Waziri wa Utumishi iangalie vizuri Wizara yako, Upandishaji Madaraja umeshindikana sababu ya Mfumo

Waziri wa Utumishi iangalie vizuri Wizara yako, Upandishaji Madaraja umeshindikana sababu ya Mfumo

Mizega

Senior Member
Joined
Feb 10, 2021
Posts
150
Reaction score
321
Mhe Waziri pole na Majukumu yako ya kila siku, hivi karibuni Ofisi yako ilitoa waraka wa kuwapandisha madaraja Watumishi wenye vigezo, ukiachilia mbali changamoto ya watumishi wakongwe na juniors kulundikwa kwenye daraja moja (mfano mtu aliyeajiriwa 2013-2014 kuwekwa sawa na mtu wa 2016).

Mfumo wa Lawson umekufa na Maafisa Utumishi hawafanyi kazi zao ipasavyo.

Ingilia kati suala hili likome kwani kutasababisha madai ya malimbikizo ya mishahara na kuwanyima haki watumishi. Upandishaji vyeo kwa karatasi bila mfumo ni kuwahadaa Watumishi.
 
Mambo yamesimama kisingizio mtandao! Ina maana mwaka mzima ukisumbua kazi hazitafanyika?
 
Wataishia kupata malalamiko kwa wale ambao wataachwa. Nafikiri mwendazake alivuruga sana utumishi wa umma kwa kujifanya kuendesha mambo kimungu mtu, wengine tunalo la kujifunza.
 
Duh,naona TZ ya changamoto ikirudi kwa kasi tena!
 
Daah, Waziri wa Utumishi na Utawala bora alishughulikie hili pamoja na kulipa malimbikizo ya mishahara kabla ya mengine yote.
 
Back
Top Bottom