Waziri wa TAMISEMI umelala wapi milioni 500 za miradi ya afya zinatafunwa Singida

Waziri wa TAMISEMI umelala wapi milioni 500 za miradi ya afya zinatafunwa Singida

MAHANJU

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
5,252
Reaction score
8,003
Wasalaam wanajukwaa!

Na Gregory Jumbe Mahanju,

Nataka kutuma ujumbe kwa wateule wa Rais Samia Suluhu Hassan akiwemo Waziri wa TAMISEMI Ndg Angela Kairuki, Katibu mkuu wa TAMISEMI,Mkuu wa mkoa wa Singida ndugu Petter Serukamba na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi ndugu Jery Cornel Muro ya kwamba Pesa alizotoa Mama Samia shilingi milion 500 zilizotolewa kwa ajili ya ujenzi wa Vituo vya afya NTUNTU na IRISYA zinatafunwa na watumishi wasiokua na huruma kwa fedha za umma. Ujenzi wa vituo hivi vya afya ulikua ukamilike tangu mwezi wa 7 mwaka huu lakini mpaka sasa mwaka unaisha hakuna kilichokamilika wala hakuna majibu ya kueleweka kutoka kwa watendaji wa serikali.

Ni takribani zimepita wiki 3 zimepita tangu mkuu wa Wilaya hiyo ndugu Jery Muro atoe maagizo kwa ofisi ya TAKUKURU Wilayani humo kuwakamata maafisa 3 waliokua wakisimamia ujenzi wa Kituo cha Afya Irisya baada ya kubaini kuna ubadhirifu mkubwa wa pesa za Mhe Rais. Lakini pamoja na hayo yote wananchi na baadhi ya viongozi ndani ya Wilaya hiyo wanadai Mkuu wa Wilaya anamuogopa Mkurugenzi wa Halmashauri ndugu Justine Kijazi ambaye inasemekana yeye ndiye msimamizi mkuu wa miradi hiyo na pia inadaiwa kua ununuzi wa vifaa vya ujenzi unafanywa na mke wake kutoka kwenye maduka yake ya ujenzi. Inawezekana DC anatoa maagizo kukamatwa kwa dagaa lakini wakaachwa Kambare ambao ndio chanzo kikuu cha utafunaji wa pesa hizi. Wananchi wanaomba ikiwa DC anamuogopa Mkurugenzi huyo basi RC wa mkoa huo na Baraza la madiwani wanaogopa nini?

Siku ya jana tarehe 21/11/2022 mbunge wa jimbo la Singida Mashariki ndugu Miraji Mtaturu aliamua kufanya ziara ya kushtukiza katika ujenzi wa kituo cha Afya Ntuntu ambacho kipo jimboni mwake na kujionea kwa masikitiko makubwa jinsi ambavyo pesa za Mama Samia zinatafunwa mchana kweupe. Ndugu Miraji Mtaturu ameongea kwa sauti ya ukali na huruma sana kwa kuwaomba TAKUKURU katika Wilaya hiyo kufanya uchunguzi wa mradi wa ujenzi wa kituo hicho pamoja na kwenda mbali zaidi kuapa kuwashtaki kwa Mhe Rais na bungeni wale wote waliotafuna pesa za umma.

Niasikitiko makubwa sana kuona miradi ambayo ni ya huduma za msingi kabisa kwa wananchi pesa zinatafunwa bila huruma. Hivi huyu DED wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi anaogopwa? Kwanini anaacha kushughulika na matatizo ya wananchi na badala yake anatumia rasilimali za umma kujinufaisha yeye na familia yake? Kwanini miradi ya umma inanusuasua na malalamiko yote yanaelekezwa kwake?

Ni wakati sasa watendaji wa juu wa Mama Samia kuchukua hatua, ndugu Waziri sijui ni kwanini kuna kigugumizi juu ya hili?
 
Kwamba wamehack account yake ya Bank wakamuibia pesa zake?
 
Kwa hiyo mama Samia aliingia mfukoni kwake akatoa 500 mil.
 
Huyo waziri hpn kwa kweli hawezi ile wizara sijui ni nani alimshauri mama wetu amlete wizra hyo si angempa ubaliz au mkuu wa wilaya uko uko same
 
Back
Top Bottom