JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) ametoa wito wananchi kuacha kuvamia maeneo ya jeshi na kuweka makazi kwa kuwa ni hatari kwa usalama kwao na nchi kwa jumla.
“Ili Jeshi liweze kutekeleza majukumu yake linahitaji maeneo, na maeneo hayo yanakuwa ni ya kimkakati, kwanza ni hatari kwao na hatari kwa usalama.
“Wanapofanya mazoezi wanatumia vitu vingi, unaweza kuona ni eneo kubwa ukaweka mizigo yako mwisho ukasababisha madhara, tunaomba waache maeneo ambayo yametengwa kwa ajili ya jeshi,” anasema Dkt. Stergomena.
Aidha, ameelezea kufurahishwa na mwenendo wa Utendaji kazi wa Watumishi walio chini yake upande wa Wizara pamoja na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) chini ya Uongozi Mahiri wa Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Salvatory Mabeyo.
Waziri Stergomena Tax ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam alpokuwa akihojiwa katika kipindi cha TWENDE PAMOJA kinachoandaliwa na Kurushwa na Channel Ten.