Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) ni miongoni mwa viongozi walioshiriki Kikao cha Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Magu.
Kikao hicho ngazi ya Wilaya kimefanyika leo tarehe 11 Septemba, 2022 katika Ofisi ya CCM Wilaya.
Viongozi wengine Walioshiriki kikao hicho ni pamoja na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja (Mb.), Mbunge wa Jimbo la Magu, Boniventure Kiswangwa, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu, Mpandalume Simon, Katibu wa CCM Wilaya ya Magu Bi. Moza Ally, pamoja na Wajumbe wengine.