TANZIA Waziri wa zamani, Dkt. Pius Yasebasi Ng'wandu afariki dunia

TANZIA Waziri wa zamani, Dkt. Pius Yasebasi Ng'wandu afariki dunia

Mbunge wa zamani wa jimbo la Maswa pia aliwahi kuwa Waziri, Dkt Pius Ng'wandu amefariki dunia.

Amefariki Usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Somanda mjini Bariadi.

Alikimbizwa jana katika Hospitali hiyo baada ya kupata matatizo ya presha.

Mungu amlaze Mahali pema Peponi.

Dr. Pius Yasebasi Ng’wandu aliwahi kuwa balozi wa Japan Tokyo 1990 hadi 1993

Waziri wa Sayansi na Teknologia mwaka 2000 hadi 2008

View attachment 1653866
Balozi Pius Yasebasi Ng'wandu enzi za uhai wake
Du aisee ni wiki kama mbili zimepita tumeona ameoa binti mbichi, binti kawa mjane sasa.Apumzike kwa amani mh balozi.
 
MGOGORO wa kifamilia umezuka baada ya kifo cha aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan, Dk. Pius Ng’wandu, kuhusu mahali yatakapofanyika mazishi yake.

Dk. Ng’wandu aliyewahi kuwa waziri katika serikali zilizopita akihudumu wizara mbalimbali, alifariki asubuhi kuamkia leo, Desemba 19, 2020 mjini Bariadi, Simiyu baada ya kuugua ghafla. Alifariki muda mfupi alipofikiswa Hospitali ya Mkoa wa Simiyu, Somanda, iliyopo mjini Bariadi.
Taarifa zilizotufikia SAUTI KUBWA zinaeleza kuwa kumezuka mgogoro kati ya watoto wa marehemu na mjane wake, Mary, aliyefunga ndoa naye mwezi Oktoba, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Mke wa kwanza wa Dk. Ng’wandu, Lucy, alifariki Aprili 25, miaka sita iliyopita baada ya kuugua kwa shinikizo la damu. Alizikwa Makabe, Dar es Salaam. Aliacha watoto watano; wasichana watatu na wanaume wawili.

Taarifa zinaeleza kuwa watoto wa marehemu, Dk. Ng’wandu wanataka baba yao azikwe pembeni ya kaburi la mkewe wa kwanza, Lucy, huku mjane wake, akipendekeza azikwe Sumve, eneo ambalo kuna ukoo wa marehemu, na kwamba Ng’wandu alichangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya eneo hilo alipokuwa mbunge kwa miaka 15.

SAUTI KUBWA imeelezwa kwamba mke mpya amewaeleza ndugu wa marehemu kwamba mumewe, pamoja na kuwa hakuandika azikwe wapi, lakini aliwahi kueleza kwamba atakapofariki, azikwe jirani na hapo.
Taarifa zilizotufikia jioni leo, zinaeleza kuwa watoto wawili wa marehemu, Dolres na Alex, tayari wako safarini kwenda Bariadi ili kushawishi famili ili kufanikisha “mapendekezo” ya baba yao kuzikwa pembeni mwa kaburi la mkewe wa kwanza, Makabe, Dar es Salaam.

“Mtoto mmoja amefika hapa Bariadi, mwingine kaka yao amefika Mwanza jioni hii na safari ya kuja hapa imeanza, kazi kubwa ni kujadili mahali pa kumpumzisha mzee wetu,” ameeleza ndugu wa Dk. Ng’wandu aliyeko Bariadi, hakupenda kutajwa jina.

Mvutano huo wa maziko ya Dk. Ng’wandu, umeelezwa na wakili John Masele kwamba kisheria, mke wa marehemu anatambuliwa na kupewa nguvu zaidi na sheria juu ya uamuzi wa chochote cha marehemu.
“Ikiwa marehemu hakuandika wosia, na yuko na mkewe, sheria inambeba zaidi mkewe halali, sasa kwa hili la Dk. Ng’wandu kama kweli kuna mgogoro, mkewe anaweza kuamua azikwe wapi, lakini majadiliano na watoto yanaweza kuleta muafaka na kuepusha mvutano,” amesema wakili huyo aliyebobea masuala ya familia.

