Waziri wa Mambo ya Ndani asonga ugali wa wafungwa katika gereza la Isupilo wilayani Mufindi mkoani Iringa

Waziri wa Mambo ya Ndani asonga ugali wa wafungwa katika gereza la Isupilo wilayani Mufindi mkoani Iringa

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Hawa ndio viongozi wa kuivusha Tanzania!

Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene, akisonga na kula ugali wa wafungwa katika Gereza la Isupilo, Wilayani Mufindi, Mkoa wa Iringa, alipolitembelea gereza hilo katika ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa taasisi zake mkoani humo.
1627032127009.png
 
Hii habari haiwezi kusikika mbali kama habari za kukamatwa akina Mbowe kwa suala la kongamano la katiba.
Na kama hii habari ni kweli, tuna safari ndefu kuliko hata wanazuoni wengi wanavyodhani.
Vijana wanaita habari kama hizi ni 'kick '.
 
Ni ujinga kujadili kazi anayoifanya waziri, kwani ukiwa waziri ghafula unakuwa si binadamu wa kawaida?

Ukisonga ugali unajadiliwa utadhani hawi tena binadamu kama wengine,

Badala ya kuleta hoja za katiba sasa mnaleta hoja za hovyohovyo tu, na ccm walishawajulia, mkianza mijadala mhimu tu, waziri anajitokeza akiwa shamba akilima na ng'ombe, mnaanza kumjadili yeye

Doh! Bongo, bongo kweli
 
Asiishie kusonga alale na kulala kabisa humo gerezani Ili aonje ladha ya kunguni na mbu Ili kudumisha uzalendo
 
Jamani wanaCCM waambieni watu wenu waache maigizo wawe serious basi kidogo badala aje na mpango wa kuboresha mazingira ya wafungwa na Askari analeta maigizo na kupiga picha, wakati juzi kati katoka kumlalamikia mkurugenzi wa vitambulisho vya NIDA yaani "waziri" analalamika kumbe wanafanya futuhi 😄😄😄
 
Za kusonga unga wa ngano zinaouwezo wa kusonga ugali pia
Kama hazitumiki huku kwetu Tanzania, bado hilo ni gepu la kuzibwa. Hata hivyo, kama inawezekana tutengenezee clip ya hiyo mashine ya kusonga unga wa ngano ikitumika kusonga ugali wa unga wa mahindi nakisha unga wa muhogo.

Natanguliza shukrani.
 
Kama hazitumiki huku kwetu Tanzania, bado hilo ni gepu la kuzibwa. Hata hivyo, kama inawezekana tutengenezee clip ya hiyo mashine ya kusonga unga wa ngani ikitumika kusonga ugali wa unga wa mahindi nakisha unga wa muhogo.
Check madukani ya vyombo vya jikoni zipo
 
Check madukani ya vyombo vya jikoni zipo
Mkuu mimi nilidhani umeisha ijaribu kuitumia kusonga ugali wa mahindi ama muhogo, yaani unauzoefu na matumizi ya mashine hiyo. Kama bado hujaitumia basi wazo langu bado lina thamani, hivyo wanajukwaa waniunge mkono.
 
Back
Top Bottom