Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mkutano huo wa Waziri wa Ulinzi na JKT ulikuwa na lengo la kujadili matumizi bora ya ardhi kati ya jamii ya Wafugaji wa Monduli pamoja na kujadili changamoto mbalimbali za matumizi ya ardhi wilayani hapo, ambazo zimejitokeza katika siku za karibuni, aidha Waziri Tax alipata fursa ya kupata taarifa zinazohusu Mafunzo ya Kijeshi katika eneo hilo.
Akimkaribisha Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, kuzungumza, Mbunge wa Jimbo la Monduli, Fred Lowassa amemshukuru Waziri wa Ulinzi na JKT kwa kufika Monduli kwa haraka baada ya kuombwa kufanya hivyo naye, kuja kujadiliana na viongozi wa kimila wa jamii ya wafugaji na wakulima, na namna bora ya kutatua changamoto zinazohusiana na matumizi ya ardhi na kuimarisha uhusiano wa muda mrefu baina ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania pamoja na wananchi.
Pia, Waziri Tax amewaambia wananchi wa eneo la Monduli kuwa taratibu zote za kisheria ili kila mtu apate haki yake na kwa usawa zitafuatwa.
Mkutano huo wa Waziri wa Ulinzi na JKT ulihudhuriwa pia Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Festo Shem Kiswaga pamoja na viongozi wa jamii ya wafugaji wa jamii ya Kimasai, Halmashauri ya Mji wa Monduli na viongozi waandamizi toka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.