Kuna taarifa kuwa katika miezi michache iliyopita, watoto hao walivutana na baba yao wakipinga wazo mpango wake wa kuoa mke mwingine. Alipowashirikisha wazo hilo, walimkatalia katakata kw amadai kuwa umri wake ni mkubwa mno kuwa na mke mpya.
Dk. Ng’wandu alizaliwa mwaka 1944 huko Budekwa Maswa. Mjane, ambaye ndiye alikuwa mke wake mpya aliyemuoa Oktoba mwaka huu, ana miaka 33.

Baada ya watoto hao kumgomea kuhusu mpango wake huo, Dk. Ng’wandu aliamua kufunga ndoa isiyo na mbwembwe akisindikizwa na watu waapatao sita. Picha na ndoa hiyo zilisambazwa mitandaoni na kuibua gumzo katika jamii.

SAUTI KUBWA imeambiwa kuwa hata watoto hao wa Dk. Ng’wandu walipata taarifa za ndoa hiyo baada ya picha hizo kusambazwa mitandaoni.

Taarifa zinasema kuwa kila walipompigia simu kumuulizia habari hizo, akiwa safarini mikoani na mkewe mpya, baba yao aliwambia: “Msiwe na wasiwasi, niko salama. Nitawajulisha nitakaporudi Dar es Salaam.”

Tangu Oktoba, Dk. Ng’wandu na mkewe mpya wamekuwa ziarani Arusha, Tanga na Morogoro. Walikuwa wakielekea Sumve ambako Dk. Ng’wandu, shabaha ikiwa ni kumtambulisha mkewe kwa wana ukoo.

Dk. Ng’wandu amewahi kuongoza wizara za elimu ya juu, maji, ardhi, nyumba na kwamba baada ya kustaafu utumishi wa umma, alisoma sheria Chuo Kuu Huria cha Tanzania na baadaye kuidhinishwa kuwa wakili waliomaliza kwa ufaulu, Shule Kuu ya Sheria.

 Like



Sent from my Infinix X622 using JamiiForums mobile app
 
Mbunge wa zamani wa jimbo la Maswa pia aliwahi kuwa Waziri, Dkt Pius Ng'wandu amefariki dunia.

Amefariki Usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Somanda mjini Bariadi.

Alikimbizwa jana katika Hospitali hiyo baada ya kupata matatizo ya presha.

Mungu amlaze Mahali pema Peponi.

Dr. Pius Yasebasi Ng’wandu aliwahi kuwa balozi wa Japan Tokyo 1990 hadi 1993

Waziri wa Sayansi na Teknologia mwaka 2000 hadi 2008

Ng’wandu aliwahi kuwa Mbunge wa Maswa, pia Waziri wa Ardhi, Maji, Nyumba na Maendeleo ya Mji kuanzia mwaka 1985 hadi 1987, na alikuwa Waziri wa Maji 1987 hadi 1990, nafasi ambayo aliishika tena mwaka 1996 hadi 1999.

View attachment 1653866
Balozi Pius Yasebasi Ng'wandu enzi za uhai wake
Angekuwa mchagga asingekufa
 
Wewe ni kilaz.a sana kwanza hakuna mtu alikuwa anaitwa zitto zitto bali alikuwa ni ZITTO KABWE,pia hakuwa Waziri Mkuu bali Katibu Mkuu na pia hakuna kitu kilikuwa kinaitwa UDSA bali ni DARUSO (Dar es Salaam University Students Organization).
Hata wale wanafunzi waliokosa mikopo na baadaye wakapewa hawakuwa 203 bali walikuwa 603.
Watu wengine mbona mko weupe sana vichwani,hivi maisha mnatoboaje?!!!!
Mkumbushe kistaarabu tuu maana huo usahihi uliouleta hapa haubadili exchange rate ya leo ya USD.
 
juzi mlipoleta uzi kwamba mzee kaoa toto dogo nikajua tu ameoa Mchaga leo ndio nimeamini alioa mmachame.

Ameshindwa kjifunza kwa R.Mengi.
Rest in Peace mzee hakika umeumaliza mwendo.🙏🙏🙏
Nini kinakufanya uamini kaoa Mchagga au Mchame
 
Back
Top Bottom