Wazo: Eneo la Makaburi ya Viongozi na Mashujaa ya Kitaifa Haliko Tayari Dodoma?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
Watanzania wenzangu poleni kwa msiba wa Mzee Mkapa. Tunapoendelea kuijenga Dodoma Kama Makao Makuu, ule mpango wa kuwa na eneo la Makaburi ya viongozi na Mashujaa wa Kitaifa ulifikia wapi? Sidhani Kama mfumo wa kuwazika Viongozi/Mashujaa kila mtu kijijini ni endelevu kwani watasahaulika na kukumbukwa na watu wa kwao.

Mfano Edward M. Sokoine wengi hawajapata na hawatopata nafasi ya kutembelea Monduli. Hilo ni kweli hata kwa Mwalimu Butiama au kwa Dr. Omar Ali Juma na Mzee Marine, Kawawa, n.k. Tunawazika ili kuwasahau!?

Kwanini tusianzie na Mzee Mkapa na baadaye kuhamisha Mikki ha Viongozi na Mashujaa huko Dodoma? Huko mbeleni watu wakienda Dodoma wanaweza kuzuru Makaburi ya viongozi wetu na hata Mashujaa wa kale ( tukihamishia makaburi huko)...tujenge na Maktaba Kubwa itakayotunza historia ya Marais (presidential library) katika eneo Hilo.

Tuanze na Marehemu Mzee Mkapa....RIP
 
Wanapendelea wakawazike makwao sababu ndipo miungu yao ilipo.

Waliofika butiama wanajua naongea nini, kuanzia ardhi ya pale, milima, anga, hali ya hewa n.k

Wazikwe tu makwao, hakuna la maana ccm walotenda ktk hii nchi mpaka ifike hatua ya kukumbukwa. Hata uyo sokoine walimuondoa haohao.
 
Nakumbuka kama Mheshimiwa Rais alisema yeye atazikwa Chato. Mjadala na mradi ukaisha.

Na hilo la Maktaba ndio kabisa. Huko Marekani kila Rais anajenga Maktaba yake ambayo pamoja na kutunza kumbukumbu inajihusisha na mambo ambayo alikuwa anapendelea. Mahali pa kujenga hiyo Maktaba ni uamuzi wa Rais mara anapoachia ngazi. Sisi tunawajengea nyumba na ninadhani wameridhika hivyo maana wangetaka Maktaba wangesema.

Amandla..
 
Magufuli aliliongelea siku moja hili. Yeye alisema kila mmoja atazikwa sehemu yake aliyotoka na hakuna umuhimu wa kuwa na sehemu moja.
 
Nakumbuka kama Mheshimiwa Rais alisema yeye atazikwa Chato. Mjadala na mradi ukaisha.
Na hilo la Maktaba ndio kabisa. Huko Marekani kila Rais anajenga Maktaba yake ambayo pamoja na kutunza kumbukumbu inajihusisha na mambo ambayo alikuwa anapendelea. Mahali pa kujenga hiyo Maktaba ni uamuzi wa Rais mara anapoachia ngazi. Sisi tunawajengea nyumba na ninadhani wameridhika hivyo maana wangetaka Maktaba wangesema.

Amandla..
Miaka miwili nyuma nilipendekeza nasi tuwe na maktaba na makumbusho ya urais.

Maktaba na Makumbusho ya Urais [Presidential Libraries & Museums]

Maktaba na Makumbusho ya Urais [Presidential Libraries & Museums]
 
Nakumbuka kama Mheshimiwa Rais alisema yeye atazikwa Chato. Mjadala na mradi ukaisha.
Na hilo la Maktaba ndio kabisa. Huko Marekani kila Rais anajenga Maktaba yake ambayo pamoja na kutunza kumbukumbu inajihusisha na mambo ambayo alikuwa anapendelea. Mahali pa kujenga hiyo Maktaba ni uamuzi wa Rais mara anapoachia ngazi. Sisi tunawajengea nyumba na ninadhani wameridhika hivyo maana wangetaka Maktaba wangesema.

Amandla..
Maktaba hizo huwa chini ya Ungalizi wa Makumbusho ya Taifa ( National Arc hives)
 
Back
Top Bottom