Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amelipongeza jeshi hilo kwa kusimamia ulinzi na usalama kwa weledi katika mkutano mkuu wa CCM uliofanyika Dodoma pamoja na wa Chadema uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Bashungwa amesema hayo leo Januari 22, 2025 wakati alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Dodoma na kusisitiza kuwa, vyama vya siasa kutimiza wajibu wa kutii sheria bila shuruti ili kuepuka kulazimishwa kutii sheria.
“Matarajio yangu ni kwamba haki hii mnayoitenda Jeshi la Polisi kwa kutoangalia itikadi, pia vyama vya siasa kwa jumla, haki hii ije na wajibu kwa wao kutii sheria bila shuruti, hakuna haki bila wajibu” amesisitiza Bashungwa.