Iyerdoi
JF-Expert Member
- Jun 30, 2012
- 2,717
- 3,895
Nanukuu: "kikao hicho kilihusu mambo yanayohusu Usalama na Amani ya nchi ikiwemo kujadili matukio ya kiuhalifu yanayotokea sehemu mbalimbali nchini na hatua zinazochukuliwa kuendelea kudhibiti matukio hayo".Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amekutana na kufanya kikao na Uongozi wa Jeshi la Polisi nchini ukiongozwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura ambapo kikao hicho kilihusu mambo yanayohusu Usalama na Amani ya nchi ikiwemo kujadili matukio ya kiuhalifu yanayotokea sehemu mbalimbali nchini na hatua zinazochukuliwa kuendelea kudhibiti matukio hayo.
Kikao hicho kilichofanyika Jijini Dodoma kimehudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Maduhu Kazi.
Upande wa Jeshi la Polisi kilihudhuriwa na Viongozi wafuatao Kamishna wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimaliwatu, Suzan Kaganda, Kamishna wa Fedha na Lojistiki, Liberatus Sabas, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo, Awadh Juma Haji, Kamishna wa Sayansi ya Uchunguzi wa Jinai, Shabani Hiki, Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai, Kamishna wa Polisi, Ramadhani Kingai, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna,David Misime, Naibu Kamishna kutoka Kamisheni ya Intelijensia na Jinai, Kheriyangu Khamis Mgeni, Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Jumanne Muliro.
Kikao hicho kimeonesha mapungufu yafuatayo:-
1. Hakuna Mdau mwingine walau hata mmoja aliyekaribishwa kikaoni ila badala yake wamekaa wao wenyewe Maafande (Watendaji/Watekelezaji)na Waziri na kuwasahau wale wanaowatumikia i.e. Raia. Walisahau umuhimu wa watu hao kwamba hao ndo miongoni mwao wapo wahalifu na walio wema, hao ndo wenye kutatiza usalama na amani ya nchi, hao ndo wengi na wenye nafasi kubwa sana kuchangia uwepo wa Amani na Usalama wa nchi kwa ujumla.
2. Suala la Usalama na Amani ya nchi ni Suala mtambuka na kamwe sio la Polisi na Waziri wa Mambo ya ndani.
Kwa kujitenga kwao hivyo ni kama kusema "Nyie wengine haiwahusu". Lakini uhalisia unabaki kwamba mbona suala la Usalama na Amani ya nchi sio siri? Siri inakuwa kwenye utendaji kwa kutumia Utaalam wao waliosomea lakini ukweli ni kwamba sisi SOTE (wao na wadau) tunahitaji sana Usalama na Amani ya nchi. Tunahitaji sana ushirikiano. Tusibaguane kwenye uwekaji wa Mikakati kwani Usalama na Amani vikiharibika au kutatizika, hakuna ambaye hataguswa - tutaathirika wote.
Ni hayo tu.