Ndiyo maana nikauliza, na kubeti nako Waziri atalazimisha watu wabeti kizalendo?
Kwamba hata watu wakijua timu ya Tanzania haitoboi asilani, atalazimisha wabeti kizalendo tu kwenye timu ya Tanzania?
Kuna watu hawajielewi 100% suala la mpira ni burudani tu, kama wengine wanavyochukulia kufanya ngono kamastarehe, au kunywa pombe kama starehe ndo vivyo hivyo hata katika soka, mpira hajawahi kuwa kipimo cha uzalendo,
Sasa kama mpira ni starehe kama starehe zingine ni sawa na jamaa kuja kukwambia upige bao ngapi, au unywe kinywaji chako, by the way katika socca tunalipia galama kuingia uwanjani kwa pesa zetu wenyewe na ratiba zetu wenyewe, leo hii huwezi kunipangia nishabikie team gani, au ipi nisishabikie bali nitashanikia ile team ambayo naona ndio itanipa raha au itakidhi uhitaji wa furaha yangu kwa siku hiyo,
Afu swala la mashabiki kushabikia vilabu ambayo sio vya nchi zao kwenye International games sioBongo tu, Imagine waarabu na itikadi zao na udini wao ila linapokuja swala la mpira wanashabikia vilabu vya mataifa mengine, sasa itakuwaje bongo hii tuanze kulazimisha, na hizo mbwembwe ndio zinakuza soccor na kuleta chachu,
Afu jamaa anavyosema Jezi kwake anaona Jezi sio kitu cha maana hii ni kuonesha mpira haujui kwetu sisi mashabiki wa soka jezi ni mhimu sana kwetu hata zaidi ya kadi ya uanachama maana jezi ni kitu kinaweza kukutambulisha popote unapoenda tofauti na kadi ambayo inakaa kwenye warret,
Jezi huleta umoja,
Jezi huleta ushirikiano,
Jezi huleta muungano,
Jezi husaidia watu kutambuana,
Jezi huleta upendo,
Zaidi na zaidi jezi hiyo unayoiona sio ya maana ila imesababisha baadhi ya watu kupata ajira na wengine kupata kipato.
Acheni kuleta siasa katika mpira hiki sio kijiwe cha wauza kahawa,
Pia linapokuja swala la uhuru wa mtu binafsi ni pamoja nakuchagua kipi kinakupa furaha mathalani hauvunji sheria, sasa leo Mjinga mmoja aniforce nishabikie team flani au nipigwe kisa nimevaa jezi ya team hiyo kikatiba nakisheria ni kosa gani sasa.
Acheni uchawa katika soka lambaneni mguu huko mlikozoea, huku kwetu mkijichanganya tutawanyoosha. Na mtauponza.