Waziri wa Maji Jumaa Aweso asisitiza Mamlaka za Maji nchini, kufunga mita za malipo ya kabla

Waziri wa Maji Jumaa Aweso asisitiza Mamlaka za Maji nchini, kufunga mita za malipo ya kabla

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
WAZIRI AWESO ASISITIZA UTEKELEZAJI AGIZO LA RAIS KWA MAMLAKA ZA MAJI NCHINI

Ahimiza ufungaji wa mita za malipo ya kabla


IMG-20240406-WA0010.jpg

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amesisitiza Mamlaka za Maji Nchini ikiwemo Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kuhakikisha agizo la Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan la kufunga mita za malipo ya kabla kwa wateja kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma ya maji kwa wananchi wote.

Ametoa wito huo wakati wa hafla ya futari ya DAWASA na wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa Serikali, Viongozi wa Mkoa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wadau wengine wa Sekta ya Maji iliyoenda sambamba na dua maalum ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan.

IMG-20240406-WA0012.jpg

Amesema kuwa ili kufanikisha utekelezaji wa agizo hilo, Wizara itashirikiana na Mamlaka za Maji Nchini kuhakikisha utekelezaji wa agizo hili unafanyika vizuri.

Mbali na hapo Mhe. Aweso ameitaka DAWASA kuongeza nguvu katika kukabiliana na upotevu wa maji kwenye maeneo yote ya huduma ili kuimarisha usambazaji wa maji kwa wateja wote.

Ameipongeza Mamlaka kwa kuendelea na utekelezaji mzuri wa majukumu yake ya kutoa huduma bora kwa wananchi na kuahidi Wizara kuendelea kutoa ushirikiano mkubwa ili huduma ya majisafi iweze kuwafikia wote sambamba na malengo ya Serikali ya kusambaza maji mijini kwa asilimia 95 na vijijini kwa asilimia 85 kufikia mwaka 2025.

IMG-20240406-WA0013.jpg

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ndugu Edward Mpogolo ameipongeza Serikali kwa jitihada kubwa zinazofanyika za kuhakikisha huduma ya maji inafika kwa kila mwananchi.

"Kazi kubwa imefanyika na Serikali kwa kupitia DAWASA ya kuboresha upatikanaji wa huduma kwa wananchi wote hususani wa Mkoa wa Dar es Salaam," ameeleza Ndugu Mpogolo.

Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Ndugu Laston Msongole ameishukuru Wizara kwa kuendelea kutoa ushirikiano mkubwa kwa DAWASA na kuwezesha utekelezaji mzuri wa majukumu ya kutoa huduma ya maji kwa wote.

Amesema DAWASA imejipanga kikamilifu kuhakikisha utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan la ufungaji wa mita za malipo kabla linatekelezwa na tayari zoezi limeanza kwa majaribio kwenye baadhi ya maeneo.
 
Hiki kitu practically ni worse. Hakuna haja ya kuimpliment hii takataka.
Hizi ni bench project tuu, kwenye uhalisia ni changamoto kubwa sana

Tusiingie kwenye huu mtego.
Am saying in technical perspective 🙏
 
Ila hii tabia ya ku allied mambo ya serikali na futari za dini inakera sana. Mara bank fulani imefuturisha wateja wake, mara ofisi fulani ya serikali imeandaa ifta, kwani kuna ulazima wa kuandaa event kwa futari ya dini? Kibaya zaidi viongozi wa idara/ofisi hizo wanavalia kidini kana kwamba serikali ni ya kidini.

Huu ni upuuzi wa kidini unaoingizwa serikalini wakati inajulikana nchi haiongozwi kwa misingi ya dini fulani. Viongozi wamekosa haya kunasbisha event za serikali na unasaba wa dini.

Miaka ya nyuma haya mambo ya dini kuingizwa serikalini kwa namna yeyote ile yalikemewa waziwazi na kukomeshwa.

Kiongozi wa serikali kuvaa vaa kanzu na barghashia inaleta ukakasi na haipendezi katika nchi isiyo ya kidini fulani. Hayo mavazi ya dini wakayavae kwenye shughuli inayohusu dini yao
 
Back
Top Bottom