwe na Busara pamoja na Hekima na siyo Ukali wa Kupitiliza "
Nimemsikia akizungumza haya Leo Asubuhi katika Kipindi cha Nipashe cha Radio One baada ya Waziri huyu Kukutana na Kamati ya Bunge inayohusika na Madini.
JamiiForums ikiwapendeza mje na Jukwaa litakaloitwa WATAMBUE WANASIASA NA VIONGOZI WANAFIKI TANZANIA kwani kiukweli sasa tumechoka na Wengine tumeshaanza hata Kukereka.
Alianza Spika wa Bunge Ndugai kuhusu Bandari ya Bagamoyo ambaye kabla ya tarehe 17 Machi, 2021 alikuwa hataki ijengwe ila baada ya tarehe hii husika leo anasema ijengwe.
Ni huyu huyu Waziri wa Madini Biteko alikuwa akiufurahia huu huu Ukali na Ubabe dhidi ya Wadau wa Madini, ila baada ya tarehe 17 Machi, 2021 leo nae kabadilika na Kujifanya ni Muungwana na anaungana na Sisi Watanzania tunaojitambua ( wenye Akili ) tuliokuwa hatuupendi Utendaji wa Mpwa wake ( sasa Marehemu kama si Hayati ) pia.
Hakuna Kitu nakichukia tu kama Unafiki.