Waziri Zungu: Mitumba inachafua mazingira

Waziri Zungu: Mitumba inachafua mazingira

Nikushukuru sana Rais kwa kuniamini na kuniteua kuwa Waziri, wakati nakuja Watu waliniuliza utavaa nguo zako za mitumba au utavaa kitu kipya, lakini leo nimetia suti mpya, maana hatas hiyo mitumba ni sehemu ya mazingira na ni sehemu ambayo inachafua hadhi ya Nchi yetu.

Rais Magufuli umefanikiwa sana kupiga vita mifuko ya Plastic, lakini sasa mifuko hiyo inarudi kwa njia za pembeni, vifungashio (packages) sasa vinaboreshwa na Watu wanabebea vitu na kuharibu mazingira, watu wa NEMC tuulize kwanini vitu hivi viko mitaani, nitalifanyia kazi

Kwa Watu wa Wizarani (Muungano na Mazingira) urafiki upo lakini kwenye kazi za Umma hatutofanya urafiki, tukikutana nje ya kazi za Umma tutaendelea na Urafiki wetu

Amakweli mwenye shibe kamwe hamjui mwenye njaaa sasa tusubiri mapya ya kupiga marufuku mitumba.

View attachment 1337322

Sent using Jamii Forums mobile app
hatimaye Baraza la mawaziri limepata mjumbe mwenye asili ya Asia.
 
Mkuu sikuamini alicho kitamka lkn ndiyo hivyo tena maana mwenzetu tayari yupo matawi ya juu sasa.
Hivi Zungu Anafikiri kwamba huko kijijini nako kuna maduka ya nguo kila kona kama ilivyo Kariakoo?

Ifike mahala viongozi wafikirie kimapana wasifikirie kama wako kwenye chupa kwamba Tanzania nzima iko kama dar.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hayo wayasikie wauza mtumba wa ilala na karume maneno ya mbunge wao hayo anataka tuvae supesheri


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kama huyu?
Maneno tu hayo.
Ajue walikuwepo walionengua hadi viuno!
Muache abwabwaje tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
FB_IMG_1579773272376.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi Zungu Anafikiri kwamba huko kijijini nako kuna maduka ya nguo kila kona kama ilivyo Kariakoo?

Ifike mahala viongozi wafikirie kimapana wasifikirie kama wako kwenye chupa kwamba Tanzania nzima iko kama dar.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata yakiwepo nani kijijini anaweza kununua nguo moja laki au hata elfu 80 kwenda juu huko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom