Waziri wa Mambo ya Ndani, Masauni aitisha Kikao na Uongozi wa Juu wa Jeshi la Polisi

Nanukuu: "kikao hicho kilihusu mambo yanayohusu Usalama na Amani ya nchi ikiwemo kujadili matukio ya kiuhalifu yanayotokea sehemu mbalimbali nchini na hatua zinazochukuliwa kuendelea kudhibiti matukio hayo".
Kikao hicho kimeonesha mapungufu yafuatayo:-
1. Hakuna Mdau mwingine walau hata mmoja aliyekaribishwa kikaoni ila badala yake wamekaa wao wenyewe Maafande (Watendaji/Watekelezaji)na Waziri na kuwasahau wale wanaowatumikia i.e. Raia. Walisahau umuhimu wa watu hao kwamba hao ndo miongoni mwao wapo wahalifu na walio wema, hao ndo wenye kutatiza usalama na amani ya nchi, hao ndo wengi na wenye nafasi kubwa sana kuchangia uwepo wa Amani na Usalama wa nchi kwa ujumla.
2. Suala la Usalama na Amani ya nchi ni Suala mtambuka na kamwe sio la Polisi na Waziri wa Mambo ya ndani.
Kwa kujitenga kwao hivyo ni kama kusema "Nyie wengine haiwahusu". Lakini uhalisia unabaki kwamba mbona suala la Usalama na Amani ya nchi sio siri? Siri inakuwa kwenye utendaji kwa kutumia Utaalam wao waliosomea lakini ukweli ni kwamba sisi SOTE (wao na wadau) tunahitaji sana Usalama na Amani ya nchi. Tunahitaji sana ushirikiano. Tusibaguane kwenye uwekaji wa Mikakati kwani Usalama na Amani vikiharibika au kutatizika, hakuna ambaye hataguswa - tutaathirika wote.
Ni hayo tu.
 
Kwani ili uwe Waziri wa Ulinzi ni sharti ujue kushika binoculars?
Huwa nina imani kwamba duniani hakuna swali la kijinga. Lakini,hilo lako ngoja nitafakari kama ni "sharti",lazima au kuna umuhimu wa kujua kushika binoculars kwa waziri husika!Halafu,niende mbele zaidi nijiulize;Kama aligeuza binocular,aliona mbali au alijiangalia kwa karibu?
 
Kaita kikao au kawaita ofisini?
 
Ni kweli hakuna swali la kijinga.
Ukigeuza binoculars utaona vitu viko mbali sana i.e. Wewe ulikusudia/ulitaka uvione kwa ukaribu zaidi lakini kwa kufanya/kuishika binoculars kinyume utaviona lakini vitaonekana kuwa mbali zaidi ya ulivyotegemea.
 
Kwani ili uwe Waziri wa Ulinzi ni sharti ujue kushika binoculars?
Si lazima kama upo Banana republic. Ila kama ni kwenye mataifa ya maana, hukuti daktari wa mifugo anateuliwa kuwa Waziri wa Maji au mwalimu wa Michezo anakuwa Naibu Waziri wa Teknolojia. Wala hukuti aliyekuwa Wizara ya Afya anahamishiwa Wizara ya Habari, kila mtu anachezea anakomudu na akifeli anawekwa pembeni sio kuhamishwa.
 
Ni kweli hakuna swali la kijinga.
Ukigeuza binoculars utaona vitu viko mbali sana i.e. Wewe ulikusudia/ulitaka uvione kwa ukaribu zaidi lakini kwa kufanya/kuishika binoculars kinyume utaviona lakini vitaonekana kuwa mbali zaidi ya ulivyotegemea.
Lengo la mtazamaji litakua limetimia?
 
Huyu mwenye suti nyeusi mbona anaonekana bwana mdogo sana ndio nani cheo chake ?
 
 
Masauni kuachia ngazi sio kosaa ,Wizara imekushindaa .achia tuuu
 
Hawana conference room mpaka wafanyie chumbani?
 

Huyu kauawa au?
Yeah alitekwa na siku Anakuja kupatikana kapatikana akiwa mfu na Kafungwa kwenye boda yake kama picha inavyoonesha
 
Kupongezana kwa show waliyoifanya Mbeya na Iringa? Au kukumbushana majukumu muhimu ya Kikatiba?

Sisi wananchi tumegoma kuwapa polisi ushirikiano kwa sababu wao wanajua kila kitu na hawwtuhitaji ndo maana wanaua raia hovyo kila wakipata nafasi.

Polisi ya Tanzania ni janga la kujitakia
 
Hoja za kutekwa na kupotea zitachukua nafasi kubwa ya mazungumzo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…