Waziri wa Michezo Dkt. Ndumbaru kama sasa TFF wameamua Makocha wa Taifa Stars watakuwa ni Wazawa Kocha Amrouche Mshahara anapewa wa kazi ipi?

Waziri wa Michezo Dkt. Ndumbaru kama sasa TFF wameamua Makocha wa Taifa Stars watakuwa ni Wazawa Kocha Amrouche Mshahara anapewa wa kazi ipi?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Najua unanisoma sana GENTAMYCINE hapa JamiiForums hivyo nasubiria Jibu lako kwani Wewe ulivyo na Kiherehere baada ya Kocha Amrouche Kutukera Watanzania kule AFCON ulisema tena kwa Kujiamini kabisa kuwa Kocha Amrouche bado ni Mwalimu Mkuu wa Taifa Stars ila hivi karibuni / majuzi tu Rais wa TFF Wallace Karia alisema tena na kutuhakikishia Watanzania kuwa kuanzia sasa Makocha wa Timu ya Taifa (Taifa Stars) watakuwa ni Wazawa tu.

Wachunguzi wa Mambo tunajua kwanini Kocha Amrouche bado analipwa Mshahara wake Mnono wakati hakuna Kazi aifanyayo sasa na labda nikuonye tu kuwa huu Ujanja Ujanja (Usamjo Usamjo) wako unaoufanya kwa Mgongo wa huyo Kocha usipoangalia utakugharimu na Utatumbuliwa kwa Kashfa ndani ya Siku nyingi. Haraka sana Tangaza kwa Watanzania kuwa Serikali imesitisha Kumlipa Mshahara Kocha wa hovyo hovyo Amrouche na Waambie TFF ambao wanakuogopa ili wasiharibi Uhusiano wao na Serikali kuwa na Wao watangaze rasmi kuwa Amrouche siyo tena Kocha wa Taifa Stars.
 
Bado ana mkataba, itakua pesa ya kuvunja mkataba ni kubwa ukilinganisha na ya kumlipa mkataba
 
Back
Top Bottom